Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

Mkuu,

makampuni mengi ya Mabasi hayana maisha marefu. Nikiwa Moshi nakumbuka kulikuwa na Makampuni yalivuma kama Lang'ata, Ngorika, Yellow, TAMT nk. Lakini yote sasa hivi Kwishnei.

Wafanyabiashara karibu wote wa mabasi huendeka sana ushirikina. Na ushirikina huo huambatana na masharti ya hali ya juu ya kishetani. Kwahiyo huwa si rahisi kuya-maintain na kisha hufilisika kwani ibilisi anachukua chake.
 
Hivi nani mmiliki/wamiliki wa Scandinavian Express? Kuna kipindi nilikua nasikia tetesi kuwa John Momose Cheyp(Mapesa) alikua mmoja wa wamiliki ila sina uhakika.


Owner ni Huyu Mkuu:

Mr. Mohamed Abdullah
Scandinavian Express Services Ltd.
P.O.Box 2414, Tel: 2850847/9
Fax: 2850224, Mob: 0754-336611
E-mail: Scandinavia@raha.com
Dar es Salaam
 
Kuna kupanda na kushuka eeh! Maisha ni mlimaa japo kuteleza sio kuanguka eeh mtoto wa mamaa!
 
Owner ni Huyu Mkuu:

Mr. Mohamed Abdullah
Scandinavian Express Services Ltd.
P.O.Box 2414, Tel: 2850847/9
Fax: 2850224, Mob: 0754-336611
E-mail: Scandinavia@raha.com
Dar es Salaam

Asante kwa kunifahamisha mkuu.

Mimi nadhani kuna tatizo kubwa la uendeshaji na vision maana sielewi kampuni iliyokuwa ikivuma kama hii imekufajekufaje. Kama tatizo ni la kukopa basi itakuwa walikopa kiasi kikubwa mno kuliko wanavyoweza kumudu au hizo pesa za mkopo hazi kuwekezwa vizuri. Na pia nadhani hawa wali taka sana kuwa "ndege" za barabarani kiasi cha kutumia pesa nyingi katika kufanya mabasi yao luxury bila kuzingatia wateja wao ni wakina nani na wana uwezo kiasi gani.
 
Kiswere ni wapi hao?
Kiswere alipata mkopo mkubwa sana wa Mabasi toka katika benki zetu hapo nchini. Mengi ya mabasi yake yalikuwa na safari za mikoa ya kusini, na mikoa ya kusini nyanda za juu.

Hata hivyo kampuni hii haikudumu na ilianguka na sasa haipo kabisa. Sijui tatizo ni nini kwa hawa wanaochukua mikopo katika Benki.

Awali kabla ya mkopo huu Kiswere alikuwa akifanya biashara ya usafirishaji wa mizigo kwa gari lake la mizigo la tani sabaa.
 
Hawa waliondoka na iliyokuwa serikali ya 'AWAMU YA TATU' sijui nani alikuwa anawabeba maana baada tu ya utawala huu wa sasa kuingia ofisini, mabenki yakawashikia bango na magari yao mengi yalikamatwa.

Wali-negotiate muda wa kulipa wakaachiwa walipe lakini inaonyesha biashara imekuwa haiwaendei vizuri siku za karibuni.

Hilo Ndo tatizo la biashara kuanzishwa kwa nguvu au ulinzi wa siasa nyuma ya mwanasiasa. Nguvu ya Scandi ilikuwa Sumaye kupitia Omary Mahita. Tulipata shida sana awamu ya 3, ilikuwa ukikamata gari la scandi, ukilifikisha kituoni tu wakati uko njiani unarudi juani, gari hilo hilo linakupita likiendelea na safari. "MEMO WORK"

Wiki ya kwanza tu ya utawala wa awamu ya nne, gari na magdreva wa scandi walisumbuliwa saana. mengi yalianza kupaki na kushinda vituo vya polisi. IGP naye akachoka kuendelea kuwalinda. Na pengine tulifanya maksudi kuwakamata ili kumkera IGP na wakubwa wenziwe.

