Habari wana jamvi wenzangu?
Mi leo nimeamka na hii,baba yake Steve Kanumba(Mungu amlaze panapostahili), Mzee Charles Kanumba kaweka bayana sababu ya mwanae kutozikwa kwao Mwanza kwa babu yake ambaye ni baba wa mzee C.Kanumba...
Mzee C.Kanumba alidai kuwa kwao kabisa ni mkoani Mwanza, wilaya ya Magu katika sehemu moja inayoitwa Nasa(pembeni kidogo ya Magu mjini, barabara iendayo Musoma)....
Hivyo mwanae alipaswa akazikwe huko kwao walipozikwa ndugu zake wengi tu waliotangulia kabla yake..
Ila tatizo ni miundo mbinu ya huko ni mibovu hivyo ingewachukua muda mrefu na fedha nyingi kuikarabati na kuifanya ivutie kwa ajili ya mazishi mtu maarufu sampuli yake.Alidai hiyo ndio sababu kubwa iliyomfanya kuridhia mwanae kuzikwa Dar es salaam katika makaburi ya Kinondoni.
Pendekezo langu:Wanajf wenzangu tupakumbuke na tupakarabati nyumbani kwetu pamoja na kujiandaa maana hatujui siku wala saa
CHANZO CHA HABARI: Gazeti la Mzawa kutoka Mwanza hutolewa kila Jumamosi.