Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Mama lulu aongea na wanawake live nakuomba msaada wa mwanasheria ili kumsaidia mwanaye.

Source: channel five - wanawake live

Ni majonzi makubwa sana kwa mama ya binti huyu Lulu, Ila napenda kujua na kufahamu hii kesi itakvyo endeshwa katika nchi yetu hiiii.

Kwani nina uhakika ina mapungufu ya kitaaluma makubwa sana na pamoja tuna wana taaluma walio bobea.

My Take;

Itakuwa among the Unsolved Case


 

Hivi wewe unajua maana ya 'except'???? Jaman hiz lugha za watu ni ngumu!!
 

mtoto wa mama ,aliekwambia kuchunga mbuzi na kuosha vyombo ni mateso nani?hayo ndo mateso ambayo kanumba alikuorodheshea ? Umebahatika kulelewa na wazazi wako wawili shukuru mungu,habari za mama wa kambo tuulize cc tuliepitia maisha hayo..
 
Ni funzo pia kwa SK kwamba 'WAHESHIM BABA NA MAMA UPATE MIAKA MINGI NA HERI DUNIANI'

ahaaa ,kumbe Amina chifupa,regia,vivian ,complex,mtoto wa dandu,motie mengi walikuwa hawawaeshimu wazazi wao,?
 
KiFO CHA kANUMBA –MASWALI MENGINEYO




kwa mujubu wa mtuhumiwa Kanumba alianguka na kujingonga ukutani na kufariki ndani ya muda mfupi

kwa mujibu wa shahidi mdogo wake na Kanumba, sETH, alisikia mzozo kati ya kanumba na Lulu kuhusiana na lulu kupiga simu kwa wanaume wengine, anadai kanumba na lulu walijifungia chumbani, na aliskia vishindo. Kabla ya Lulu kufika Kanumba alimwambia mdogo wake wajiandae kutoka.. HEBU TUJIULIE MASWALI MADOGO