Hali ya scandi itawakuta pia ABOOD mara tu siasa zikienda kombo kwa Mh. Abood. Yaani sasa ABOOD BUS SERVICE na Madreva wake ni sawa Convoy ya Msafara wa RAis. Hawagusiki..
 
Wafanya biashara wa mabasi TZ wakachukue desa Kenya kwa Akamba. Hawa jamaa hawayumbi!
 
Biasahara ya mabasi yaendayo masafa marefu yahitaji mitaji mikubwa na pia serikali yatakiwa kutoa ruzuku ili kuwapa hawa investors incentives,government ya TZ ya ajabu kabisa,public trsnsport hovyo kila kitu shagara bagala.Kitu muhimu ktk society ni usafiri watu waende na kurudi ktk shughuli zao za kila siku na hili ni kiungo kikubwa kwa maisha ya kila siku.Uozo uliopo sasa 1.ajali nyingi kupindukia,watu tena watanzania masikini hawa wanapoteza maisha na malizo wengine vilema 2.Msongamano dsm,watu wanafanya kazi masaa macahache badala na kupoteza resources nyingi i.e Tegeta-Posta inachukua masaa matatu na zaidi badala ya nusu saa(UJINGA GANI HUU) na serikali ipo tu"why" no initiatives
CHAKUFANYA
1.Serikali yatakiwa kutoa ruzuku ktk public transport
2.Ipitie upya miundo mbinu iliyopo dsm i.e transport system irekebishwe upya
3.Mass rapid transit ianzishwe ikisaidiana na BRT itakayoanza hapo baadae
5.Good governance i.e management makini ktk uwajibikaji
6.Serikali itambue kumkomboa masikini ni kumpa miundo mbinu imara na bora
NASHANGAA SERIKALI IMESINZIA "YAANI HAKUNA RUZUKU KTK PUBLIC TRANSPORT"Kilio cha masikini ajari kibao.... HOVYOOOOOOOOO=Gornment not responsible for her citizen!!!!!!!!! tutafika kweliiiiii
 
Bei ya mabasi ya mikoani si inapangwa na serikali au? Ukijumlisha hiyo na cost ilivyoongezeka ya mafuta = Kifo.
 
Yap bei inapangwa na serikali,ili watu wanufaike na hizo bei huwa inatakiwa price =marginal cost,twasema hiyo ndo optimal price or welfare price,mtu binafsi hawezi fanya biashara ktk hiyo price ndo maana serikali hutakiwa kutoa ruzuku kuwasaidia walipa kodi.SUMATRA wapo pale kula mishahara bure hukuna lolote wafanyalo.
 
kila jambo Duniani lina kanuni yake.
Ukienda kinyume cha kanuni huna haja ya kwenda kupiga Bao kwa Bibi Kalembwana, kifo ni halali yako.
Biashara ina kanuni zake.
Pamoja na kanuni nyingine kadhaa,Ili Biashara isife ni lazima kwanza iwe na faida pili Matumizi binafsi yasizidi asilimia 10% ya faida. Sivyo biashara inakufa.
Kuna Mtu alianza kuuza karanga kwenye kapu nikiwa darasa la kwanza miaka 35 ilopita leo hii bado anaendelea na biashara nyingine kubwa za Maduka na Usafirishaji kwa kutumia kanuni ile ile ya kutengeneza faida kwa kuuza karanga.( Ubahili)
Watu wasio jua kanuni za biashara, husaidiwa na kitu inaitwa ubahili.
Ukifanya biashara na kutanguliza ubahili biashara itakua wanapenda hawapendi.

Ukipangiwa bei kwenye biashara ikatokea kwamba bei ulopangiwa haiendani na gharama za kuendesha biashara, ni wazi kwamba biashara yako itakufa kifo cha asili.

Kufuata kanuni katika kila jambo ulifanyalo ndiko kuletako mafanikio hakuna zaidi.
Unaweza kuleta Visingizio Magunia milioni moja yote yakapanguliwa na kanuni ukabaki mtupu.
kanuni ni kanuni haina mjadala.

