Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Jaji Kimaro alisema baada ya kupitia hoja za upande wa mashitaka na upande wa utetezi, amebaini kuwa kuifilisi Kampuni ya Scandinavian si jambo la busara.
Alisema anakubaliana na hoja za mawakili wa upande wa utetezi kuwa kampuni hiyo ina mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa.
Alisema inasafirisha abiria zaidi ya 2,000 kila siku kwa kutumia mabasi zaidi ya 80.
Mabasi hayo yanafanya shughuli zake katika eneo lote la Afrika Mashariki hadi katika nchi za Malawi na Zambia.
Kampuni imeajiri wafanyakazi zaidi ya 600; ambao Jaji Kimaro alisema kwa hali ya sasa ya ukosefu wa ajira na ongezeko la uhalifu nchini, kuifilisi ni kuleta matatizo zaidi.
Alisema kampuni inatumia sh 69,343,500 kila mwezi kuwalipa wafanyakazi mishahara.
Hapa naona Mheshimiwa jaji amehukumu kizalendo zaidi ya kisheria. Swali ni je Scandinavia wandaiwa na Shell na je wanaweza kuwalipa baada ya kuwalipa wadeni wengine.
Bankruptcy nielewavyo mimi si mwisho wa biashara. Kinachofanyika ni kumweka mdaiwa katika hali atakayoweza kulipa madeni yake. Marekani wanaita chapter 11. Hii inajumuisha kuchukua maamuzi machungu kama kuuza non-perfoming assets, kupunguza mishahara na kwa kampuni kama hii hata pengine kujitoa kwenye route ambazo hazilipi. Makampuni makubwa mengi ya marekani (Delta Airways n.k)yalijitangaza kuwa bankrupt na baadhi yameweza kurudi katika hali yake ya awali na hata kuipita.
Sasa hiyo miezi tisa ikipita bila makubaliano na hali ya kampuni kuwa mbaya zaidi atafanya nini? Kwa vile mimi si mwanasheria au economist wale wenye uelewa zaidi wa namna suala la kufilisika linavyoshughuliwa Tanzania wanaweza kunisahihisha nilipokosea.
The primary purpose of bankruptcy is: (1) to give an honest debtor a "fresh start" in life by relieving the debtor of most debts, and (2) to repay creditors in an orderly manner to the extent that the debtor has the means available for payment. Bankruptcy allows debtors to be discharged from the legal obligation to pay most debts by submitting their non-exempt assets, if any, to the jurisdiction of the bankruptcy court for eventual distribution among their creditors.