Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

Kifo cha kampuni ya mabasi SCANDINAVIA EXPRESS

wamefilisika, ila kwa kipindi cha uhai wao , walileta mapinduzi katika sekta ya usafirishaji mabasi.
 
Watoto wa MOHA ndio wameichukua wanataka pia kujihusisha na mabasi yaendayo kasi ya jiji la dar. ambayo tumeambiwa yanakuja soon. Japo sijui how soon is soon.
 
Hawa walitesa sana na kutawala anga ya usafiri katika nchi hii na za jirani...labda ni usemi wa kweli kwamaba hakuna marefu yasiyo na ncha!..Hata hivyo heshima yenu hiwezi kusahaulika kwa hapa TRanzania, tangia kusafirisha watu, mizigo na pesa!...Good job!
 
Hawa walitesa sana na kutawala anga ya usafiri katika nchi hii na za jirani...labda ni usemi wa kweli kwamaba hakuna marefu yasiyo na ncha!..Hata hivyo heshima yenu hiwezi kusahaulika kwa hapa TRanzania, tangia kusafirisha watu, mizigo na pesa!...Good job!

Ni kweli PJ, mimi bado nawaheshimu wale jamaa, walituonesha namna Mtanzania anavyopaswa kupewa huduma ya usafir, mara kadhaa nimewahi kwenda nayo Songea, Mbeya na Iringa katika harakati za kufuta umasikini....Nawaheshimu sana.
 
Wanaleta mabus YonTong za kichina according to dataz yapo 50.
Mpaka sasa anauza mabus yale ya zamani yooote naona akina supernajimunisa wanayagombania wanayabadili rangi pamoja na hao wengine hawa wanao penda kununua mabus mabovu wanayanunua ya Scand kama akina Upendo. Mpaka sasa madereva wake wanakula mishahara wanasubili hayo 50 yatoke.
 
Wanaleta mabus YonTong za kichina according to dataz yapo 50.
Mpaka sasa anauza mabus yale ya zamani yooote naona akina supernajimunisa wanayagombania wanayabadili rangi pamoja na hao wengine hawa wanao penda kununua mabus mabovu wanayanunua ya Scand kama akina Upendo. Mpaka sasa madereva wake wanakula mishahara wanasubili hayo 50 yatoke.
Itakuwa habari njema kama jamaa wataendelea kuwapo. Ni kampuni pekee ya usafirishaji hapa nchini inayoelewa maana ya customer service. Mengine yote hayana tofauti na dala dala za Dar. Rekodi yao ya usalama pia ni nzuri. Hawana matukio ya ajali za kizembe. Tuwaombee washinde majaribu ya kibiashara.
 
Salaam wanaJF! Hii kampuni ilikua ni bora katika usafirishaji wa abiria na parcel katika Afrika Mashariki (ilipata tuzo ya PwC). Ila kwa takribani mwaka 1 sasa sijaona basi hata 1 la kampuni hii! Cha kushangaza ofisi zao Dar na Dodoma zimeendelea kuwepo ila zikitumiwa na kampuni nyingine;kwa Dar,zinatumiwa na Green Star Express na kwa Dodoma zinatumiwa na Al Saedy Express. La kushangaza nyingine ni kua mmiliki wa Scandinavia,Mohamed Abdullah bado anaendelea kuwa mwenyekiti wa chama cha wenye mabasi wa abiria TZ (TABOA)! Sasa nauliza hii kampuni imekufa au? Kama ndio,kwanini mmiliki wake aendelee kuongoza TABOA wakati hana basi? Pia kama ndio kwanini iendelee kua na ofisi zilizoandikwa jina lake hadi sasa? Nawasilisha.
 
aisee hata mimi nimeshindwa kuelewa nini kilitokea.
 
Biashara ilitetereka kimtaji, lakini sasa wameagiza mabasi 50 kutoka China na muda si mrefu watakuwa barabarani, baada ya kuuza mabasi yote ya zamani.
 
wamefuliaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa................. si ze comedi walimuhoji....

kama china,, MKIWAONA WAPE SALAM ZANGU...
 
Kuna kesi ilifunguliwa na kampuni mbalimbali zinazoidai mahakama kuu ili Scandinavia ifilisiwe kwa kuuzwa hayo mabasi ili walipwe fedha zao, kuanzia hapo ndipo ilianza kuteteleka, ila sijui hiyo kesi kama iliisha maana Tanzania kesi inaweza chukua hata miaka kumi.
 
Nilisikia ile kampuni ilikuwa inamilikiwa na akina Sumaye baada ya kupata faida ya kutosha sasa wameamua kugawana kila kitu ili kila mtu aendelee na mambo yake mengine.
 
QUOTE=DaMie;Green Star = Scandinavia

Hata mimi nimesikia ivyo. Je,huo si uhuni na ufisadi!? Mmiliki wa Green Star Express ndie mmiliki wa Scandinavia? Kama ndio,mbona akitambulishwa anaitwa mmiliki wa mabasi ya Scandinavia? Wadau wenye data wanisaidie tafadhali. Mana hapo kuna harufu ya uhuni.
 
QUOTE=Ndibalema;Nilisikia ile kampuni ilikuwa inamilikiwa na akina Sumaye baada ya kupata faida ya kutosha sasa wameamua kugawana kila kitu ili kila mtu aendelee na mambo yake mengine.

Sasa mbona bado wanahodhi majengo ya ofisi wakati kampuni haina basi hata 1? Na mbona bado kuna mtu anaejitambulisha kama mmiliki wa mabasi hayo.
 
QUOTE=Majimoto;Biashara ilitetereka kimtaji, lakini sasa wameagiza mabasi 50 kutoka China na muda si mrefu watakuwa barabarani, baada ya kuuza mabasi yote ya zamani.

Duh! Ina maana inawezekana ni kweli kua kampuni ya BEN BROS inayoingiza mabasi aina ya Yutong nchini ni ya kwao pamoja na BWM? Watarudi kwa jina la Scandinavia au wameshaanza kurudi kiujanjaujanja kwa jina la Green Star Express?
 
QUOTE=Mchapaji;Walianza kwa kufunga ofisi zao za Kampala, wakaja za Nairobi then wakahamia za TZ huko Dodoma, Morogoro na Mbeya juzi juzi na final Zambia.
Wale wa Dodoma wanadai kampuni imeuzwa na mnunuzi ana mpango wa kubadili jina...



Ofisi zimefungwa kwa matumizi ya Scandinavia Express,hazijauzwa bali zimekodishwa kwa kampuni nyingine. Dar zinatumiwa na kampuni ya Green Star Express, Dodoma zinatumiwa na Al Saedy Express,Iringa zinatumiwa na Sumry. Morogoro na Arusha zimefungwa tu. Lakini izo zote zinazotumiwa na kampuni zingine pamoja na zilizofungwa,bado zimeandikwa jina la Scandinavia Express!
 
Ni kweli mengi ya mabasi ya Scandinavia Express,aina ya Scania Marcopolo Andare na Viaggio yameuzwa kwa kampuni za Al Saedy,Upendo,Zuberi,Champion,Super Najmunisa na Sabena.
 
QUOTE=Fidel80;Wanaleta mabus YonTong za kichina

Ni Yutong.
 
Back
Top Bottom