  1. Mpaka Lulu anawadia (saa hatujui) Kanumba alikuwa mzima na anajiandaa ama yupo tayari kutoka. Tunaambiwa alikuwa anakunywa Whisky (kwa hiyo tuseme amelewa kwa kiasi fulani). Alikunywa whisky chupa nzima? Au chupa ngapi? Kachanganya na nini? Tukumbuke pombe inaua, unaweza kupoteza nguvu na kuanguka kwa kishindo na kufa!
  2. Lulu (anagonga geti?) anaingia ndani, nani amemfungulia geti na mlango, Kanumba au mdogo wake Kanumba, Seth?
  3. Kama ni Seth, je aliwaona watu au mtu mwengine yeyote walioambatana na Lulu? Aliona gari alilokuja nalo Lulu? Namba zake anazikumbuka? Gari liliondoka au lilipaki ?
  4. Lulu anaingia ndani, nini kilitangulia? Salamu kwa kanumba? Je kuna mazungumzo yoyote yalianza kati ya Lulu na Kanumba au Lulu na mdogo wake kanumba? Au ugomvi ulianza moja kwa moja?
  5. Kama yalikuwepo, Mazugumzo hayo yalihusu nini?
  6. Mzozo hasa ulianzia wapi?
  7. Wakati mzozo unaanza na kuendelea, mdogo wake Kanumba alikuwa sehemu gani ndani ya nyumba, sebuleni, chumbani kwake, nje ya nyumba? Tujue kama alikuwa anasikia mazungumzo au mabishano yanayoendelea
  8. Je alienda kuwagongea.? Akaambiwa nini?
  9. Je kweli Lulu alipiga simu kwa mtu mwingine wakiwa na Kanumba? ALipiga ama alipigiwa?
  10. Huyo mtu aliyepigiwa simu ni nani? Records za simu zinaonyesha nini?
  11. Kama Lulu alikuwa na mpango wa kuwasiliana na wanaume wengine, kwa nini hakufanya hivyo kabla ya kufika nyumbani? Kwa nini hakupiga simu akiwa kwenye gari au huko alikotoka hadi aje apige simu akiwa na Kanumba?
  12. Baada ya kuulizwa na Kanumba kuwa unawapigia kina nani simu, Lulu alijibu nini?
  13. Tunaambiwa alikimbia kwenda kuongea nje, kwa nini akimbie nje kama alishaamua kupiga simu mbele ya mpenzi wake Kanumba na sio kabla ya hapo?
  14. Ina maana mlango haukuwa umefungwa baada ya Lulu kuingia?
  15. Je Kanumba alimfuata huko nje? (Mdogo wake ataweza kusema hili)
  16. Lulu alijibu nini kwenye mzozo wao na Kanumba? (ambacho labda kilimuudhi Kanumba)
  17. Chumbani alimokuwa Kanumba kumekaaje? Kuna kitanda (kikubwa)? Kuna makochi? Au vitu vvoyote vilivojaza humo? Kabati?. Endapo ama vitanda na makochi tunategemea mtu anaengauka angeangukia kwenye kitanda ama makochi ama viti ama kabati ama meza. Sio lazima iwe ukutani.
  18. Pale alipogongesha kichwa ukutani, uchunguzi umefanyika? Kuna nywele zozote zimebaki? Kuna damu imevujia au mabaki ya ngozi ya kichwa? DNA? Kama hakuna kweli tuamini alijigonga ukutani?
  19. Kama kulikuwa na mzozo Kanumba alikuwa analalamikia nini? Na mtuhumiwa alijitetea nini? Tujue kama Kanumba alianguka na kuzimia baada ya kuambiwa kuwa unashika pembe tu hapa au vipi!
  20. Baada ya kanumba kuanguka Lulu alifanya nini? Alipiga kelele? Alilia?Tunaambiwa aliomba msaada kutoka kwa mdogo wake Kanumba. Ilipita muda hadi mdogo wake kanumba alipoitwa na Lulu? Ugomvi ulishamalizika? Au ni katikati ya majibizano? Kama aliitwa nusu saa baadaye, tujue kilichokuwa kinaendlea chumbani
  21. Tunasikia Lulu alikimbia nje ya nyumba? Alikimbia huko kufanya nini? Alipiga simu kuita ambulans au marafiki wa karibu?
  22. Je kuna uwezekano wowote kuwa Kanumba alipigiwa nje ya nyumba na kubebwa kuletwa ndani ya nyumba? Kwa maana hiyo suala la Lulu kukimbia nje kuongea na simu ilkuwa ni hadaa/daganya toto ya kumfanya Kanumba atoke nje akutana na wabaya wake walioandaliwa? Hii inategemea majibu ya swali namba 15 kama Kanumba alimfuata Lulu huko nje kujua anaongea na nani.
  23. Kinywaji alichokunywa kimepimwa kama kina sumu?majibu yanasemaje.Tusubiri ripoti.
  24. Uchunguzi wa madakati kuhusu kifo unasemaje? Nasikia wamekujaa na konkulusheni kuwa ni brain concussion. Mtikisiko wa ubungo! Uliosababisha respiratoru failure!
  25. Kweli brain concussion huweza kusababisha kifo endapo umesababishwa na pigo kubwa( violent shaking). Inategemea na nguvu iliyotumika. Si kila mtikisiko wa ubongo husababisha kifo. Mtikisko mingi ya ubongo husababisha kupoteza kumbukumbu, kuchanganyikiwa, au headache na sio lazima kifo, hasa pale ambapo mtu hakuvunjika mifupa ya kichwa na wala ubongo haujabonyezwa (brain compression). Kama fuvu la kichwa lipo salama (intact), maana yake ni kwamba Kanumba hakupasuka ubongo, na pengine hakuna damu iliyovujia kwenye ubongo. Kweli Kanumba alianguka kwa nguvu zote na uzito wote, kiasi cha kugongesha kichwa chake ukutani kwa nguvu sana na kuharibu ubongo wake? Au alisukumwa kwa nguvu? Kwani kulikuwa na utelezi chumbani? Kwa kawaida mtu anaeanguka hujaribu kuwahi kushika chochote kilichopo karibu ili kujiokoa na kupunguza impact unapofika chini. Ina maana Kanumba alianguka kama mti mkavu? Kuna umuhimu wa kufanya uchunguzi tena?
  26. Je Kanumba na mdogo wake Seth wanaelewana kwa kiasi gani? Na Seth na wazazi wa Kanumba? Je Kanumba aliandika wosia wowote?. Huyo Seth yeye ana kazi gani? Je alikuwa anatazamia kurithi chochote?. Je ana tamaa ya mali?
  27. Je Kanumba alikuwa na dili lolote la pesa au biashara ambamo wametofautiana na baadhi ya washirika wake?
  28. Alikuwa na visa na kina nani? Visa vinavyohusu biashara, mapenzi au wapenzi, umaarufu, n.k....???!
  29. Kama mlango haukufungwa baada ya Lulu kuingia , je kuna uwekekano kuwa kuna watu wengine waliingia?.Seth anadai alisikia vishindo chumbani mwa Kanumba na LULU. Vishindo vingapi na vya namna gani?? Kishindo cha kuanguka ni kimoja. Kweli LULU angeweza kushindilia vishindo vyote hivyo kama vilikuwepo?


