Kifo cha Nusra wa UDOM Bado ni pasua kichwa, UDOM waikana taarifa iliyosambaa

Kifo cha Nusra wa UDOM Bado ni pasua kichwa, UDOM waikana taarifa iliyosambaa

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Kuna nini kimejificha nyuma ya kifo cha huyu Binti?? Anadaiwa kufariki tarehe 29/04/2023 ila taarifa zimeanza kuzagaa Leo kwenye social media. Kuna maswali mengi kama haya....

Haya maswali yamechukuliwa sehemu nyingine, sio yangu.
IMG-20230504-WA0044.jpg
IMG-20230504-WA0052.jpg


Mwanafunzi wa UDOM, Nusura Hassan Abdallah anafar-
iki 29/04/2023 kifo chake kinatangazwa 04/05/2023, siku
6 baadae?

Hakuna taarifa za Jeshi la Polisi (pia kutoka kwa
tabibu) za kuuwawa kwa (kwa kipigo) Nusura, Moshi,
Kilimanjaro hadi sasa.

Hakuna taarifa za kukamatwa kwa huyo aliyetajwa bila
jina kuwa "mpenzi wake. Mtuhumiwa pia hajatajwa
popote katika taarifa.

UDOM, Wamefahamu vipi alikwenda Moshi kwa
mpenzi wake? Kwanini wamtambue ni mpenzi wake?
Walizungumza na marehemu?

UDOM walijuaje chanzo cha kifo cha Nusura ni kupigwa
na mpenzi wake? Walifanya postmortem? Walipewa
taarifa za kitabibu? Na nani?

Pia unaweza kusoma hapa

 
Tunaamini akili ni kujua Log na Calculus, na kiuhalisia maprofesa wetu huko chuoni wanajua sana hayo mavitu. Ila kama utawaletea malaika tambuzi wa siri atuambie akili walizonazo majibu yataonyesha wana mafuvu ya mavi tu. Wasomi wetu wanafanya vitu vya ajabu sana huko vyuoni. Ni mwendo wa sup za kimapenzi tu.
 
1683232347885.png


Kwa hii picha anaonekana ni mrembo, sijui mofoloji inasemaje.....

Vyovyote stori itavyokuwa, nawapa pole wenye majonzi ya kweli, (wazazi) kama wako hai, kaka na dada kama anao na rafiki zake wa karibu.

Apumzike kwa amani binti mwanachuo.

Kuna usemi ulikiwa unasema, MJINI CHUO KIKUU.....

SASA UKIFIKA CHUO KIKUU SIJUI UNAKUWA UKO MJINI TAYARI....🤔🤔🤔

Zile orientation course wanafanyiwaga wanachuo kila mwaka wanaojiunga mwaka wa kwanza, inatakiwa iwe na mafunzo mengi hasa namna ya kuishi chuoni, kukabiliana na wanazuoni, kuona sasa si mtoto wa sekondari tena sasa umemachua na u kundi la watu wazima, ukue na ujitambue kisaikolojia na ujue hapo chuo umefata nini na kubaki kwenye lengo lako bila kuyumbishwa na vishawishi......

DOTS CONNECTED.....

CHUO KIKO DODOMA

BUNGE LIKO DODOMA

WAFANYABIASHARA WENGI WAMEWEKEZA DODOMA BAADA YA MAGU

MOSHI....!!!?????🤷‍♀️🤷‍♀️🤷‍♀️

Alamsiki.
 
Back
Top Bottom