Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

MwanaHaki, heshima mbele.

Viongozi wa wajuu wakija kuwa private citizen haimaanishi contact na Serikali zinaisha. Mpaka leo kina Msuya na Sumaye wanahudumiwa na Serikali. Kikiwatokea kitu, utategemea familia zao ziwafahamisha Serikali. Ballali alikuwa ana kila sababu ya kuendeleza contact na Serikali. Moja wapo ikiwa Serikali bado ilikuwa inalipia matibabu yake hata baada ya kufukuzwa kwa sababu za kimkataba, tuliambiwa. Na hata baada ya kufa, mkewe Anna Muganda, ambaealisha fanya kazi Ikulu, anajua itifaki za kuendeleza contact na Serikali. Moja ya sababu hapa napo inahusu "mshiko." Kuanzia May 16, Cheki zote za pensheni na mafao yaliyobaki ya Ballali yataanza kuelekea kwa mjane. Kwa hiyo, Anna Muganda knows better than to stop contacting the gov't to say, hey look here people, change the mailing address, your guy is dead!

Ballali ni raia wa US? Moja ya matundiko machache juu ya lako limeweka rekodi ya Serikali ya Marekani, kupitia Balozi Green, kutangaza kwamba Ballali hakuwa raia. Sasa jamani sijui utata uko wapi hapa.

"Nani kati yetu ameshuhudia majivu..."? Kati yetu nani, Mtanzania yeyote au 'doubting Thomasses' wa JF? Wapo Watanzania ambao walikuwepo kwenye mazishi. Wewe na mimi hatukuwepo, lakini hiyo haisemi lolote kuhusu kufa au kutokufa kwa Ballali. Hiyo inatupa tu haki ya kusema mimi nina "shuku za Tomaso" Lakini "shuku za Tomaso" ni za Tomaso, na hazipunguzi kesi ya aliye dai Mtume kafa eti kwa sababu Thomaso mpaka aguse alama za mateso kwenye mbavu ndio aache kubisha!

Na swala la "Will," hilo ni la kifamilia. Ni mkataba kati ya mfiwa na mfu wake. Ni mpaka hapo litakapo zuka jambo na wafiwa fulani kulalamika ndio wengine, kama vile mahakama, wanaweza kuingilia kusema leteni tuone "Will." Sisi hatuwezi kudai hii Will sasa hivi. Kisheria wanasema hatuna "privity" na huu mkataba. Hautuhusu!

Huu msiba unawachanganya Watanzania, nadhani, kwa sababu ya tofauti za kiutamaduni. Mama Muganda hapa ana exercise haki za watu wa Magharibi. Desturi zinazo heshimu Private Rights, ambazo sisi labda hatuna. Lakini kwa kweli sio za ajabu sana hizi rights, na kuna wakati zina make sense. I mean, masuala ya EPA na ya kuthibitisha kifo yanakuhusu. Lakini vipi kama humo ndani, zaidi ya kuongelea mazishi na kugawanya mali, pia ana msihi mmoja wa Binti zake, kwa mfano, aache uasherati? Mpaka na sisi tujue? Well, wote tukijua inaweza ku defeat the purpose of the "Will" kwa sababu kuna Wana Haramu wanaweza kuanza kumtafuta haraka huyo aliyepewa Wosia kama huo kabla haujamkaa kichwani!

Sikusema Ballali atapata matunzo kama ex-Presidents and PM's. Soma vizuri nilicho sema. Kwanza nimeeleza kwanini Private Citizen haina blanket meaning kwamba contact zote na Serikali ndio zimekwisha. Nikatoa mifano ya Mawaziri Wakuu kuendelea kutunzwa (hizo ni contacts baina ya Serikali na Private Citizens wastaafu). Halafu nikaja specifically kwenye ishu ya Ballali, ambae nimesema mkewe ataendelea kupokea pensheni na mafao "yaliyo baki". Umeona nilitumia maneno "yaliyo baki"? Ex-Pres na PMs' wanatunzwa maisha, hakuna cha "yaliyo baki." Kwa hiyo nilicho kieleza kilikuwa sahihi, na lugha niliyo tumia ilikuchukuliwa tahadhari.

Those are your words naona unakula matapishi yako sasa.
 
Those are your words naona unakula matapishi yako sasa.

