Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania


Huku nje hata ukifia nyumbani lazima upelekwe hospitali ili wakathibitishe kifo. Najua kwenye ukimwi kuna usiri juu ya ugonjwa lakini je kuna siri hata kwenye kifo?

Mtu anaweza kufariki na ndugu zake wa karibu sana akiwemo mamake asijulishwe mpaka baada ya siku tano? Eti walikuwa wanasubiri kuijulisha Ikulu kwanza? Nosense, halafu watu hao hao wanakuja na marungu kuishambulia Ikulu hiyo hiyo, haimake sense kabisa.
 

Mkuu ES,

Kulingana na dataz zaidi ni kwamba aliyezaa na Ballali hakuwa mke wa kwanza. Mke wa kwanza wa Ballali ni mama mmoja kutokea Mbeya. Bahati mbaya hawakufanikiwa kupata mtoto.

Yule wa USA ni mke wa pili na mama Muganda ni wa tatu.

Kule Boko mpaka sasa hata baadhi ya ndugu na marafiki wamezuiwa kwenda kwenye msiba. Ni kama ndani hakuna msiba.

Swali lingine imekuwaje waseme alifariki tarehe 16 huku wanajua alifariki tarehe 18? Ni kitu gani kinafichwa hapa?

Pia inabidi utofautishe kuona mwili na kuona jeneza. Sefui na waalikwa wengine waliona jeneza na wala sio mwili. Siku ya mazishi hakuna aliyeoona mwili wa Ballali.

Tuendelee kupeana data. Ila mimi kwanzoni sikuamini kwa asilimia 95, sasa siamini kwa asilimia 99, BALALI HAJAFA, tunapigwa michanga machoni.
 
Poleni vijana na wazee wote mnaokuna vichwa kwa kifo cha Balalli,mie naona hamuendi systematic katika uchunguzi wenu na nashauri mngerudi nyuma na kuanzia kwenye swali la MKJ. KUWA SAFARI YAKE YA MWISHO KWENDA DODOMA ALIAMBATANA NA NANI? NA ALIPOKUWA NJIANI AKIRUDI DAR ALIKUWA NA NANI? NA JE NDANI YA NDEGE MLIKUWA NA CHAKULA GANI?kwani baada ya hapo ndipo ugonjwa wa tumbo ulipoanza then connect the dots............
 
Hii habari ya kifo ilikuwa complex kuanzia mwanzo na wengine tulisema kuwa kila mtu ana uhuru wa kuhoji kupata ukweli kwa kuwa habari haiko dhahiri not crtstal clear at all na pia hakuna anayeweza kupinga anachosema mwingine mpaka mpingaji adhibitishie amnachoamini ni sahihi.Kwa hiyo uko sahihi mtoa maada kutaka vielelezo mwanana ingawa umefanya hivyo kwa kuchelewa ukilinganisha na watu kama wakina MUSHI mliokuwa ukiwampinga kwa kutaka wazibitishiwe kwa maana waliona utata ktk mwenendo uliokuja kuitwa kifo cha Balali.Ok unadai umefanya kauchunguzi kiasi big up .Kwa kifupi niko na maoni kama yako yaani tuko pamoja.

Huko nyuma niliandika https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=204724#post204724
 
Ahaa! Ni yale mambo ya "PRISON BREAK" -- Ballali in the place of VP's/President's brother. Niliambiwa na mtu kuwa kuna watu ktk siri-kali ya Tz waliobobea ktk masuala ya "MISINFORMATION".

Tutashuhudia zaidi wimbi la viongozi kujiuzulu kwa hili, lkn kwa kisingizio kingine.
 
Kama balali hajafa basi huko kwetu huko tunaita uchuro! basi kajichuria na atakufa kiukweli sooner.

Hilo mbona liko wazi, atakufa kwa kuuwawa na hao hao waliomshauri abadilishe ID, Huyu sasa ndio "Bangusilo" wa ukweli, wengine wote ni feki.
 
Balali and the political spin. Picha wanazo wao, marehemu walimuona wao, kuumwa aliumwa kwao.
Sina arguments zaidi mpaka next week nikimaliza research zangu.
 

Kwahiyo...............?????
 
Mkuu FMES kwanza niseme mpaka sasa sina tatizo na source zako. Niliposoma mwanzo ilionekana Balali alikuwa amepona muda mrefu mpaka alipokufa gafla Jpili iliyopita.

Gavana wa BoT yeye amesema aliendelea kuwasiliana na Balali mpaka pale hali yake ilipoanza kudhoofika/kudorora. Inatakiwa hapa haulizwe tena tarehe zipi.

Mkuu Jasusi(ambaye tangia juzi nimekubalia hoja zake) yeye amesema kwamba walimuuguza mgonjwa kwa kipindi cha miezi tisa, mpaka hapo alipofariki dunia.

Mgonjwa ni huyo huyo mmoja. Hapa mimi pamoja na kukubaliana na kila kitu nataka kujua nani hapa anaongea ukweli? Au wote wanaongea ukweli tatizo ni jinsi ya kupangilia maneno.

Lakini labda cha mwisho waliohudhuria mazishi naamini hawakuwa wengi sana, hili kuondoa mikanganyiko hii ambayo hata familia ilijua kuwa itatokea, kwa nini hata hao hawakurusiwa kuangalia mwili wa marehemu? Mbona hata viongozi wakuu wa nchi wakifikia kipindi kama hicho huwa walioudhuria wanaruhusiwa kuangaliwa/kutoa heshima za mwisho?

Anyway hatutaki kuwaumiza wafiwa ila tunataka rekodi zetu ziwekwe sawa hili tuendelee na mengine.
 
