Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS


Hapa naona Mheshimiwa jaji amehukumu kizalendo zaidi ya kisheria. Swali ni je Scandinavia wandaiwa na Shell na je wanaweza kuwalipa baada ya kuwalipa wadeni wengine.

Bankruptcy nielewavyo mimi si mwisho wa biashara. Kinachofanyika ni kumweka mdaiwa katika hali atakayoweza kulipa madeni yake. Marekani wanaita chapter 11. Hii inajumuisha kuchukua maamuzi machungu kama kuuza non-perfoming assets, kupunguza mishahara na kwa kampuni kama hii hata pengine kujitoa kwenye route ambazo hazilipi. Makampuni makubwa mengi ya marekani (Delta Airways n.k)yalijitangaza kuwa bankrupt na baadhi yameweza kurudi katika hali yake ya awali na hata kuipita.

Sasa hiyo miezi tisa ikipita bila makubaliano na hali ya kampuni kuwa mbaya zaidi atafanya nini? Kwa vile mimi si mwanasheria au economist wale wenye uelewa zaidi wa namna suala la kufilisika linavyoshughuliwa Tanzania wanaweza kunisahihisha nilipokosea.

 

Maelezo haya yangefaa kusindikizwa na mfano wa mabasi ya Kiswele..
 
Naomba unisaidie kwenye hilo! Ya Kiswele yalikuwaje?

Kibunango tusaidie tafadhali maelezo kidogo ya mabasi ya Kiswele, bila kusahau Tawaqal na akina Safina!
Naona stori inazidi kunoga!
 
Fundi Mchundo ametoa maelezo mazuri juu ya uendeshaji wa makampuni mengi ya Tz na hasa yale ambayo yamepata mtaji kupitia mikopo ya benki. Kiswele kama alivyokuja kuyaita mabasi yake Kiswele nae alikuwa amekopeshwa na benki na akamua kuanzisha kampuni ya usafiri.

Tatizo lilikuja kwenye utawala wa kampuni hiyo. Kama alivyofafanua Fundi Mchundo. Kiswele baada ya muda alijikuta hawezi tena kuiendesha kampuni hiyo kutokana na kuwa na madeni mengi na kushindwa kuyafanyia matengenezo mabasi yake. Tatizo kubwa lilikuwa ni kushindwa kuwa na mfumo unahohitajika katika kuendesha biashara ya namna ile. Zaidi atazidi kukumbukwa kwa kuajili nduguze ambao walichangia kwa asilimia kubwa kufa kwa kampuni yake.
 
Source: The Guardian, Thursday, June 4, 2009, Page iii


Same to ES HAQ LIMITED

Habari ndo hiyo!
 
This company ilipandisha Tz chart sana haswa nchi za jirani!

Kwa nini ikaanguka??
 
This company ilipandisha Tz chart sana haswa nchi za jirani!

Kwa nini ikaanguka??

Mkuu, inaelekea walikuwa wana madeni makubwa sana. Miaka mingi sasa wameshindwa kurudisha madeni kama mikataba ya mikopo yao ilivyokuwa inataka.

Ukipita pale Pugu Road/Kurasini Garages, kuna baadhi ya mabasi yao pia yamekufa siku nyingi.

Ama kweli vyote ving'aavyo si dhahabu.
 
Du! Ni kati ya mabasi niliyokuwa napenda kusafiri nayo pia kwa huduma ya kutuma mizigo na pesa. Early 2000's walikuwa vizuri kwenye biashara.
Eniwei bado kuna Royal, Dar Expr. et al.
 
Halafu walikuwa on time hata kama wana abiria mmoja! nadhani hili pia lilichangia kuanguka kwa kampuni maana walikuwa wanapata hasara!

Makampuni mengine waliwaangalia tu...sasa makampuni kama Abood, Hood, dar express yapo siku zote mbona hayafilisiki? Au hayakuchukui mikopo?
 
Hawa waliondoka na iliyokuwa serikali ya 'AWAMU YA TATU' sijui nani alikuwa anawabeba maana baada tu ya utawala huu wa sasa kuingia ofisini, mabenki yakawashikia bango na magari yao mengi yalikamatwa.

Wali-negotiate muda wa kulipa wakaachiwa walipe lakini inaonyesha biashara imekuwa haiwaendei vizuri siku za karibuni.
 
Du! Ni kati ya mabasi niliyokuwa napenda kusafiri nayo pia kwa huduma ya kutuma mizigo na pesa. Early 2000's walikuwa vizuri kwenye biashara.
Eniwei bado kuna Royal, Dar Expr. et al.

Belinda ni kweli hawa jamaa walianzia mbali sana. nakumbuka miaka ya 1984/85 tulikuwa tunapanda sanamagari yao weekend tukitokea Kibaha kuwahi Disco la Space 1900 pale Mbowe Hotels.

Mwaka 2004 nilikutana na huyo owner, kulikuwa na mpango wa Scandinavia na mabasi ya Arriva yanayotoa huduma European Countries kufanya project ya pamoja kutoa huduma DSM. Yeye pia lidai alikuwa ametoa proposal serikalini ili afikiriwe kupata support lakini akapigwa Mizengwe.

Miaka hiyo anakwambia alikuwa analeta Marco Polo toka Brazili kila baada ya Miezi miwili, gari moja au mbili . . . .

Sijui sasa itakuwaje. Walijitahidi sana katika Africa mashariki. Ila inamwelekeo kuwa ilikuwa ya Kishow down sana kuliko Kibiashara.
 

Mkuu,

makampuni mengi ya Mabasi hayana maisha marefu. Nikiwa Moshi nakumbuka kulikuwa na Makampuni yalivuma kama Lang'ata, Ngorika, Yellow, TAMT nk. Lakini yote sasa hivi Kwishnei.
 


Habari ndo hiyo Mkuu!
 
Scandinavian, Zainabu na Kwacha hawa walikuwa na mfumo wa aina moja ya uendeshaji wa biashara hii ya mabasi ya abiria?

Je tatizo la sasa la Scandinavian linafafana na lile la Kiswere?
 
Hivi nani mmiliki/wamiliki wa Scandinavian Express? Kuna kipindi nilikua nasikia tetesi kuwa John Momose Cheyo(Mapesa) alikua mmoja wa wamiliki ila sina uhakika.
 
Last edited:

Kulikuwa na fununu ya kuwa Sumaye alikuwa na mkono wake pale.
 
Scandinavian, Zainabu na Kwacha hawa walikuwa na mfumo wa aina moja ya uendeshaji wa biashara hii ya mabasi ya abiria?

Je tatizo la sasa la Scandinavian linafafana na lile la Kiswere?


Ni kweli Mkuu, in fact walianza zamani na walikuwa washindani Kibiashara. Zainabu na Kwacha nadhani zilikufa.

Kiswere ni wapi hao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…