Kifo cha Lowassa kuombolezwa kwa Siku 5 kuanzia leo

Kifo cha Lowassa kuombolezwa kwa Siku 5 kuanzia leo

mwendo umeumaliza mzee wetu pumzika kwa amani sasa, Mungu amekuchukua kwa wakati ulio sahihi kwake, nakumbuka ulivodhihakiwa.
 
Anastahili sana.
Kuanzia leo naomboleza kwa kumuweka kwenye maombi maalum.apumzike kwa amani.
 

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo kuanzia leo February 10,2024 kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) ambaye amefariki Dunia saa nane mchana leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa kiongozi huyo mstaafu alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kujikunja utumbo, homa za mapafu na shinikizo la damu.

Katika kipindi cha siku tano zote za maombolezo bendera zitapepea nusu mlingoti Nchi nzima.

Soma:
- News Alert: - Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais wa CHADEMA 2015) afariki dunia
Hatutaenda kazini au?
 
Hawakujua dunia mapito walipolimbikiza Mali za wizi
 
Back
Top Bottom