Wewe Dua naona aidha huelewi elewi ukisoma, au unafanya makusudi. Sasa ni hivi, I got bigger fish to fry. Godspeed.
 
Wewe Dua naona aidha huelewi elewi ukisoma, au unafanya makusudi. Sasa ni hivi, I got bigger fish to fry. Godspeed.

Ha ha ha .........yamekuwa haya tena, We gona wait for the fish. When is ready just let us know......
 
Nakunukuu:

"Kwa suala la Ballali tayari alikuwa USA wakati visa yake ilivyokuwa revoked, kwahiyo ilitosha tu kuwaambia hao immigration kwamba yeye amerudi kimoja USA na anataka kuendelea na green card yake. Kwasababu yeye bado ana nyumba USA, familia yake iko USA, ana mapesa mengi tu ya kuishi USA, na kikubwa hana criminal record, nina uhakika hiyo green card wangemrudishia bila matatizo yoyote."

Umesema nini hapo? Wangemrudishia Green Card right?

Ndugu sijakurupuka bure. Ni wewe uliharakisha kunambia eti sielewi mambo ya immigration. Wasafiri tutaacha kujua mambo ya Visa bwana?
HAPA KUNA UPOTOSHAJI MKUBWA SANA.YEYE HAKUFUKUZWA MAREKANI BALI BAADA YA KUTOLEWA UGAVANA KWA AIBU ALIONDOLEWA DIPLOMATIC PASSPORT AMBAYO INGEMPASA AOMBE VIZA KWA PASSPORT MPYA MARA ATAKAPO INGIA MAREKANI BAADA YA KUTOKA.LAKINI KWA KUWA HAKUTOKA HAIMLAZIMISHI KUOMBA KWA SPEED HIYO MNAYOTAKA NYIE.
 
Kufa kwa Balali ni faraja kubwa kwa nchi yetu ya tanzania,nadhani ni Mungu mwenyewe katuokoa na janga hili nla kutaka kuwadhalilisha viongozi wetu kwa ajili ya vipes vidogo sana.Nenda Balali,shujaa wa nchi yetu,umeweza kufa kwa ajili ya nchi yako na umeweka siri za ndani moyoni mwako mpaka mwisho,hakika wewe ni shujaa wa kweli.
 
Hiyo ni sumu ya ufisadi. Kama kulishwa sumu atakuwa kalishwa na mtu wake wa karibu kupitia serikali au tuseme B.N ,R.A yeyote yule.Msiba wa kiswahili haukosi sababu hata kama amekufa kwa maradhi yake ya kawaida watu wataangalia mazingira yaliyogubika mpaka akafikia umauti pasipo kuwa na ushahidi wowote wa kisayansi. Na ndio maana katika mazingira hayo utasikia fulani kafa kwa sababu kalogwa na bibi yake au babu yake tubadilike jamani. Hata kama kalishwa sumu fuatilieni postmortem report kutoka kwa daktari. Tusianze kubashiri kwa hisia tutumie vigezo. Ni kweli Ballali anahusishwa na upotevu wa mamilioni ya EPA enzi za uongozi wake lakini inawezekana kwamba yeye alitumika kama chambo tu na sasa kumnyooshea mtu mmoja kidole kama ndiye anahusika itakuwa ni makosa na ndiyo maana hata mimi sikuwa specific kumtaja mtu fulani mwanzoni mwa comment yangu. Kama atakuwa kalishwa sumu basi mtambue serikali ndiyo inahusika na siyo huyo mhusika aliyetajwa.Hizo kitaalam twaziita collateral damage mmoja anatolewa kafara kwa ajili ya wengine na kwa taifa. "Samaki mmoja akioza na wote wameoza" Hakuna fisadi mmoja kwa sababu kwa namna moja au nyingine mtu aweza kukataa kuwa yeye hahusiki lakini kumbe vile vichembechembe vya EPA navyo vimempitia hiyo ndiyo Tanzania yetu. Mfumo wote ni corrupt kwa hiyo hakuna wa kumnyooshea kidole hata huyo RA naye anasupport yake kwenye system hivyo kumpoint yeye moja kwa moja ni makosa.
 
... huwezi kutumia permanent residence yako au green card pamoja na diplomatic passport. Sheria zote za green card zinakataa. Hivyo huyo mtu anaombewa visa kama kawaida.

