Down To Earth
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 21,940
- 16,643
Habari za sasa wadau wa celebrities forum. ni matumaini yangu mu wazima kabisa!
Jalada lililoko mbele yenu sasa linazungumzia mustakabali mzima wa tasnia ya filamu Tanzania ambayo imepewa jina la bongo movies. tasnia hii imekuwa ni sehemu ya soko la ajira la vijana wengi ambao wamekuwa na vipaji mbali mbali vya uigizaji na hata ambao hawakuwa na vipaji lakini wamefunzwa na kuweza kumudu mikiki mikiki ya filamu kama vile Jackline wolper, ray na kajala masanja, hawa ni baadhi ya wasanii tu ambao wameingia kwenye tasnia by influence of others, lakini kwa bidii zao wameweza kumudu haswaa soko la ndani la filamu Tanzania. sijafahamu hali ya nje huko ikoje, lakini kwa upande wa ndani, kwa kiasi fulani wanasikika japo si saana!
Aidha, tasnia hii ya filamu bongo, historia iaonesha kuwa ilianza mnamo miaka ya 2000 kama sijakosea na filamu za kwanza kwanza kurushwa zilikuwa ni kama filamu ya girlfriend, filamu ambayo ilifanya vizuri kiaina fulani sokoni kulingana na hali ya kiuchumi kwa kipindi kile na watanzania waliipokea kwa mikono miwili japo awareness juu ya industry haikuwa kubwa saana kwa vile ndo kwanza watu walikuwa wanaanza.
Kadri miaka ilivyokuwa inasonga pole pole, ndivyo vijana mahiri katika tasnia walivyokuwa wanajitokeza kutoka makundi mahiri yaliyokuwa yanajihusisha na ukuzaji wa vipaji vya wasanii kama vile kaole sanaa group ambapo waliweza kuwapika wasanii manguli katika tasnia kama STEVEN KANUMBA THE GREAT na RAY THE GREATEST.
Wasanii hawa wamekuwa chachu hasa ya ukuwaji wa filamu Tanzania ambapo kwa kiasi fulani waliweza kuikuza tasnia na kuweza kupendwa katika mataifa ya nje (afrika mashariki kwa ujumla) kama kenya, uganda, rwanda drc na mataifa mengine yanayozungumza lugha ya kiswahili. mbali na hawa manguli wawili, kuna wasanii wengine pia ambao wamekuwa wasaidizi wakuu hasa katika ueneaji na upendekaji wa filamu hizi za kibongo kama vile wema sepetu, jackline wolper, irene uwoya, aunt ezekiel na wengineo kadhalika, achilia mbali wasanii wanaoigiza filamu za futuhi.
HALI YA SOKO LA FILAMU BAADA YA KANUMBA KUFARIKI DUNIA APRIL 2012.
Ni miaka miwili sasa karibia itimie toka kufariki kwa mpendwa wetu, steven kanumba, steven kanumba alikuwa muhimili mkubwa sana katika taifa hili la Tanzania katika soko la filamu kwa ujumla. SK aliweza kuitangaza nchi yetu kupitia filamu alizokuwa akifanya kwa kuwashirikisha wasanii mbali mbali wa nje kama vile wasanii kutoka nollywood (actually hawa ndio wanaoongoza kwa ubora AFRIKA) kama vile ramsey noah katika devil's kingdom na katika filamu nyingine ya dar to lagos. SK alikuwa mtu wa kujituma, haogopi challenges zilizokuwa zinamkabili, alikuwa anapambana sana na alitoa filamu zenye ubora kwa kiasi kikubwa.
Toka mpendwa wetu SK atutoke toka mwaka juzi, soko la filamu limekuwa mikononi mwa giants kama Ray, Jacob Steven, mtitu william na akina dada kama jack w. gambe, wema sepetu na irene uwoya. watu hawa ni moja kati ya mihimili ambayo tunaitegemea isukume gurudumu la filamu Tanzania toka kufariki kwa mpendwa wetu SK na hata kabla yake kwa sababu ni wajibu wao kufanya hivyo kwa sababu wao ndio wako kwenye soko kama giant producers.
Hali ya upepo wa filamu toka April 2012 imekuwa tofauti sana na sasa!!! soko la filamu limedorora sana kulingana na hali ilivyokuwa zamani. kwanini siku hizi hatuoni vitu hot na vynye ubunifu na bashahsha kama vile vya enzi za kanumba? kwanini hawa wasanii wetu wa sasa wamebweteka namna hii? najua STEVEN KANUMBA alikuwa na uwezo mkubwa saana katika soko, lakini sasa, wasanii hawa wa sasa wameshindwa nini hasa kuigwa kutoka kwa STEVEN?
Jitihada kidogo tuliziona kutoka kwa wema sepetu pale alipotaka kufanya muungano ja omotola jalade kutoka NIGERIA. wema alijitangaza sana kwamba atatengeneza filamu moja na huyu dada celebrity wa nigeria na dunia kwa kiasi kikubwa. hii ilikuwa nafasi ya dhahabu kwa wema binafsi, wasanii wengine wa filamu Tanzania, na hata taifa kwa ujumla! najua ni nafasi ndogo kiasi, lakini ni kubwa sana endapo ingefanyiwa kazi, mfano halisi labda tuone kwa diamond, kitendo cha dp kutoka kimuziki na kuwashirikisha wasanii wa nje kama davido, kimeshampa mwanya wa kutoka kwa soko la nje na kimataifa kwa ujumla! vivyo hivyo kwa tasnia ya filamu tanzania.
Mbali na wema, tunao wasanii wengine kama ray, lulu michael, jacob steven, jackline wolper, irene uwoya, aunt ezekiel, mtitu william na wengineo. ni nini hasa kinawafanya hawa wasitoke nje na kuiwakilisha nchi kisanii? kwanini wanshindwa ku -master soko la ndani kwa kuanzia tu basi, huko nje itakuwaje wadau?
Kwa kumalizia tu niseme, kufariki kwa steven kanumba, the great, kumeweka doa katika soko la filamu na filamu kwa ujumla katika nchi ya TANZANIA. hakuna msanii kwa sasa anaeonyesha jitihada zake kupeleka tasnia nchi kwa nguvu!!
filamu zetu bado ziko katika kiwango cha chini sana! tena sana! nimpe hongera mzee chillo wa pilipili entertainment kwa kuweza kuchukua tuzo ya filamu bora ya kiswahili kutoka africa magic swahili (kama sijakosea). lakini bado, bongowood sijui bongo movies badotuko nyuma sana! viongozi wanaendesha uongozi kwa unafiki, chuki na ukosefu wa elimu baina zao wenyewe!
BADO NAAMINI KUWA BONGO MOVIES ILISHIKILIWA NA STEVEN KANUMBA!
Karibuni kwa maoni.. kosoa unapoweza, jenga unapoweza!