Kifo cha Dkt. Magufuli tunajifunza nini?

Kifo cha Dkt. Magufuli tunajifunza nini?

Acha kubisha bisha jambo usilolijua...

Kama kitu hujui haimaanishi kwamba hakipo...

Watu 8 wamekamatwa huko manyara kwa kusheherekea magu kufa.
Ulitaka wasikamatwe kwa walichokifanya ambacho ninuchochezi
 
Aliwachukia watu wa Kaskazini na haswa Wachaga, sijui walimfanya nini?

Tuishi kwa upendo, ukipewa uongozi usiwabague watu kwa rangi, kabila, jinsia wala dini.

Tenda mema, na kwa Wakristo unapaswa kufuata Amri 10 za Mungu ikiwemo usiue.

Sent from my HTC U12 life using JamiiForums mobile app
 
Poleni watanzania wenzangu kwa kifo cha Mpendwa wetu Hayati JPM, Apumzike kwa Amani.
Hakika kifo chake kimemgusa kila mtu, watu wote wa rika zote.
sijawahi kuona kiongozi analiliwa kama huyu, nyuso za watu wengi zimejawa na huzuni kubwa.
viongozi tuliobaki hai kuna jambo la kujifunza hapa, ni wazi kabisa Hayati Magufuli enzi za uhai wake alifanya kazi yake kwa nguvu zake zote na kwa masilahi ya watanzania,
Amepambana bila kuchoka hadi umauti umempumzisha!!

viongozi tuliobaki tunamambo yafuatayo ya kujifunza;

1. Kila kiongozi ktk nafasi yake ana wajibu wa kufanya kazi kwa uadilifu na kwa bidii kwa masilahi ya watanzania.
tuwajali na tuwatetee wananchi wanyonge.

2. Tupambane kulinda Rasilimali zetu haswa madini.

3. Lazima tupige vita dhidi ya mafisadi na wala rushwa,

Kifo cha Dr. JPM kamwe kisiwe ndio kufunguliwa kwa mafisadi, wala rushwa, wabadhirifu, kujuana, kubebana, wapiga dili, mikataba mibovu, ukwepaji kodi, wauza madawa ya kulevya, wakwepa kodi, majambazi, vibaka n.k

wananchi wa Tanzania tunataka kuona yale yote aliyo yasimamia Hayati Magufuli yanasimamiwa kwa nguvu zote bila kuoneana muhali.

Watanzania wanatarajia kuona heshima na utiifu ulio onekana kwa JPM pia unaonekana akipatiwa Rais wa sas Samia Suluhu.

wananchi wanatarajia kuona watendaji wote wa vyombo vyote wana fanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu kama ilivyo kuwa wakati wa JPM, hatutegemei kuwa ona mawaziri na watendaji wengine waki relax.

Huwezi kuwa kiongozi Mwadilifu kama huna hofu ya Mungu. Magufuli alikuwa ni Kiongozi mwenye hofu kubwa kwa Mungu.
viongozi mlio baki kuweni na hofu kwa Mungu, hofu ya kweli ili Muwatendee watanzia haki.

Viongozi tuache tamaa ya kujilimbikizia mali na kuwa na Tamaa ya madaraka.

4. Hayati JPM alijenga Imani kwa wananchi, alisema na kutenda, ukiharibu tu hajili wewe ni rafaki yake lazima akutumbue, hakuna mambo ya kujuana mbele ya kazi ya watanzania.

5. Watanzania hawategemei kuona wala kusikia hujuma ya maendeleo kwa taifa letu.

Tumpe ushirikiano wa kweli sio wa kinafiki Rais wetu Mama Samia Suluhu ili nchi yetu iendelee kuwa na heshima.

Pumzika kwa Amani JPM, mwanga wa milele ukuangazie.
Tusidharau sayansi
 
viongozi mliobaki jufunzeni kusema ukweli hata kama ni mchungu, msiwe wanafiki.
JPM ametufundisha kusema ukweli hata kama hauwafurahishi baadhi ya watu.

Jasiri asiye yumba wala hakubali kuyumbishwa.

kiongozi ambaye hakufikiria tumbo lake bali watanzania wote.

kiongozi ambaye alisimamia sheria bila uoga wala aibu.

Kiongozi aliye fikiria masilahi ya watanzania kwanza kabla ya wengine. alitetea madini yetu na kubadilisha sheria kandamizi ili kulinda na kunufaika na madini yetu.

Kiongozi aliye chukuia kudanganywa na hivyo alitumia kila mbinu kuujua ukweli wa jambo kwa ufasaha na uhakika. mfano makinikia yaliyo kamatwa bandarini n.k

kiongozi ambaye hakubali kupokea majungu na fitina bila kwanza kujiridhisha.alibaini viongozi wengi waliachishwa kazi au kusimamishwa kazi kwa hila na kisha kuwarudisha.

aliwapenda sana watanzania wabunifu na wachapa kazi. aliamini kuwa kufanya kazi kwa bidiii ndio msingi wa maendeleo.

aliye dhamiria kujitegemea zaidi kuliko kuwa tegemezi.

aliye toa elimu buree kwa watanzania wote kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

aliye boresha na kujenga vituo vya afya vingi zaidi karibu kila wilaya.

aliye iunganisha mikoa yote na wilaya zote za tanzania kwa Lami.

aliye fanikiwa kusambaza umeme hadi vijijini.

iliye boresha huduma ya maji safi.
nashangaa mimi nikifata fundisho lake la kusema ukweli kuwa mimi sijahuzunika alivyokufa watu wana mind
 
