Japo ni mipango ya Mungu lakini asilimia kubwa sana za vifo vinavyotokea mahospitali yetu ni sababu ya uzembe na dharau.
Asilimia kubwa ya hospitali hasa za serikali hazina huduma za maana usiku. Ukienda hospitali usiku unakutana na manesi wenye visirani na kama kuna dokta basi kalala fofofo hana hata habari.
Maabara unaambiwa hakuna mtu, mpaka ukija kupata huduma ya maana basi kumekucha na ikiwa ni maradhi ambayo yalihitaji kipimo cha haraka ili kutibiwa yanakuwa yashakumaliza.
Yote kwa yote, Mungu akupe subira katika machungu unayoyapitia. Ikiwa ni faraja yeyote kwako, basi elewa kuwa kijana wako yupo mahala pazuri zaidi. Pole.