Mh nilikuwa nasubiri mtu aanzishe huu uzi maana kwenye twitter nafasi ni fupi sana ya kupost.
We are all not sure kama Lulu ndiye alimuua Kanumba. kuwa nae chumbani haimaanishi kuwa ndo muuaji. Biology nilisoma kidogo ila sijawahi kusikia eti ukigonga kichwa kwa kitu kigumu kama ukuta basi unatoa mapovu. Mapovu yanahusiana na kula au kunywa (Drs wanaweza kusaidia hapa kwa technical terms).
Kuna maswali ya msingi hapa.
1. Lulu aliletwa na nani kwa Kanumba
2. Lulu alikuwa anaongea na nani kwenye simu iliyoleta huo ''ugomvi'' na Kanumba?
3. Alipokimbia aliondoka na usafiri gani wakati yeye ndo alimwambia mdogo wake kanumba kuwa kaka yako kaanguka?
4. Ray alikuwa na bifu na kanumba la mda mrefu na alimuahidi eti watamalizana kiume, na sasa ray anasema alipopigiwa simu alikuwa jirani na muhimbili. alipigiwa simu na nani na alipigiwa simu kama nani wakati hawakuwa marafiki wa karibu tena?
kwa nchi yetu ambayo haki ya mtu inaweza ikauzwa ili apewe mwingine, Lulu lazima apate msaada wa kisheria ili aweze kufunguka katika kumtafuta muuaji halali wa Kanumba. Kuwa nae ndani haimaanishi ndo muuaji ila kwa kuwa alikuwa eneo la tukio lazima aisaidie polisi mpaka ukweli ujulikane.
Zitto na Halima wamefanya vizuri na nawaomba mama Bisimba na Usu malya nao wamsaidie huyu mtoto.
Anahitaji msaada wa kisaikolojia maana kampoteza mpenzi wake na hili tukioo ni kubwa sana kwa umri wake na mazingira yalivyotokea.
With a fair trial to Lulu, the truth will be revealed and it may surprise us all