Kifo cha George Floyd: Mashirika ya haki za binadamu yanaiogopa Marekani?

Chief Mtangi

Member
Joined
May 11, 2020
Posts
73
Reaction score
119
Tokea tukio la kikatili na kibaguzi lililopelekea kifo cha George Floyd, mashirika ya haki za binadamu yapo kimya sana tofauti na ilivyo upande wa mataifa ya kiafrika.

Tumezoea kuona mashirika haya yakikemea vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu katika nchi za ki-Africa lakini leo hii yamekuwa kimya sana hata ile nguvu wanayoitumia kupiga kelele mara kwa mara imekuwa tofauti.

Je, yanaiogopa marekani na kuhofia kutopata misaada ama kuna sababu nyingine?
 
Panya walifanya kikao....namna gani tumzuie paka asiendelee kutula Kila siku.

Mjumbe mmoja kwenye kikao akasema ili paka asitusumbue Basi afungwe Kengele ili akiwa anakuja tumsikie.

Wajumbe wote walipenda Hilo wazo ila mzee mmoja akainuka akauliza panya wenzie. NANI WA KUMFUNGA PAKA KENGELE?

Hadi leo panya wanaulizana swali Hilo.
 
Bila shaka Panya mabaka alimaliza mchezo
 
Kumjadili Mmarekani sio kazi ndogo mjue unapata wapi huo ujasiri kwanza.
 
dronedrake,

Yeah, Amnesty international and Human rights watch yote hayapigi kelele kama wafanyavyo kwetu huku, watajifanya kuongea kinafki ili kuua soo ila sio kama wanavyobwatuka kwa nchi za ki-Africa!
 
Alokuwa anawafanya wakemee ndo katenda kwa sasa
 
dronedrake,

Yeah, Amnesty international and Human rights watch yote hayapigi kelele kama wafanyavyo kwetu huku, watajifanya kuongea kinafki ili kuua soo ila sio kama wanavyobwatuka kwa nchi za ki-Africa!
Amnesty international wamekosoa mbona

USA: police must end 'excessive' militarised response to George Floyd protests

Japo kwa upumbavu wanaofanya wale waandamanaji, Ni sahihi kuwakabili na jeshi

Yale sio maandamano Ni ugaidi, kuchoma majengo Moto? Kupora? Kuharibu Mali?
 
Walaani nini wakati ili ni ukatili uliofanywa na matakwa binafsi na sio sera za nchi.Wallaani nn wakati hatua zimeshachukuliwa? Wanalaani Africa sababu polisi anayo haki ya kuuwa ili kumfurahisha mtawala na akaendelea na kazi bila kuchukuliwa hatua.So wangelaani USA Kama hatua zisingechukuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…