Acha kabisa. Halafu kuna vichaa 2020, baada ya wizi wa kura, walikua wanapiga kelele "Mzalendo, Jiwe, Aongezewe Muda, Kiongozi wa Malaika, Aongozewe Muda". Basi kila akisifiwa ndio akawa anazidisha aisee. Sheenz Kabisa!
Wakawa wanajitoa ufahamu jinsi raia walivokua wanaingiliwa mpaka uhuru wao wa kufanya starehe na maisha yao. Mara baa na kumbi za starehe (Hata kama kumbi za harusi) mwisho saa 6, mara mitandao ya kijamii ifungwe, mara internet ishushwe 2G, mara bando zipandishwe mara mbili bei n.k
Yaani raia tulikua tunapelekwa kama watoto wa chekechea! Amani ya moyo ilitoweka, mtu hujui kesho yako utaishia kolokoloni mahabusu au utakula ya uhujumu uchumi!