Kifo cha mwanangu kipenzi kimetokana na uzembe

Mpe kwanza pole mwenzio, usiwe na moyo kama mfupa, khaa hii twabia sio njema
Pole ntampa akishajibu ila uzembe kama huo pia ulishafanyaga nikampoteza kaka yangu. Yeye alikuwa na pumu alitakiwa apige ile sindano mapafu yaachie Hospitali ya jirani wakawa wanataka buku 5 enzi hio ni 2001.

Wakakaza hawamchomi mpaka hela ilipwe kilichotokea kakaa mpaka mzee aliporudi jioni ndio kumkuta hali ni mbaya sana. Huduma hakuna ile kumpeleka amana kafia njiani.

Hio tabia ya kishenzi ipo sana mahospitalini.
 
Inaelekea ulitumia bima ya afya na kadi inaonesha muda wake haujaisha, kwanini wasiruhusiwe kutia huduma kwanza na mambo ya mtandao yakafuata baadae?
 
Mazingira yapi mbona mimi niliwaambia waseme wanachotaka watanzania tutakufa wengi nankupoteza wengi kwa uzembe wetu hakika inaumiza sana mwnangu naumia sana jamani naumia nimekuja humu mnipe faraja angalau nashindwa naumia nalia kila wakati sijui nimekosea nini mimi kupewa hii adhabu ya maisha ya mwanangu
 
Vifo tanzania ni uzembe hasa mahospitalini
 
Waseme wanachotaka...

Pole sana ila kama ungeweza kuwapa wanachotaka, ulishindwa kweli kumpeleka hospitali nyingine?
 
Kwanza tujue tatizo ni nini kabla ya kutoa lawama. Network ambayo ilikuwa mbovu ni ipi? Internal au external? Kama ni external tatizo lipo hapo hospital ie connectivity au kwenye server ya vendor (bima)?
Ni vizuri ungetaja jina la hospital
 
Dah, pole sana asee.
 
Pole sana
 
wiki iliyopita nilimpeleka jirani mmoja hospitali kubwa tu hapa arusha, tumefika saa 10 usiku maana alikuwa anahema kwa shida akikaa na akilala anashindwa kuhema.

Tumefika nikakimbiza bima chap chap daktari akaja akampima akasema oxygen iko chini hivyo anatakiwa awekewe oxygen, mara akasema mpeleke maabara akatoe damu nikawa nawaza damu ya nini na mtu ana matatizo ya kupumua?

saa 12 asubuhi ikafika majibu ya damu yakatoka hana malaria na damu iko fresh, nikamuambia ndugu yake apa tutapoteza mtu tukambeba tukamkimbiza hospitali flani ya wahindi pale wakasema mara hatuwez kutumia bima tena mambo kibao.

ndugu yake akatoa pesa basi akapimwa moyo na mambo mengine akalazwa sasa hivi anaendelea vizuri.

hizi hospitali zimebaki na sifa ya kudumisha usafi tu mambo mengine hamna kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…