MASWALI HAYA HAYANA LENGO LA KUMTUHUMU MTU YEYOTE, BALI
NI MASWALI AMBAYO YANASAIDIA KUTOA MWANGA KUHUSU utata wa KIFO CHA SK,
SOTE BADO HATUJUI NINI HASA CHANZO CHA KIFO,


ReST IN pEACE, SK
 
Ni funzo pia kwa SK kwamba 'WAHESHIM BABA NA MAMA UPATE MIAKA MINGI NA HERI DUNIANI'

wazazi pia wawalee watoto wao kwa mapenzi ili wajisikie kupendwa na hatimae wawaheshimu wazazi wao
 
Yaani vyombo vya habari vinatoa habari tofauti kabisa. Cheki hapo Mwananchi na The Citizen


Alichoeleza Lulu polisi hiki hapa


MSANII Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi kuwa kifo cha Steven Kanumba kimetokana na ugonvi kati yao, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo.

Habari zilizopatikana jana kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa, Lulu alisema kuwa kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye kuzungumza na simu kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake. "Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo Kanumba akamfokea na ndiyo ugomvi ukaanzia hapo," chanzo hicho kimesema.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje na kuondoka kwa gari lake hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari wa Kanumba alimpigia simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali. "Alipororudi Sinza ndipo akakamatwa, lakini walikuja Kituo cha Polisi Oysterbay kuchukua PF3," kilisema chanzo hicho.

Chanzo kiliongeza kuwa tangu Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivu asiye na wasiwasi wowote hata katika mahojiano na polisi. Katika hatua nyingine, Polisi wa kituo hicho jana walipata wakati mgumu baada ya kuibuka kundi la vijana waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika Kanumba, walioandamana wakidai wanamtaka Lulu.

"Tunataka jembe letu", waliimba vijana hao waliofikia 100 wakitokea Barabara ya Ali Hassan Mwinyi huku wakishika majani na kufanya askari waliokuwapo kituoni hapo kuwahi kuchukua silaha na mabomu ya machozi kujiandaa kutuliza ghasia kama zingezuka. Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayari kupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali.

Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/21911-alichoeleza-lulu-polisi-hiki-hapa

Lulu's side story of Kanumba's death

The prime suspect in the death on Saturday of local film star Steven Kanumba spoke out on the tragedy for the first time just a day before tens of thousands of people gathered for his funeral yesterday. Elizabeth Michael, alias Lulu, broke her silence on Monday-two days after she was arrested. Investigators at Oysterbay police station had to engage a crime psychologist to get her to open up on the events leading up to the death of the star who had just been invited to Hollywood in the United States.

Highly placed police sources told The Citizen in an exclusive interview yesterday that Lulu, girlfriend of the deceased, started narrating what had transpired on the night the 28-year-old died after meeting the psychologist. "The suspect, who had refused to cooperate with police detectives from the Kinondoni regional police office, has now managed to speak for three hours with the psychologist," the sources said on condition of anonymity since they are not official spokespersons of the Tanzania Police Force.

The psychologist from the Criminal Investigation Department (CID) headquarters in Dar es Salaam chatted candidly with the suspect for three hours on Monday, a day before Kanumba was buried. Lulu reportedly told the investigators that Kanumba phoned her on the fateful night asking her to join him for an outing. She went to his home but told him she did not really want to go out and that she preferred to return home.

Kanumba allegedly wanted Lulu to accompany him to a Mashujaa Band show at Vingunguti, and became furious when she refused to accompany him. According to the sources, the misunderstanding between the two developed into a quarrel, with Kanumba demanding to know what it was that she had left at her home."According to Lulu, the deceased locked the door to his room," said the sources. "In a panic, she unlocked the door and fled."

