Licha ya kufa kizembe lazima nikiri huyu jamaa alikuwa maarufu. Angalia wakati wa msiba wake;
1.Macho na masikio ya serikali yote yalikuwa sinza ndo maana viongozi wote kuanzia rais,makamu wake,waziri mkuu,mawaziri,mbalimbali,wabunge,vyombo vyote vya usalama,serikali ya mkoa na wilaya zote za Dsm ilikuwa sinza
2.Macho na masikio ya media zote (redio,magazeti,blogs n.k.) yalikuwa sinza,
3.Maazimisho ya kifo cha waziri mkuu wa zamani Sokoine yamepita kimyakimya km panya anavyopita chini ya mlango,hakuna mwenye habari
4.Hakuna mwenye habari km aliyekuwa mkuu wa majeshi katutoka huko Mwanza
5.Kazi hazifanyiki huko maofisini, kila unayemwona anazungumzia kifo cha SK
6.Hata baada ya mazishi maongezi na minon'gono ni kuhusu kifo cha SK
7.Sio watu wengi wanaokiri jamaa alifariki kizembe akifanya uzinzi tena na kitoto kidogo!
8.Kila mtu anadai jamaa ni shujaa anayepaswa kuigwa!