Familia ya mke wa marehemu, ni kubwa sana nafikri kama sikosei kwa wale tuliowahi kufika Musoma, hawa ni next almost to familia ya Mwalimu, kwa heshima ya African Clan, wametokea kwenye very strong family values kwa sababu baba yao alikuwa kiongozi mkubwa sana wa dini ya Christianity kule, watoto wote wamesoma sana isipokuwa mmoja tu wa mwisho, ni familia inyoheshimika sana kwa ujumla, ni watu very objective na kwa wale tunaowajua kwa kairibu ni watu wenye very strong mind na very independent kwamba sio rahisi kuwafanya wote wakubali kunyamaza wakati wanajua ukweli kuwa ni tofauti na unaosemwa,

Ina maana kuwa baada ya yote haya, Balali na mkewe wataendelea kusihi kama kaiwada, hao wazungu marafiki zao wa IMF wataendeelea kuwatembelea kama kawaida, kina Sefue wataendelea kushirikiana nao kama kawaida,

Halafu Mkuu Freeman, ambaye wengi tunamtegemea kuja kuwa rais wetu one day, na yeye amepoteza muda wote huu kuilaumu serikali kwa kitu ambacho anajua kuwa sio kweli, akakubali kuweka credibility yake na sisi wananchi at stake kwa kuwaheshimu sana familia ya Balali kuliko sisi wananchi, kwa sababu familia hiyo imemuahidi kuwa Balali hatakuja kuonekana tena maana watamficha vizuri sana?

Halafu watoto wa familia nzima ya watu wa Balali na Muganda waliokuwepo kwenye msiba mpaka mazishi, na wao pia wataendelea kuelimishwa kila siku kuwa uncle Balali hajafa ila tulikuwa tu tunadanganya for a good reasons, kwa hiyo msishangae mlipokuwa watoto tulimzika that was not him ila tulikuwa tunadanganay tu!

It does not make a sense at all!
 
and it wont make sense in the near future!
 
Well, It is about being sure 100% .
Nimefurahishwa na msemo mpya .Serikali ya Ki zecomdy.
 
Mwafrika wa Kike napenda kuunga hoja yako kwa 100% ni ukweli mtupu uliosema hapo juu.Hapa nyumbani kuna maswali mengi yanayo kosa majibu kama BoT kujichanganya na msemaji wa Ikuli Lweimamu......kwa hiyo tunakosa majibu.
 

FMES,

Imagine source za info zote ni kutoka sehemu moja, unategemea Mbowe angesema nini?

Ninachomlaumu Mbowe mimi ni kuchanganya mambo ya chama na familia. Hili suala kwenye chama angemwachia mtu mwingine kushughulikia.

Kama wamefake kifo cha Ballali, unasema tena ataendelea kukutana na nani? HAPANA, mtu kama amefake kifo ndio inakuwa mwisho wa kukutana na marafiki wa zamani.

Kama ballali hajafa basi wanaojua ukweli ni watu wachache sana na huenda hata ikawa yeye na mkewe tu, wengine wote ni ile ile ya kuamini wanayoambiwa.

Yaani hata siku ya kufa watu wanasema tarehe tofauti.
 
sasa natangaza rasmi kuwa napenda kuungana na MWafrika wa kike kwa kusisitiza tena kuwa BALALI HAJAFA


Social Security Death Index Search Results
81,529,674 Records
last updated on 5-20-2008 The key to your research
Join Ancestry.com Today!



The most full-featured SSDI search engine on, the internet

Field Value Records Results
Last Name BALALI 0 0
First Name DAUD Scanned
Middle Name T Scanned

Nothing found
Sasa hapo ndio sijui kama hiyo result ni kweli au si kweli ila hakuna rekodi ya mtu anaeitwa Daud T balali kuwa amefariki. naenda kuguguli tena.
 
watuambie tu hospitali gani imethibitisha kifo chake, yalobakia tutafanya wenyewe...
 

Balali kafa. "Akifufuka", atakuwa mtu wa pili kufanya hivyo baada ya Yesu Kristo!
 
Hivi, hao devil, I mean Devol mortuary si inabidi/wanaweza kuona maiti? Maiti inapokuwa inatunzwa si wanatunza kwa madawa? Kwahiyo ina maana mchezo (kama umechezwa) umechezwa na mortuary pia au nurse aliyedunga madawa? Kwahiyo kama sio mwenyewe, ina maana kuna maiti imenunuliwa?

Its possible to fake it, ila leaks mnazoacha kina MKJJ, FMES, MWK etc itaangusha credibility yenu na board. Tangazo la uhakika la Invisible siku ya kwanza, na mnavyochanganyana humu, inatia wasiwasi hii board.

Whattever propaganda you guys are on..........mmmh!!
 

Pamoja na respect zote, mabosi wote wa IMF walijua vizuri balali alichokifanya Tanzania na wote waliendeleza heshima hiyo hiyo waliokuwa nayo kwake mpaka kufa kwake.

Balozi wetu pamoja na kujua yote yaliyotendeka Tanzania aliendelea kuwasiliana naye vizuri tu na kumtembelea kama baadhi walivyosema hapa.

Watoto wake wenye misimamo/walisoma na kuelimika saana walijua yote kuwa Balali anatafutwa na watanzania mpaka sasa hakuna aliyejitokeza hata kumuuliza ilikuwaje hata wakfahamisha jamii ya watanzania tukajua kulikoni, ili tusiendelee kumuandama?

Kwa nini hawakutumia usomi wao, Hata hawakumsaidia kumpeleka ktk vyombo vya kisheria vya kimatifa hili asiendelee kuandamwa? maana alikuwa na madocument kibao.

bado kuna ka-mshikeli fulani fulani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…