Dua
JF-Expert Member
- Nov 14, 2006
- 3,236
- 669
MwanaHaki, heshima mbele.
Viongozi wa wajuu wakija kuwa private citizen haimaanishi contact na Serikali zinaisha. Mpaka leo kina Msuya na Sumaye wanahudumiwa na Serikali. Kikiwatokea kitu, utategemea familia zao ziwafahamisha Serikali. Ballali alikuwa ana kila sababu ya kuendeleza contact na Serikali. Moja wapo ikiwa Serikali bado ilikuwa inalipia matibabu yake hata baada ya kufukuzwa kwa sababu za kimkataba, tuliambiwa. Na hata baada ya kufa, mkewe Anna Muganda, ambaealisha fanya kazi Ikulu, anajua itifaki za kuendeleza contact na Serikali. Moja ya sababu hapa napo inahusu "mshiko." Kuanzia May 16, Cheki zote za pensheni na mafao yaliyobaki ya Ballali yataanza kuelekea kwa mjane. Kwa hiyo, Anna Muganda knows better than to stop contacting the gov't to say, hey look here people, change the mailing address, your guy is dead!
Ballali ni raia wa US? Moja ya matundiko machache juu ya lako limeweka rekodi ya Serikali ya Marekani, kupitia Balozi Green, kutangaza kwamba Ballali hakuwa raia. Sasa jamani sijui utata uko wapi hapa.
"Nani kati yetu ameshuhudia majivu..."? Kati yetu nani, Mtanzania yeyote au 'doubting Thomasses' wa JF? Wapo Watanzania ambao walikuwepo kwenye mazishi. Wewe na mimi hatukuwepo, lakini hiyo haisemi lolote kuhusu kufa au kutokufa kwa Ballali. Hiyo inatupa tu haki ya kusema mimi nina "shuku za Tomaso" Lakini "shuku za Tomaso" ni za Tomaso, na hazipunguzi kesi ya aliye dai Mtume kafa eti kwa sababu Thomaso mpaka aguse alama za mateso kwenye mbavu ndio aache kubisha!
Na swala la "Will," hilo ni la kifamilia. Ni mkataba kati ya mfiwa na mfu wake. Ni mpaka hapo litakapo zuka jambo na wafiwa fulani kulalamika ndio wengine, kama vile mahakama, wanaweza kuingilia kusema leteni tuone "Will." Sisi hatuwezi kudai hii Will sasa hivi. Kisheria wanasema hatuna "privity" na huu mkataba. Hautuhusu!
Huu msiba unawachanganya Watanzania, nadhani, kwa sababu ya tofauti za kiutamaduni. Mama Muganda hapa ana exercise haki za watu wa Magharibi. Desturi zinazo heshimu Private Rights, ambazo sisi labda hatuna. Lakini kwa kweli sio za ajabu sana hizi rights, na kuna wakati zina make sense. I mean, masuala ya EPA na ya kuthibitisha kifo yanakuhusu. Lakini vipi kama humo ndani, zaidi ya kuongelea mazishi na kugawanya mali, pia ana msihi mmoja wa Binti zake, kwa mfano, aache uasherati? Mpaka na sisi tujue? Well, wote tukijua inaweza ku defeat the purpose of the "Will" kwa sababu kuna Wana Haramu wanaweza kuanza kumtafuta haraka huyo aliyepewa Wosia kama huo kabla haujamkaa kichwani!
Sikusema Ballali atapata matunzo kama ex-Presidents and PM's. Soma vizuri nilicho sema. Kwanza nimeeleza kwanini Private Citizen haina blanket meaning kwamba contact zote na Serikali ndio zimekwisha. Nikatoa mifano ya Mawaziri Wakuu kuendelea kutunzwa (hizo ni contacts baina ya Serikali na Private Citizens wastaafu). Halafu nikaja specifically kwenye ishu ya Ballali, ambae nimesema mkewe ataendelea kupokea pensheni na mafao "yaliyo baki". Umeona nilitumia maneno "yaliyo baki"? Ex-Pres na PMs' wanatunzwa maisha, hakuna cha "yaliyo baki." Kwa hiyo nilicho kieleza kilikuwa sahihi, na lugha niliyo tumia ilikuchukuliwa tahadhari.
Those are your words naona unakula matapishi yako sasa.