Lulu is quoted as saying that she managed to escape after he fell and had no idea what transpired after her departure. The sources said police have also interrogated another suspect, a Bongo Flava musician (name withheld), who gave Lulu a lift when she left Kanumba's Sinza residence. "I am sorry, brother, I cannot comment on that issue," he told The Citizen before he hang up. According to detectives, other suspects have also been lined up for questioning. The sources could not say how long the interrogations would take.

In another development, the sources said heavyweight politicians related to Lulu have been sending her consolation text messages pledging to assist her. "Their involvement with the suspect could complicate our investigations," said the sources. Yesterday, this paper reported that Kanumba died of a brain injury caused by a sudden blow to the head.

One of the doctors who examined Kanumba's body at Muhimbili National Hospital hinted that the actor died on the spot after suffering such severe brain damage that he collapsed and stopped breathing. His sudden death sent shockwaves across the country, East Africa and West Africa-particularly Ghana and Nigeria-where he had achieved prominence in the continent's leading film industry, Nollywood. He had returned home from a trip to Ghana just a few days before his death.

Source: The Citizen: Lulu
 
Lulu is quoted as saying that she
managed to escape after he fell and
had no idea what transpired after her departure
Kwa hiyo zile habari za kwamba alienda kumuita mdogo wake SK kuwa jamaa ameanguka ni uongo?
Na habari tena kwamba alimuona jamaa anaanza kulegea na kuanguka ni uongo?
Huyu mtoto kitakachokuja kum cost ni kutokuwa mkweli watu watashindwa hatat jinsi ya kuanza kumsaidia., Sidhani ka yupo serious kusema hakujua kilichotokea hadi anaondoka
 
Hivi unapoamua kuandamana na kicheche, wivu wa nini?

Hivi hamuwezi kuwa wasanii na sehemu zenu za uzazi mkazitumia kama ilivyokusudiwa mpaka mkapatwe na mabalaa ya namna hii?

Mtoto mdogo ana mabwana 6, kisa umaarufu, poh!
 
Right now it's just her word against whatever evidence they managed to collect. No smoking gun.

She has a good chance of walking free.
 
Right now it's just her word against whatever evidence they managed to collect. No smoking gun.

She has a good chance of walking free.

Tatizo anajichanganya, kama kweli hizo habari ambazo tunaletewa zinatoka kwake.
 

Kumbuka kuwa katika mazingira ya mwanzo habari huwa ziko nyingi sana na ambazo si za uhakika. Mwisho wa siku nina imani tutapata tu simulizi iliyonyooka.
 
Right now it's just her word against whatever evidence they managed to collect. No smoking gun.

She has a good chance of walking free.

What about the "heavyweight politicians" who have been sending her consolation text messages pledging to assist her?
 
Tatizo anajichanganya, kama kweli hizo habari ambazo tunaletewa zinatoka kwake.

Yaliyotokea ni makubwa mno kwa mtu yeyote yule kuyahimili.

Yeye kupatwa na kiwewe ni jambo ambalo linategemewa.

Mimi sitegemei binti mdogo mwenye umri kama wake kuwa na utulivu akili kiasi cha kutoa simulizi iliyonyooka hususan baada ya mtu maarufu aliyekuwa naye chumbani kufa mbele yake.

Natumaini watazingatia pia hali yake ya kiakili na kihisia ya wakati huo katika maamuzi yao ya kama wamshitaki au la.
 
What about the "heavyweight politicians" who have been sending her consolation text messages pledging to assist her?

Nothing wrong with that because there is no legal case that is sub judice.

And she does deserve assistance. Or doesn't she?

"Heavyweight politicians"? I wanna see some names and judge it for myself if they are indeed "heavyweight".
 
Nadhani ka inawezekana wangemuacha kwanza kwa muda wasimuhoji chochote, kama kweli aliyemuhoji ni mtaalamu wa psych nadhani itasaidia..Af tatizo jingine hao polisi ndo wanazidi kuchanganya watu kwa kuripoti kila siku habari tofauti tofauti, kwa nini wasimalize kwanza upelelezi wao ndo waje na habari kamili?
 
Reactions: EMT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…