Kifo cha Dkt. Magufuli tunajifunza nini?

Kifo cha Dkt. Magufuli tunajifunza nini?

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Poleni watanzania wenzangu kwa kifo cha Mpendwa wetu Hayati JPM, Apumzike kwa Amani.

Hakika kifo chake kimemgusa kila mtu, watu wote wa rika zote.

sijawahi kuona kiongozi analiliwa kama huyu, nyuso za watu wengi zimejawa na huzuni kubwa.

viongozi tuliobaki hai kuna jambo la kujifunza hapa, ni wazi kabisa Hayati Magufuli enzi za uhai wake alifanya kazi yake kwa nguvu zake zote na kwa masilahi ya watanzania. Amepambana bila kuchoka hadi umauti umempumzisha!

Viongozi tuliobaki tuna mambo yafuatayo ya kujifunza:

1. Kila kiongozi ktk nafasi yake ana wajibu wa kufanya kazi kwa uadilifu na kwa bidii kwa masilahi ya watanzania.
tuwajali na tuwatetee wananchi wanyonge.

2. Tupambane kulinda Rasilimali zetu haswa madini.

3. Lazima tupige vita dhidi ya mafisadi na wala rushwa

Kifo cha Dr. JPM kamwe kisiwe ndio kufunguliwa kwa mafisadi, wala rushwa, wabadhirifu, kujuana, kubebana, wapiga dili, mikataba mibovu, ukwepaji kodi, wauza madawa ya kulevya, wakwepa kodi, majambazi, vibaka n.k

Wananchi wa Tanzania tunataka kuona yale yote aliyo yasimamia Hayati Magufuli yanasimamiwa kwa nguvu zote bila kuoneana muhali.

Watanzania wanatarajia kuona heshima na utiifu ulio onekana kwa JPM pia unaonekana akipatiwa Rais wa sas Samia Suluhu.

Wananchi wanatarajia kuona watendaji wote wa vyombo vyote wana fanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu kama ilivyo kuwa wakati wa JPM, hatutegemei kuwa ona mawaziri na watendaji wengine waki relax.

Huwezi kuwa kiongozi Mwadilifu kama huna hofu ya Mungu. Magufuli alikuwa ni Kiongozi mwenye hofu kubwa kwa Mungu.
viongozi mlio baki kuweni na hofu kwa Mungu, hofu ya kweli ili Muwatendee watanzia haki.

Viongozi tuache tamaa ya kujilimbikizia mali na kuwa na Tamaa ya madaraka.

4. Hayati JPM alijenga Imani kwa wananchi, alisema na kutenda, ukiharibu tu hajili wewe ni rafaki yake lazima akutumbue, hakuna mambo ya kujuana mbele ya kazi ya watanzania.

5. Watanzania hawategemei kuona wala kusikia hujuma ya maendeleo kwa taifa letu.

Tumpe ushirikiano wa kweli sio wa kinafiki Rais wetu Mama Samia Suluhu ili nchi yetu iendelee kuwa na heshima.

Pumzika kwa Amani JPM, mwanga wa milele ukuangazie.
 
Tuzidi kuiomba neema ya Mungu.
IMG-20210320-WA0000.jpg
 
Kinatukumbusha kuwa kila mtu ataonja umauti. Hakuna atakayetoroka. Safari ameimaliza salama.
 
Mikoani Kuna taarifa za watu kukamatwa wakishangilia kifo chake. Hakika ameumiza wengi
Hamna lolote, uongo tu. Tunachoona mikoani ni watu kulia kumpoteza kipenzi chao. Tuletee ushahidi wa hayo unayoyasema!
 
Mikoani Kuna taarifa za watu kukamatwa wakishangilia kifo chake. Hakika ameumiza wengi
Wewe ndiyo labda unaumiza mengi. No wonder you chose an avatar from "I Go Chop Your Dollar". You character resembles "I Go Chop Your Dollar" movie. By the way how did you come to choose the avatar. Is it a glorification of Nkem Owoh's movies? Sometimes things (movies) you like may depict one's character. By the way there no $$$ to chop, President Mama Samia Suluhu is very awake and alert.
 
Na hao aliowaacha waache uonevu na kupendelea watu/upande fulani tu.
 
Wewe ndiyo labda unaumiza wengi. No wonder you chose an avatar from "I Go Chop Your Dollar". You character resembles "I Go Chop Your Dollar" movie. By the way how did you come to choose the avatar. Is it a glorification of Nkem Owoh's movies? Sometimes things (movies) you like may depict one's character. By the way there no $$$ to chop, President Mama Samia Suluhu is very awake and alert.
 
Back
Top Bottom