Kifo cha Mustafa Kamal Ataturk laana za allah zimshukie

huyu si ndio alitudanganya idadi ya misikiti iliyopo Dar es salaam uwongo wake anauhusisha zaidi na dini
Rodrick...
Ikiwa umenikusudia mimi hilo swali nakusihi tuzungumze na kujadili kwa adabu.

Nikumbushe kuhusu hili la misikiti ya Dar es Salaam kwani sikumbuki kama nilipatapo kuwa katika mjadala huo.

Tujaalie nimesema jambo ambalo si sahihi hilo inawezekana lakini haiwi kudanganya.
 
Braza...
Tatizo ambalo tutakuwanalo hapa Majlis ni kupishana wa uelewa.

Nimechangia kama mabandiko mawili katika mjadala huu lakini inakuwa kama vile hakuna anechukua kutoka hapo akaendeleza mjadala.

Anaechangia anakuwa kama hasomi post za nyuma au kama kasome hakuelewa lolote.

Nimesema katika bandiko langu lililopita kuwa ardhi kupigwa sururu na ardhi isichimbike
na tabu mtu kuamini ingawa inawezekana.

Nikasema kuwa kile kitendo cha Ataturk kuwa hakuzikwa maana yake ni kuwa ardhi imemkataa kwa sababu Kemal Ataturk kama ni Muislam alitakiwa azikwe lakini yeye hadi leo maiti yake iko juu ya mgongo wa ardhi.

Kuna kitu Waingereza wanaita ''figurative meaning,'' mathalan mtu akasema, ''He is running away from the truth.''

Hii maana yake si kuwa anatoka mbio kukimbia kwa miguu yake bali anaukataa ukweli.
Hii inaitwa, ''figurative speech.''

Ndipo inaposemwa Ataturk ardhi imemkataa.

Swali inaweza kuwa iweje asizikwe ili hali yeye ni Muislam na Waislam hawahifadhi maiti ila huzikwa ardhini?
 
Inaonekana umeyasoma hayo maandiko kishabiki, hebu yarudie tena!

Yakobo anaiba baraka!??? How???

Utaratibu wa kuwanyanyua viumbe wake wakiwa hai hauulizwi na kiumbe yeyote maana yeye mwenyewe (Mungu) ndio kaamua. Unaulizia kuhusu kutokunyanyuliwa kwa Muhammad (s.a.w) kama kipimio cha kuonesha uwezo wake Mwenyezi!?? Lol
 
Okay ngoja waje wataalamu wa historia.
Uongo mtupu.

Historia ya Ataturk imeandkwa vizuri katika kitabu kinaitwa "Grey Wolf, Mustafa Kemal. An Intimate Study of a Dictator".

Nimekisoma. Hakina uongo wa hadithi hizi za ardhi kukataa maiti na chagizo zake tulizoambiwa hapa.

Dini ikitumia uongo ili kitisha watu waiamini inakosa hoja yoyote ya kuifanya iheshimike.

Waislamu hawampendi Ataturk kwa sababu alikuwa secular leader aliyekataa kuendesha nchi kidini.

Mimi namuheshimu sana kwa uamuzi huo. Ameitoa Uturuki kutika Ufalme ulioanguka wa Ottoman mpaka kuifikisha kuwa nchi ya kileo.

Ataturk ni bonge la kamanda ambaye hakuyumbishwa na Waislamu wenye siasa kali.

Pia, wanaoamini Mungu hawafi kwa kuugua?
 
Udugu tulonao kati ya mie na weye ni udugu wa jinsi; wewe ni binadam na mimi ni binadam na asili yetu wote ni moja.


Wewe ulisema hayo maelezo ni aya na zurri akaja akathibitisha ukweli wa hayo maelezo lakini hakusema kuwa ni aya kama ulivosema wewe. Tatizo lilipo si kwenye maelezo bali ni asili ya maelezo, wapi yametoka!?? Je, ni aya au hadithi? Sasa wewe kwa vile unasukumwa na mihemko ukashindwa kumuelewa zurri alikuwa anakizungumzia kitu gani.
 
Hawa jamaa kama Nyerere angekua muislam na akaunda serekali scular Tanzania wangemlaumu na. Wangekuja na hadithi za kuungaunga kuhusu nyerere ! Hawana wema wanataka kila kitu kiende kwa misingi ya dini
 
Ukiona hauelweki au wengi wamekuelewa tofauti na ulivyokusudia;ujue hukujieleza vizuri.
 
Hawa jamaa kama Nyerere angekua muislam na akaunda serekali scular Tanzania wangemlaumu na. Wangekuja na hadithi za kuungaunga kuhusu nyerere ! Hawana wema wanataka kila kitu kiende kwa misingi ya dini
Kidadari,
Raha ya kujadili jambo ni kuwa uwe unalijua.

Laiti ungelimsoma Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).
Usingeliandika maneno hayo.

Lakini hujui.