...Nilisoma statement ya Green, kwa kweli ilikuwa na utata mkubwa na pia inaficha ujumbe nyuma yake. Kama nilivyosema mwanzoni ukirudi kwenu kwa kazi ya muda mrefu inatakiwa upoteze haki ya green card, labda hicho ndio alikuwa anaongelea Balozi, lakini kupoteza huko sio permanent, hali ikibadilika unaweza kurejeshewa kwa muda mfupi sana.

Nimesoma ile case ya UK. Lakini ishu hapa sio re-entry baada ya kupoteza PR. Ishu ni hizo claims zenu kwamba unahitaji Visa mbili, kama ulivyo elezea hapo juu.

Tafuta hiyo sheria inayosema ukiwa na Permanent Resident Visa huwezi kuitumia kwenye Diplomatic Passport na unahitaji Visa nyingine. Balozi wa US kasema huhitaji Visa mbili. We unasema unahitaji, na kwamba walio sema Ubalozi yana utata, yameficha vitu. Na ukasema Sheria zote za Green Card zinakataa. Naomba hizo Sheria.
 
HAPA KUNA UPOTOSHAJI MKUBWA SANA.YEYE HAKUFUKUZWA MAREKANI BALI BAADA YA KUTOLEWA UGAVANA KWA AIBU ALIONDOLEWA DIPLOMATIC PASSPORT AMBAYO INGEMPASA AOMBE VIZA KWA PASSPORT MPYA MARA ATAKAPO INGIA MAREKANI BAADA YA KUTOKA.LAKINI KWA KUWA HAKUTOKA HAIMLAZIMISHI KUOMBA KWA SPEED HIYO MNAYOTAKA NYIE.

Ha ha haaaaaaaa. Sasa huo hapo juu ndio upotoshaji. Man it's crazy. LOL!
Umeyapata wapi hayo?

Hata hivyo, Mchawi, pale awali nilikuwa namnukuu mtu ndani ya tundiko langu. Sio maneno yangu yale. Soma juu yake, nimesema naukuu. Na chini ya nukuu nikaendelea na maneno yangu. Kwa hiyo, upotoshaji kama ulikuwepo, haukuwa wa kwangu. LOL!
 
Kufa kwa Balali ni faraja kubwa kwa nchi yetu ya tanzania,nadhani ni Mungu mwenyewe katuokoa na janga hili nla kutaka kuwadhalilisha viongozi wetu kwa ajili ya vipes vidogo sana.Nenda Balali,shujaa wa nchi yetu,umeweza kufa kwa ajili ya nchi yako na umeweka siri za ndani moyoni mwako mpaka mwisho,hakika wewe ni shujaa wa kweli.

Kweli wewe ni mchawi
 
Nimesoma ile case ya UK. Lakini ishu hapa sio re-entry baada ya kupoteza PR. Ishu ni hizo claims zenu kwamba unahitaji Visa mbili, kama ulivyo elezea hapo juu.

Tafuta hiyo sheria inayosema ukiwa na Permanent Resident Visa huwezi kuitumia kwenye Diplomatic Passport na unahitaji Visa nyingine. Balozi wa US kasema huhitaji Visa mbili. We unasema unahitaji, na kwamba walio sema Ubalozi yana utata, yameficha vitu. Na ukasema Sheria zote za Green Card zinakataa. Naomba hizo Sheria.

KM,

Naona tone imebadilika labda unaanza kugundua makosa yako. Kwenye mambo ya visa
entry na remain yanaongozana na sheria zinazofanana, kinachotofautiana ni wapi suala lako limeshughulikiwa. Kwa mfano ukiombea PR kwa hapa UK inaitwa indefinite leave to remain wakati ukiombea nje ya UK inaitwa indefinite leave to enter. Ni kitu kile kile ila tofauti ni wapi umeombea.

Sasa ukija kwenye PR kama ni UK inagongwa kwenye paasport kama passport unayo. Ikitokea baadaye ukapata diplomatic passport unaweza kwenda kuomba hiyo visa igongwe humo. Ila utakuwa mjinga maana ukipoteza hiyo diplomatic passport itabidi ukaombe tena igongwe kwenye passport nyingine pia unaweza ukawa umejichongea na hivyo kunyang'anywa hiyo ILR. Wenzako wanachofanya ni kwamba wakipewa diplomatic passport na kama wanasafiri basi wanomba visa kwa kutumia hizo diplomatic passports, kwanza hawalipi wao, pili hawaendi kujipanga queue wao, kuna watu wanawafanyia na tatu chance ya kunyimwa ni ndogo sana.