Ndiyo maana Watu waovu huweza kutajirika na kuzidi kutajirika na wasifirisike katika biashara maisha yao yote kwa sababu wanafuata kanuni za fedha. Watu wema huweza filisika mpaka ukawaonea huruma kwa sababu hawafuati kanuni za fedha. Wema si sehemu ya kanuni za fedha hapa Duniani labda katika ulimwengu wa Roho.
Ili fedha ikue ni lazima iwe na mfumo wa ndani kwa ndani wa kujiongeza kadri muda uendavyo.
Wako waibao kuongezea mtaji,
wako waongezao mtaji kutoka katika faida,
wako waongezao mtaji wa biashara kwa kubadiri aina nyingine ya utajiri wao na kuwekeza kwenye biashara isiyo leta faida.

Gharama ya kununua ikiwa ni Tshs100,000. ukauza bidha hiyo kwa Tshs 100,000. utaishia kukamata fedha mkononi lakini faida yake ni -###.
Gharama ya kununu ikiwa ni Tshs 100.00 ukauza kwa Tshs 200.00 faida yake ni 100 umeshika fedha kidogo lakini faida yake ni 100%. Ukiuza unit 100000 kwa wiki hiyo inaitwa biashara bila kujali unauza pipi au vitumbua.

Maji yanafuata mteremko.
jiwe likirushwa juu lazima lishuke tena chini.
Mwanga ukiingia giza linatoweka.
Ukipanda Mahindi unavuna mahindi au mabua.
Mbegu ya harage huzaa harage au haizai.
Chenye mwanzo kina mwisho.

Kwa kutumia derived theories kanuni zote hapo juu zaweza kuvunjwa bila shida.
Ili kuvunja Natural principles derived theories zote ni lazima zi hold at semuliteneously when one fails unapata Disaster kama ile ya Spaceship ya NASA Challenger.

Watu hawafilisiki kwa sababu ya uzembe tu, upofu wa kanuni nao ni hoja ya kutweza.
 
Last edited:
Ipo dhana kwamba kampuni ya Scandinavia ilijitanua sana kwa muda mfupi na kusababisha kifo chake. baadhi ya wachumi wanasema ingelifaa wakati wanaanza huduma za nje ya nchi, wangetenganisha kuwa na makampuni mawili tofauti. Kwa kufanya hivyo, ingewawia rahisi kuwa na strategies tofauti kwa mazingira tofauti ya biashara.
 
mwe kakampuni kangu je si kataded nako pia maana ni moja ya kumi ya scandi woowi,

ila nilimsikia mkurugenzi wa crdb kwenye semina moja akilalamika sana kwamba hawa jamaa wamewatenda mbaya kwani waliposhinda kesi na kuamua kuseize kwa kushindwa kulipa deni walitetewa na sheria ya wakati huo lakini sheria imebadilika sasa lakini hakuna kitu tena cha kukamata kwani wako hoi hivyo walipaji mkopo huu ni sisi wadau kwa kodi zetu
 
biashara ya mabasi kwa tanzania ni ngumu sana, kwa sababu asilimia kubwa ya wamiliki wa vyombo hivyo wanakuwa hawana mitaji yenye base nzuri, scandinavia ni kampuni ya zamani na ilikuwa imesurvive kwa muda mrefu sana kwa kuwa ilikuwa na mtaji halali wenye base, kosa kubwa alilolifanya mmiliki ni kukubali kuwa joint na mafisadi na kuanza kutumbukiza mapesa yasiokuwa na base, wajanja walikuwa wanakopa bank kwa ajili ya company lakini ni 20 to 50% tu ndio iliyokuwa inaingia kwenye company the rest jamaa walikuwa wanakula na hiyo ndio ikawa chanzo cha kumwaribia owner biashara yake ambayo aliiendesha kwa miiko sana
 
