Filamu ni burudani kama ilivyo burudani yoyote...pamoja na mambo mengine, lengo kuu la burudani ni kukonga roho za audience. Katika hili la kukonga roho za audience, na hasa linapokuja suala la filamu, hakuna cha filamu za Kitanzania wala Kiajemi...kinacho-matter ni how namna gani filamu yako imesukwa na ikasukika. Leo hii unaweza kuandika story kuhusu familia za askari wa kikoloni kutoka India ambao waliacha familia zao Bombay na kwenda kupigana WWI huko Korea na kisha ukaonesha ni namna gani familia hizo za askari zinavyopambana na maisha nyumbani wakiwa peke yao na bado filamu ikavutia maelfu kwa malaki ya Watanzania provided story imesukwa vizuri ikasukika...kuna msuko wa matukio unaoeleweka, kuna conflicts zenye mantinki; unapoona watu wanapigana unaridhika kwamba kweli pale walipaswa kupigana, unafika kwenye climax zone; mtu anakupigia simu na unaipotezea..n.k, n.k, n.k...hiki ndicho tunakosa kwenye soko tasnia yetu ya filamu.
Tukirudi kwa Kanumba, sidhani kama alikuwa too far kulinganisha na wenzake coz' wote hawa wanategemea waandishi wale wale na directors wale wale. Kilichokuwa kinamfanya Kanumba awe outstanding from other actors/actress ni kwa sababu alikuwa na uthubutu...hakuona taabu kutumia fedha ili kufanya kolabo coz' aliamini hii ndiyo njia pekee ambayo ingemfanya aweze kuvuka mipaka ya East AFrica. And am telling you, Kanumba alikuwa anafanya kosa moja kubwa la kiufundi. Chance ambazo alizipata za kuigiza na wasanii wakubwa endapo angejiandaa nazo, zingekuwa zimemfikisha mbali zaidi kuliko alipoishia! Ninachomaanisha ni kwamba, ikiwa story zake zilikuwa ni zile za kuandika mwezi mmoja, basi zile ambazo alitaka kufanya international collaboration alitakiwa kuandika miezi miwili...ikiwa alikuwa anatumia sh.500K kununua script, anapopata international collaboration angetumia hata 5 million just for a script. Kwavile kipaji cha uigizaji alikuwa nacho, and in fact, waigizaji wengi wanajitahidi sana; tatizo ambalo lilibaki kwake na ni stori iliyoenda darasani....iliyopangwa ikapangika!
Sasa ni kwanini tasnia inaonekana kupwaya! Kanumba tayari alishaingia kwenye nyoyo za watu...kama enzi za Juma Nature! Nature ilikuwa hata akitoa nyimbo ya hovyo hovyo, itashibikiwa ile mbaya! So, kumshusha Natur enzi zile ilikuwa ni lazima ufanye hatua mia zaidi ya zile za Nature! Ndicho kilichopo! Kwavile Kanumba alishaingia kwenye nyoyo za watu ingwaje siamini kwamba ndo alikuwa far far best than the rest; bado kuwa ktk level yake inabidi watu wafanye mara mia zaidi kuliko alivyokua anafanya! So, am very certain kwamba watu wanafanya sana filamu lakini ndo kama alivyosema
Ruttashobolwa..hazikidhi! Hazikidhi coz' wanafanya business as usual...inawezekana kabisa kwamba level ya stori zao ni sawa tu na ile Kanumba; but kama nilivyosema; the guy was Kanumba and the rest not!