Kama wewe unafuata sheria, inatakiwa uwaambie home office kama ni UK kwamba wewe umerudi nyumbani ili waifute hiyo PR yako. Lakini ukweli ni kwamba kama kuna watu wanafanya hivyo, basi ni wachache mno. Walio wengi wanakaa nazo mpaka authority ikiwaambia kwamba haziko valid tena. Walio wajanja wanazitumia hata mara moja kwa mwaka ili kuhakikisha bado ziko valid.

Sasa kama Ballali alikuwa na green card ni wazi hakuirudisha. Akaendelea kukaa nayo huku akitumia diplomatic passport yake. Siku alipopoteza kazi angekuwa TZ ingetakiwa atumie passport ya kawaida na labda na hiyo green card kwenda USA. Ili asirudishwe mpakani angeweza kwenda ubalozi na kuomba entry clearance kwa kutumia sababu ambazo tumezijadili hapo juu ikiwemo familia yake kuwa USA. Lakini kwasababu alikuwa tayari USA wakati anafutiwa visa basi hapo ni yeye kutumia lawyer wake tu kwenda kuhakikisha green card yake inakuwa valid. Kwa mwingine wala asingehangaika na angeendelea kukaa tu.

Lazima pia ujue kwamba kwa mfano ingelikuwa kwa UK, hata kama wangemnyang'anya ya kwake, angeomba nyingine pale ubalozi wangempatia permanent residence nyingine kwa kutumia PR ya mkewe, yaani angepewa indefinite leave to enter, ambayo ni kitu kile kile.

Njia pekee ya kumfanya Ballali apoteze hizo haki zake ni kama serikali ya TZ ingemshitaki na kumhukumu, vinginevyo hata USA hawakuwa na sababu ya kumnyima nafasi ya yeye kuungana na familia yake na kuendelea kukaa USA.
 
But hawa wazee wa kihehe ni balaa

wanaweza shusha kila mmoja aliyeshiriki...
 
Hivi ni kweli hawa wazee wanaweza kushusha galika??kwa maana nakumbuka hata wale wazee wa Lupembe kuhusu kifo cha Amina Chifupa walisema hivi hivi nashangaa kimya mpaka leo....itakuwa biti tu ila kule Nyumba nitu mhhh sijui kama mtu atapona hapo.
 
Wazee Wa Iringa Watoa siku 30 kwa muuaji wa Ballali!

Wazee wa kihehe wametoa siku 30 kwa aliyehusika kwa njia moja ama nyingine na kifo hicho, kujisalimisha kijijini Luganga, Mufindi mkoani Iringa alikozaliwa gavana huyo la sivyo wamedai patakuwa hapatoshi.
Hayo yalizuka baada ya mwili wa aliyekuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BOT Dk. Daudi Ballali kuzikwa huko Washington, Marekani Ijumaa iliyopita.

Wakizungumza na waandishi jana kwa niaba ya wenzao, waliojulikana kwa jina la Mzee Samweli Kalinga (76) na Yohanes Kalinga (85), walisema wataamini kuwa mtoto wao amekufa baada ya kupata ufafanuzi wa kina kupitia kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu kifo hicho la sivyo haiwaingii akilini kabisa.

Timu hiyo ya Wazee hao wanaotoka kijiji cha Luganga na Mtwango, wameiomba serikali ifanye uchunguzi wa kina juu ya kifo hicho na kufanya kila linalowezekana kurejesha mwili huo nchini, na kama itashindikana ilete mchanga wa kaburi hilo ili wafanye mazishi ya kimila hapa nchini.

Walisisitiza kwa kusema sema kama wao ni wazee wa siku nyingi wa kijiji cha Luganga na Mtwango, wanashindwa kuamini kuwa mtoto wao amekufa, wataamini jambo hilo baada ya kuona maiti au picha yake akiwa amekufa.