Nadhani Kituko ndo amesema kweli, it does not make sense huyu owner alieanzia chini kwa mtaji wake aje ashindwe kwavile kachukua mkopo. Kama issue ni kuruhusu share na wengine nadhani ndo ameharibikiwa hapo - Jamani tusikate tamaa kuwa haiwezekani isipokuwa tafuta sababu unaweza kukuta biashara fulani unayoona imekufa pengine mwenyewe kaicha na kaona nyingine nzuri na kahamishia mtaji huko inapeta.
Kikubwa ni kuangalia wanaokuijia wakuongeze mtaji wanafanya biashara gani/ imefikia wapi?
Kuna shemeji yangu alistaafu miaka 4 anaishi vizuri tu kwa biashara ya baa na guest na nyumba 5 amepangisha hakuwa na tatizo ni nyumba hasa zenye hatimiliki mjini hapa. Alitokea rafiki akamshauri aweke rehani nyumba zote kisha wapewe mtaji yeye rafiki anunue korosho kupeleka India kwa mwezi inaingiza 10m. ndio ulikuwa mwanzo wa kufilisika na mwisho kufariki kabisa kwa huyo mtu within 2 months only baada ya benki kunyang'anya vyooote.
Biashara fanya mwenyewe tamaa ya mtaji toka chama, rafiki, sijui raisi itabidi udance to their tune, which is not possible
 
Hilo Ndo tatizo la biashara kuanzishwa kwa nguvu au ulinzi wa siasa nyuma ya mwanasiasa. Nguvu ya Scandi ilikuwa Sumaye kupitia Omary Mahita. Tulipata shida sana awamu ya 3, ilikuwa ukikamata gari la scandi, ukilifikisha kituoni tu wakati uko njiani unarudi juani, gari hilo hilo linakupita likiendelea na safari. "MEMO WORK"

Wiki ya kwanza tu ya utawala wa awamu ya nne, gari na magdreva wa scandi walisumbuliwa saana. mengi yalianza kupaki na kushinda vituo vya polisi. IGP naye akachoka kuendelea kuwalinda. Na pengine tulifanya maksudi kuwakamata ili kumkera IGP na wakubwa wenziwe.

Hali ya scandi itawakuta pia ABOOD mara tu siasa zikienda kombo kwa Mh. Abood. Yaani sasa ABOOD BUS SERVICE na Madreva wake ni sawa Convoy ya Msafara wa RAis. Hawagusiki..

aisee hivi Abood huyu mheshimiwa waziri/naibu waziri na yule wa Morogoro ni ndugu?
 
Kuna tetesi kuwa baadhi ya wanasiasa ndiyo waliochangia kuiua kampuni yetu maskini.
 
Hii kampuni ilifanya kazi kisiasa zaidi, inadaiwa kuna watu wa nyadha za juu serikalini ambao walikuwa wanashare na kampuni hii, ndio maana mabenki-nbc na standard chartered bank walivyokuwa wanamface moha/md wa scand. Alikuwa anajibu mbofu mbofu na kujiamnini sana
 
Ohhhh mambo mazito hayo!!!!! Jamaa walibebwa sana kwa kuwa shareholders walikuwa ni hao tunaowatuhumu kwa dhuluma!!! Wengi wao baada ya kuachia madaraka walichomoa kilicho chao!!!! On the other hand, Biashara ambazo zinaendeshwa kwa ushirikina huwa hazidumu!!!! R.I.P wale wafanyakazi ambao kila mwaka walikuwa ni lazima afe binadamu kwa mazingira ya kutatanisha, poleni sana ndugu wa marehemu!!!! Madereva taxi wa muda mrefu pale wana details nzuri sana kuhusu mambo ya giza ya hii kampuni!!! Na kwa bahati njema yule mganga wao mkuu alikufa kati ya 2006 mwishoni au mwanzoni mwa 2007. Jamani tegemea jasho lako, na si nguvu za mwanadamu!!! Imeandikwa hivi, ole wake amtegemeaye mwanadamu. Hapa haimaanishi kuwa tusitegemeane bali utegemezi wetu uwe wa mambo ya kawaida ila tujifunze kusimama kwa miguu yetu wenyewe kwa asilimia kubwa na asilimia kidogo ndiyo uwe tegemezi. Kinyume na hapo ni matatizo. Hata haya traditional (extended) family wetu ni lazima tuwape namna ya kusimama wenyewe na si kumpa mtu eti leo cent, kesho shilingi, etc mpatie kitu ambacho kitazalisha asimamie aone ni chake au mpe elimu period, sana sana baada ya kumpa mtaji au elimu msaidie mawazo ya kusonga mbele. Period.
 
Tunarejea ratiba za kusafiri na ungo very soooon.
 
Back
Top Bottom