Kifo cha ghafla cha Mfugale sawa na Prof. Chachage: Kuna viashiria vyote vya kupewa sumu. Serikali ichunguze

unasema?
 
Mimi sitaki kutilia shaka sababu nimeshuhudia watu kufariki ghafla tu tena sana mtu mzima mara anajisikia vibaya anapoteza maisha. Shida yangu moja tu kwa yule sijui katibu mkuu aliyekuwa anasimulia tukio. Kwa mujibu wa maelezo yake kajisikia vibaya akamwambia nenda ofisini kapumzike kikao kiendelee baadae akasema ngoja nikamwangali kaenda kamkuta kwenye kitu ila wazi hali yake sio nzuri akauliza wasaidizi kimetokea nini wakasema aliomba tu AC iongezwe iwe baridi basi akakaa mpaka alivyokuja na kumkuta.

Tuseme yote ni kweli ila hivi mtu kasema najisikia vibaya utamwambia nenda ofisini na wasaidizi walichofanya kuongeza AC sio mara moja kuandaa usafiri kumpeleka Hosp au kuita huduma ya kwanza bila kusubiri mpaka katibu mkuu aje ndio aratibu magari hivi kweli goverment city hakuna hata first aid clinic?

Kwa hapo kuna uzembe mkubwa sana katika ku deal na emergency case sisemi watu hawafariki lakini kuwe na hatua za haraka za kujitosheleza unaweza kuokoa maisha ya mtu yoyote. Kwenye hili haliko sawa na sio kwa marehemu tu kwa wafanyakazi wote linaweza kutokea.
 
Vipi na Dr. Magufuli naye, ni njia ile ile?
 
Basi wewe utakuwa Chahali yule wa Ughaibuni. Ndio anaandikaga mambo ya ovyo kama haya.
 
Uviko unaandika bila kujua ukweli hutu mzee alikuwa na mgonjwa kwa muda mrefu tuu na ndio maana hata mwendazake alimruhusu afanyie kazi DSM ili kuwa jirani na matibabu.

Hv unafikiri mtu mwenye umri zaidi ya 70 years afya yake ikoje!
 
Hivi Dr.Mwakyembe alibahatika kufikwa na umauti.
 
Huyu Marehemu alivyokuwa Hai alishawahi Kukuambia kuwa ameingia Makubaliano Maalum na Mwenyezi Mungu kupitia Wakala wake Mkuu wa Vifo na Kuua aitwae Israeli kwamba Yeye hatokufa na ataishi Milele hapa duniani?

Watanzania baadhi yetu tunaanza sasa Kupanda Mbegu mbaya ya kuanza Kuhoji kila Mtu maarufu au Kiongozi tu akifa huku tukihusisha kuwa ni Mauwaji ya Kimafia na hatutaki Kukubali kuwa hata uwe nani chini ya Mbingu hii ukifika muda wako wa Kufa utakufa tu

Na bahati mbaya kuna baadhi ya Watu ( siyo Marehemu Mfugale ) ambao mnahoji Vifo vyao huku mkivihusisha na Njama za Kimafia kwa miaka mingi tu wanajulikana kuwa walishaathirika na Ugonjwa wa Kuishi kwa Matumaini, Saratani na Shinikizo la Damu.
 
Uviko unaandika bila kujua ukweli hutu mzee alikuwa na mgonjwa kwa muda mrefu tuu na ndio maana hata mwendazake alimruhusu afanyie kazi DSM ili kuwa jirani na matibabu.

Hv unafikiri mtu mwenye umri zaidi ya 70 years afya yake ikoje!
Mgonjwa alikuwa anapiga kazi kweri kweri
 
Naweza kukubaliana na wewe ili ulichokosea mkuu ni kutaka kutuonyesha kazi yako, ulitakiwa wewe utiririke tu ukimaliza Kaa kimya acha watu wacoment wawezavyo Ila Sasa mmh unatia Shaka hata Kama ni kutaka sifa tukujue wewe ni Nani sio poa🙄🙄🙄
 
Mwaka jana kuna watu wengi sana walikufa kwa covid-19 eneo ninaloishi. Kuna wakati mwanafunzi wangu aligua covid-19 nikaandika hapa kuwa huenda na mimi ni mhanga, watu wengi wakanitoa hofu na kunishauri nitumie nyungu! Mungu ni mkuu alininususru, na namshukuru sana kwa hilo.

Covid-19 huwa haiui mtu kwa siku moja au mbili tu; inachukua muda wa kuanzia siku nane na kuendelea, kwani huanza na homa kabla ya mapafu kuanza kubana. Ile homa inaweza kuchukua siku nne au tano hivi kabla mapafu hayajaanza kubana; baada ya mapafua kuanza kubana inachukua si chini ya siku nne za mtu kuishi akiwa anahema sana kabla hajashindwa kabisa kupumua. Kwa mtu anayeugua ghafla siku moja na kufa siku hiyo hiyo au baada ya siku mbili tatu tu ujue siyo Covid-19, kuna kingine zaidi.

Data zilizotolewa na madaktari waliofanya utafiti wa kupima ni muda gani mwili unaweza kuhimiri covid-19 umeonyesha kuwa siku za chini ni nane hadi siku 37; paper yao iko hapa

 

Attachments

Mimi nimehisia tu (suspect). Serikali ndiyo inatakiwa na inauwezo wa kuchunguza na kuthibitisha
Kwamba postmortem, yaani uchunguzi wa ripoti ya kitabibu juu ya chanzo cha kifo ambapo hufanywa na madaktari hautoshi? Kwani haukufanywa?? Kama umefanywa je unasemaje?
 
Acha uzushi kama kidume weka namba zako za sinu hapo mwisho,yaani serikali ikuue then ikuchunguze yenyewe acha kujichanganya
 
Umeeleza VIZURI ila naongeza uyu bwana sio maskini familia wanashindwa vipi kufanya uchunguzi binafsi wa ndugu yao hata KWA kupeleka mwili kenya ,ili mwisho wa siku waje na majibu mazuri , kwamba kama alitendewa Jambo baya wanafikili watapata majibu sahii,

Wafiwa poleni lakini pia yawabidi jiongeza , ili mpate chanzo au tatizo lililosababisha kifo chake , aliopokua wanasema hawajui tatizo Sasa mnashindwa vipi jiongeza kufanya uchunguzi binafsi wa marehem KWA kutumia watu Wengine nje ya tz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…