Mzee Samweli alisema taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari hazitoshelezi kuamini kuwa ni kweli mtoto wao kipenzi, Dkt. Ballali amekufa hivyo ameiomba serikali kuunda tume haraka kuchunguza mazingira ya kifo cha gavana huyo wa zamani.

Alisema moja ya sababu inayowafanya waendelee kuamini kuwa Dkt. Ballali bado mzima ni mazingira ya sasa ya nyumbani kwao kijijini Luganga na nyumbani kwa baba zake wadogo eneo la Ziroziro, Mtwango.

"Nimeishi Mtwango tangu utoto wangu sijawahi hata siku moja kuona nyumba yenye msiba haina waombolezaji nah ii ni dalili ambayo itaendelea kutustua mpaka tutakapothibisha kwa kina", alisema Mzee Samweli

Alisema kwa mujibu wa taratibu za kihehe, msiba unapotokea huombolezwa siku tatu mfululizo ama zaidi ambapo kwa muda huo, majirani hukusanyika nyumbani kwa wafiwa kuwafariji lakini hali hakuwa hivyo baada ya taarifa hizi kufika hapa kijijini.

Aliongeza Mzee huoy "Tunaomba kuelezwa ugonjwa uliosababishia kifo cha mtoto wetu na jitihada zilizofanywa na serikali kuokoa maisha yake... Tunashindwa kuelewa serikali inapotoa pole wakati iliwahi kusema Ballali hajulikani alipo", alisema Mzee Samweli.

Kwa upande wake Mzee Yohanes alisema wanafanya mpango kukutana na ndugu wa marehemu kufanya tambiko la aina yake la kifo hicho na kuomba dua maalum kulaani kifo hicho kama kimetokana na 'mkono wa mtu'.

Mzee huyo, alisema wametoa siku 30 kwa watu waliohusika kwa njia moja ama nyingine na kifo hicho kujisalimisha kijijini hapo, vinginevyo watu hao hawatadumu kwenye nyadhifa zao.

Alisema iwapo kifo hicho kimetokana na mapenzi ya Mungu basi wanamshukuru kwa kutimiza matakwa yake na kama ni kwa mipango ya shetani na wanadamu, basi itashughulikiwa ipasavyo.

Pamoja na mwili huo kuzikwa Marekani, wazee hao wameiomba serikali kufanya kila linalowezekana kuurejesha nchini, ikishindikana waletewe mchanga wa kaburi lake ili wafanye mazishi kwa mujibu wa mila za kihehe, Luganga alikozikwa baba yake mzazi Mzee Timoth Ballali aliyefariki dunia Aprili 3 mwaka 2000.

"Hata kama imeshindika kuleta mwili wake basi wasafirishe mchanga wa kaburi tuje tufanye mazishi kwenye makaburi ya Luganga alipolala baba yake mzazi. Kumzika Marekani ni sawa na kumtenga
 
Jmushi1,

Usanii tu mwingine huo, kama wana uwezo huo si wangemlinda mwanao asiuawe?

Nini bora? kulinda mali yako au kuja kulipiza kisasi?
 
Mkuu wangu Mtanzania, darasa zito sana endelea tu kuelimisha taifa mkuu, kuna tunaonufaika sana huku pembeni,

Ndio maana I love JF, bila ya vichwa kama vyako tungelishwa logic hapa mpaka tulewe bila ya kunywa ugimbi wenyewe, nawaona wanajaribu kuchanganya majina yao mengi ili washinde lakini wapi facts zinazidi kuwapiga chenga, mkuu Matanzania weka darasa hapa, na tuko ukurasa mmoja!

Mungu Aibariki JF!
 
Kada nilikwambia mwanzo mwa mwaka huu kuwa huu mwaka wa ukombozi na mtakuwa na hali ngumu sana kwani kila siku yataibuliwa mengine mengi, washauri waache kusema uongo kwanza, the watueleze kwanini walificha balali alikuwa anaumwa nini, alilazwa hospitali gani, alikufa lini, na kwanini hakurudishwa nyumbani kwa mazishi. Usimlinganishe balali na watu wengine balali alikuwa gavana na alikuta mtuhumiwa mkuu wa EPA.

serikali ifiche kwani ballali alikuwa employed na serikali tu wakati wote hadi kufa kwake ? na lazima ujue tofauti kati ya serikali (taifa) na ccm (chama) ! ni kweli wakati ni mgumu lakini sio kwa sababu mambo yanaibuliwa, bali ni daily challenges ambazo hata wewe unaziface katika maisha yako ! Mbowe anaongea kama mbowe mwanasiasa, hapo ndipo anapotegemea kufanikiwa wakati hadi leo sijui nini anachoongelea ! yaani ni blah blah !
 
