Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa walitesa sana na kutawala anga ya usafiri katika nchi hii na za jirani...labda ni usemi wa kweli kwamaba hakuna marefu yasiyo na ncha!..Hata hivyo heshima yenu hiwezi kusahaulika kwa hapa TRanzania, tangia kusafirisha watu, mizigo na pesa!...Good job!
Itakuwa habari njema kama jamaa wataendelea kuwapo. Ni kampuni pekee ya usafirishaji hapa nchini inayoelewa maana ya customer service. Mengine yote hayana tofauti na dala dala za Dar. Rekodi yao ya usalama pia ni nzuri. Hawana matukio ya ajali za kizembe. Tuwaombee washinde majaribu ya kibiashara.Wanaleta mabus YonTong za kichina according to dataz yapo 50.
Mpaka sasa anauza mabus yale ya zamani yooote naona akina supernajimunisa wanayagombania wanayabadili rangi pamoja na hao wengine hawa wanao penda kununua mabus mabovu wanayanunua ya Scand kama akina Upendo. Mpaka sasa madereva wake wanakula mishahara wanasubili hayo 50 yatoke.
Biashara ilitetereka kimtaji, lakini sasa wameagiza mabasi 50 kutoka China na muda si mrefu watakuwa barabarani.