Poleni watanzania wenzangu kwa kifo cha Mpendwa wetu Hayati JPM, Apumzike kwa Amani.
Hakika kifo chake kimemgusa kila mtu, watu wote wa rika zote.
sijawahi kuona kiongozi analiliwa kama huyu, nyuso za watu wengi zimejawa na huzuni kubwa.
viongozi tuliobaki hai kuna jambo la kujifunza hapa, ni wazi kabisa Hayati Magufuli enzi za uhai wake alifanya kazi yake kwa nguvu zake zote na kwa masilahi ya watanzania,
Amepambana bila kuchoka hadi umauti umempumzisha!!

viongozi tuliobaki tunamambo yafuatayo ya kujifunza;

1. Kila kiongozi ktk nafasi yake ana wajibu wa kufanya kazi kwa uadilifu na kwa bidii kwa masilahi ya watanzania.
tuwajali na tuwatetee wananchi wanyonge.

2. Tupambane kulinda Rasilimali zetu haswa madini.

3. Lazima tupige vita dhidi ya mafisadi na wala rushwa,

Kifo cha Dr. JPM kamwe kisiwe ndio kufunguliwa kwa mafisadi, wala rushwa, wabadhirifu, kujuana, kubebana, wapiga dili, mikataba mibovu, ukwepaji kodi, wauza madawa ya kulevya, wakwepa kodi, majambazi, vibaka n.k

wananchi wa Tanzania tunataka kuona yale yote aliyo yasimamia Hayati Magufuli yanasimamiwa kwa nguvu zote bila kuoneana muhali.

Watanzania wanatarajia kuona heshima na utiifu ulio onekana kwa JPM pia unaonekana akipatiwa Rais wa sas Samia Suluhu.

wananchi wanatarajia kuona watendaji wote wa vyombo vyote wana fanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu kama ilivyo kuwa wakati wa JPM, hatutegemei kuwa ona mawaziri na watendaji wengine waki relax.

Huwezi kuwa kiongozi Mwadilifu kama huna hofu ya Mungu. Magufuli alikuwa ni Kiongozi mwenye hofu kubwa kwa Mungu.
viongozi mlio baki kuweni na hofu kwa Mungu, hofu ya kweli ili Muwatendee watanzia haki.

Viongozi tuache tamaa ya kujilimbikizia mali na kuwa na Tamaa ya madaraka.

4. Hayati JPM alijenga Imani kwa wananchi, alisema na kutenda, ukiharibu tu hajili wewe ni rafaki yake lazima akutumbue, hakuna mambo ya kujuana mbele ya kazi ya watanzania.

5. Watanzania hawategemei kuona wala kusikia hujuma ya maendeleo kwa taifa letu.

Tumpe ushirikiano wa kweli sio wa kinafiki Rais wetu Mama Samia Suluhu ili nchi yetu iendelee kuwa na heshima.

Pumzika kwa Amani JPM, mwanga wa milele ukuangazie.
AMINA!
 
Wasukuma wenzake. Nikiwataja hapa utashangaa
Acha uzushi wataje,so ulihitaji akupendelee wewe kama nani na awaache aliokaribu nao?

Alikufahamu?

Sidhani kama kunampumbavu kama wewe anayeweza kuwagawia mkate watoto wa jirani kwanza kabla ya watoto wake kisa eti anaogopa kusema anapendelea.
 
Povuu halibadilishi ukweli. Magufuli alikuwa mbaguzi full stop.
Alienjoy sana watu kuonewa na kuumizwa. Ndiyo maana wale wa Mwanza alisema wasivunjiwe. Kina Luena wameuwawa hamna waliokamatwa.
Ndiyo maana hata leo wanaoshangilia kufa kwake wanakamatwa sababu ya legacy yake mbaya. Hamuwezi kutulazimisha tulie na nyie. Kila mtu apambane na hali yake. Na hakuna tena msukuma atakuwa rais wa tz maisha.

Swallow your pride
 
Hakika Hayati Magufuli alikuwa Kipenzi cha watanzania wengi.
mwenye macho hambiwi tazama.
mambo yanajionyesha yenyewe.

kwa maombi, sala na machozi ya watanzania hawa wanao mlilia na kumuomba basi hakika Mungu atapokea sala zao.
 
hakuwa mnafiki, alikuwa msema kweli, ukiharibu alikuwa hakopeshi anakuchana hapo hapo live au anakupa makavu live.

alionyesha kwa vitendo kuwa cheo ni dhamana.

ktk kipindi chake kwa mara ya kwanza tulishuhudiwa viongozi wakiwajibishwa kwa uzembe au kushindwa kwao kutimiza wajibu wao.
 
Inatukumbusha God bless lema ni mtabiri na nabii wa kweli! Alimtabilia!
Hii sasa kali hivi swala la binadamu kufa nalo linahitaji utabiri au ndo ukweli wenyewe?kwani kuna atakaebaki?ukiniambia mimi ntakufa hata nikikasirika lakini ni kazi bure kwa sababu ni kweli lazima itafika siku nitakufa nitake nisitake.
Kwa hiyo lema hakutabiri bali alisema ukweli na sasa ni kweli siku yake magu imefika amekufa pamoja na kuhangaika kutafuta sababu.
Sasa kama yeye ni mtabiri mzuri atutabirie kifo chake au tuseme hata kama ni cha mshikaji wake mbowe au vipi?[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Back
Top Bottom