Hivi ni kweli hawa wazee wanaweza kushusha galika??kwa maana nakumbuka hata wale wazee wa Lupembe kuhusu kifo cha Amina Chifupa walisema hivi hivi nashangaa kimya mpaka leo....itakuwa biti tu ila kule Nyumba nitu mhhh sijui kama mtu atapona hapo.

Una hakika? Usibishe sana. Hujui wameamua kuwashughulikia watuhumiwa kwa njia gani.
 
kuna watu hapa jf kazi yao ni moja kumshambulia mbowe hata kama hawajsoma between his lines, jaribu kufikiri hali ya upinzani hapa tz ingekuwaje bila akina mbowe, zito , slaa etc, bila shaka tungebaki na akina mrema, sasa hawa wachache ambao wako tayari kuiambila serikali wazi wazi kuwa wewe uko uchi, tunawabeza, kabla ya kuwashambulia hawa tujiulize sisi wenyewe tumeifanyia nini nchi yetu? je kwa kubadili majina na kuweka thread hapa jf inatosha? nani kati yetu angekuwa angalau tayari na kwa jina lake halisi kusema aliyosema mbowe, KWA SASA TUJIULIZE, EWE TAIFA LANGU NIMEKUKINDA NAMANA GANI DHIDI YA MAFISADI? NIJIBU, EWE TAIFA LANGU, UMENIPA ELIMU YA LUTOSHA, UMENIPA KAZI YA MAANA, NIMEKUFANYIA NINI CHA KUSHUKURU? NIJIBU, EWE TAIFA LANGU NINAPOKAA HUKU ULAYA AU AMERKA NAKUKUMBUKA NA KUKUTAMANI KAMA KUNGURU ANAVYOTAMANI VIJITO VYA MAJI, LAKINI EWE TAIFA LANGU KILA NIKIAMBIWA NIANDAMANE KUPINGAWATESI WAKO KAMA MAFISADI, MOYO WANGU UNAKUWA MZIGO, NIJIBU
 
Aseme nini? Anatafuta umaarufu tu wa kisiasa. Wenzie tunamlilia ndugu yetu yeye anataka kuleta mzaha. Hivi hawa wanasiasa wa Bongo hawajui kifo?
basi mbowe si aseme tu anachojua kuliko kusema mkono wa vigogo (awataje) !! hata kama anawasuspect ! otherwise nachukulia maneno yake kama politics ! yeye pia si alivunjika mguu wiki iliyopita, au kulikuwa na mkono wa vigogo ?
 
Nimesoma taarifa isemayo Bernad Membe, waziri wa mambo ya nchi za nje, amesema iwapo itathibitika kuwa serikali ndiyo iliyomuua Balali, basi atajiuzulu wadhifa wake.

Kimantiki, mtu mwenye madaraka hujiuzulu wadhifa wake kama hatua ya uwajibikaji ya kukiri kushindwa kwake kuyamudu madaraka hayo, ama kushindwa kutimiza malengo aliyowekewa, ama kwa kuthibitika kuwa amepoteza sifa ya kuendelea kuwa na madaraka hayo. Sasa kumbe kifo cha Balali kina uhusiano mkubwa kiasi hicho na nafasi ya Membe? Kwa kauli ya Membe mwenyewe, ndivyo anavyotusadikisha, kuwa pengine lilikuwa jukumu lake kuhakikisha kuwa serikali haimuui Balali, na kama ni serikali imemuua basi atajiuzulu kwa kushindwa jukumu hilo! Au ana jukumu la kuilinda siri hiyo, na kama atashindwa hadi ukapatikana ushahidi kuwa serikali ilifanya mauaji hayo, basi atajiuzulu. Au waliofanya mauaji hayo wako chini ya usimamizi wake, na ikithibitika hivyo atajiuzulu kutokana na makosa ya wasaidizi wake. Au ni nini basi? Siamini kuwa ni uropokaji tu!
 
Back
Top Bottom