Kitabu cha Bergen ilipojulikana kimeandika nini kitabu hiki kikaondolewa kimya kimya katika soko. Kilikuwa kinauzwa Cathedral Bookshop.



Kitabu cha Sivalon halikadhalika ilipokuja kujulikana nacho kimeandika nini kimya kimya nacho kikaondolewa katika soko.

Kitabu cha Njozi serikali imekipiga marufuku.
Ni kosa la jinai kuwa nacho.

Haya ni mambo mazito sana wahusika wenyewe wanaolaumiwa wako kimya mnaokuja kuwajibia ni watu kama wewe ambao hawajui lolote katika yale ambayo Waislam wameshaieleza serikali miaka mingi nyuma.

Rais Mkapa alisema Waislam wampe ushahidi wa kisayansi na ushahidi alioutaka akapewa na Prof. Hamza Mustafa Njozi.

Kitabu hakikuruhusiwa kisomwa.

Somo hili nalijua vizuri nimelitafiti, kuandika na kutoa mihadhara kadhaa:
  1. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)
  2. The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam).
  3. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam).
  4. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).
  5. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).
  6. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27th February – 4th March 2004).
  7. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11th April 2004).
  8. Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8th - 10th February 2006).
 
Ukiona hauelweki au wengi wamekuelewa tofauti na ulivyokusudia;ujue hukujieleza vizuri.
Bradha,
Wewe umenielewa?
Usiwasemee wengine ikiwa hawakuelewa watanifahamisha.

Lakini hilo sidhani.
Jitahidi tufahamiane.
 
Thanks mtaalamu kwa nondo za ukweli zisizo na shaka,Dini tumeletewa tu na lengo lake lilikuwa kuleta amani(kutisha watu wawe wapole).
 
Kiranga,
Umekisifia kitabu cha cha Ataturk kilichoandikwa na H. C Armstrong, The Grey Wolf, Mustafa Kemal. An Intimate Study of a Dictator," kilichochapwa 1932.

Vitabu vinaishi na kufa kama binadamu.

Kitabu kimetoka Uturuki aliyoitaka Ataturk bado changa, Uturuki iliyopiga marufuku mila zote za Kiislam na kuleta Uzungu yeye akiamini Uzungu ndiyo maendeleo.

Yeye mwenyewe akitumia ulevi na kufanya mengi ya ufuska kinyume na Uislam.
Wametokea wengi wa kumpenda na kumuunga mkono na haishangazi

Haya wewe hukuyagusa umekisifia kitabu tu kuwa kinaeleza ukweli na umezungumza kuhusu dini kutumia uongo na kusema kuwa Ataturk anachukiwa na Waislam kwa kuukana Uislam.

Nitaanza na uandishi wa kitabu kwani hii ni fani yangu nikiwa mwandishi wa vitabu kadhaa na katika somo la historia kama alivyofanya Armstrong.

Ukweli wa kitabu hauwezi kutokana na msomaji mmoja inataka somo hili lifanyiwe utafiti na waandishi zaidi ya mmoja kutafuta hiyo kweli.

Kuna kitabu hapa hapa nyumbani kinaitwa Historia ya TANU 1954 - 1977 kimeandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni (1981).

Mimi nimeandika historia ya TANU (1998) somo hilo hilo lililoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni.

Nakupa changamoto soma vitabu hivi viwili na ufananishe.

Sihitaji kukitaja kitabu changu kwani ni maarufu wengi hapa Majlis wanakifahamu na wengine wamekisoma.

Mfano wa kitabu cha Armstrong uliouleta hapa ni sawa na kutoa mfano wa kitabu chochote kilichoandikwa kokote katika nchi yeyote wakati wa uchanga wake.

Ukipenda unaweza ukakiangalia kitabu hiki, ''The Ottoman Empire The Classical Age 1300 - 1600,'' (1973) cha Halil Inalcik ili ukielewe zaidi kitabu cha Armstrong.

Ningeweza kukupa mifano hai ya hapa nyumbani vipi waandishi wanavyoweza kwa makusudi kuvuruga historia na na mifano hii ni ya waandishi wenye majina kama John Iliffe (1970) na Alfred Tandau (1964) ambao wameandika historia na kuzipindisha.

Hadi leo kuna wanafunzi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wanapewa rejea za waandishi hawa wanazisoma na kuziamini.

Kwa kuhitimisha nakupa ushauri ii ujenge uelewa wako katika masomo kama haya.

Ikiwa unataka kuelewa zaidi ''ubaya'' wa Waislam wenye siasa kali ambao Ataturk aliwatoa madarakani itakuwa na faida sana kwako ukaisoma historia ya ''Inquisition.''

Ho Chi Minh kama Ataturk na yeye hakuzikwa kama Lenin.
Unajua nini watu hawa kinachowaunganisha na kipi kinachowatofautisha?
 
Mpinga Uislam utaachaje kuwa upande wa mpinga Uislam?

Itakuwa ni maajabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…