Kama Polisi wangeamua kuifanya hii kazi ya kupepeleza kifo cha Kanumba kiprofessional tayari hadi muda huu wangeshapata stori halisi ya kilichotokea na waache kutusumbua kwa vistori vyao visivyoeleweka, mara stori hii kesho stori nyingine.
Karibu watu muhimu wa kuwasaidia katika hii kesi wanao, kinachotakiwa ni kuwauliza maswali sahihi kwa mtu husika na katika mood sahihi wapate stori inayoeleweka.
Mdogo wake Kanumba na Lulu wanatosha kabisa kuwapa data za uhakika. Halafu ni makosa kuhusisha habari za udaku katika kesi serious kama hii. Vyombo vya habari vinaweza kuharibu objectivity ya uchunguzi.
Wakati mwingine si lazima Lulu ahojiwe kama prime suspect -- uwezekano wa Kanumba kucollapse yeye mwenyewe bila kuguswa na mtu yoyote upo (cardiac arrest, low blood pressure, comes to mind). Lulu ahojiwe, kwa upole na bila nia yoyote ya kumtisha na jela. Umri wa Lulu pia uzingatiwe.