Mkuu,
makampuni mengi ya Mabasi hayana maisha marefu. Nikiwa Moshi nakumbuka kulikuwa na Makampuni yalivuma kama Lang'ata, Ngorika, Yellow, TAMT nk. Lakini yote sasa hivi Kwishnei.
Hivi nani mmiliki/wamiliki wa Scandinavian Express? Kuna kipindi nilikua nasikia tetesi kuwa John Momose Cheyp(Mapesa) alikua mmoja wa wamiliki ila sina uhakika.
Owner ni Huyu Mkuu:
Mr. Mohamed Abdullah
Scandinavian Express Services Ltd.
P.O.Box 2414, Tel: 2850847/9
Fax: 2850224, Mob: 0754-336611
E-mail: Scandinavia@raha.com
Dar es Salaam
Kiswere alipata mkopo mkubwa sana wa Mabasi toka katika benki zetu hapo nchini. Mengi ya mabasi yake yalikuwa na safari za mikoa ya kusini, na mikoa ya kusini nyanda za juu.Kiswere ni wapi hao?
Hawa waliondoka na iliyokuwa serikali ya 'AWAMU YA TATU' sijui nani alikuwa anawabeba maana baada tu ya utawala huu wa sasa kuingia ofisini, mabenki yakawashikia bango na magari yao mengi yalikamatwa.
Wali-negotiate muda wa kulipa wakaachiwa walipe lakini inaonyesha biashara imekuwa haiwaendei vizuri siku za karibuni.
Hilo Ndo tatizo la biashara kuanzishwa kwa nguvu au ulinzi wa siasa nyuma ya mwanasiasa. Nguvu ya Scandi ilikuwa Sumaye kupitia Omary Mahita. Tulipata shida sana awamu ya 3, ilikuwa ukikamata gari la scandi, ukilifikisha kituoni tu wakati uko njiani unarudi juani, gari hilo hilo linakupita likiendelea na safari. "MEMO WORK"
Wiki ya kwanza tu ya utawala wa awamu ya nne, gari na magdreva wa scandi walisumbuliwa saana. mengi yalianza kupaki na kushinda vituo vya polisi. IGP naye akachoka kuendelea kuwalinda. Na pengine tulifanya maksudi kuwakamata ili kumkera IGP na wakubwa wenziwe.
Hali ya scandi itawakuta pia ABOOD mara tu siasa zikienda kombo kwa Mh. Abood. Yaani sasa ABOOD BUS SERVICE na Madreva wake ni sawa Convoy ya Msafara wa RAis. Hawagusiki..