Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Atazikwa kwa taratibu za VATICAN na misa itaendeshwa na balozi wa Vatican hapa nchini
 


TAARIFA YA TANZIA

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) kwa masitiko makubwa linachukua fursa hii kutoa salaam za rambirambi na pole za dhati kwa vijana nchini na hususan kwa wasanii wa fani mbalimbali kwa msiba wa mmoja wa waigizaji mahiri, Steven Charles Kanumba.

BAVICHA inamtambua kijana Kanumba kuwa mmoja wa vijana wapambanaji ambao pamoja na serikali kushindwa kuboresha mazingira ambayo wasanii wangeweza kunufaika na kazi zao ipasavyo kama moja ya maeneo muhimu ya ajira yenye staha, yeye na wenzake wachache walimudu kupambana na vikwazo vingi hata wakaweza kuikuza na kuipatia jina, tasnia ya uigizaji nchini.
BAVICHA tunatambua juhudi binafsi za Kanumba na wenzake, ambazo zilisababisha vijana wengine kuweza kupata ajira kutokana na kazi zinazotokana na mchakato wa hatua mbalimbali za ukamilishaji wa filamu, kuanzia katika utungaji, utengenezaji hadi hatua ya uuzwaji wa filamu hizo.
Kwa dhati kabisa, BAVICHA inapenda kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na kwa Watanzania wote kwa ujumla walioguswa na msiba huo. Tunawaombea kwa Mungu, awajalie moyo wa subira wakati huu wa majonzi makubwa.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Marehemu Kanumba, Amina.
Imetolewa kwa vyombo vya habari na
John Heche
Mwenyekiti wa BAVICHA
Aprili 9, 2012
 
Kanumba atazikwa na kanisa lake as long as alikuwa muumini!.

Yesu alikuja kwa ajili ya waliopotea na determinant ya kuzikwa sio umekufaje bali kama ulikuwa muumini!.
 
Mzee Jangala kafa lini Mkuu?
mi nipo dunia gani? mbona sina habari
 
Kuna baadhi ya wachambuzi wanadhani kifo cha SK kimetekwa "kwa makusudi" na Serikali ya CCM kwa faida wanazozijua wao!

Wengine wanadai ni kudivert attention ya jamii kutoka katika masuala ya Lema na mipango yake...
Wengine eti ni kugain sympathy ya vijana na kina mama mbalimbali wa hapa nchini kwani marehemu alikuwa kipenzi cha vijana wengi na kina mama wengi pia..
 
RIP the legend of film industry in TZ, hatutakusahau haswa kwenye bongo movie sijui itaelekea wapi!
 
Kanumba alikuwa ni enterpreneur ambaye aliajiri/ alikuwa na mpango wa kuajiri Watanzania wengi sana siku za usoni, hivyo kumsaidia JK katika motto yake!
 
alilegea akaanguka? Iyo brain concussion inatokea after sudden impact to head. So something happened before impact. Maelezo yake ni ya uongo. Jela iyooo! Inamuita.

Mahakamani ushahidi unahitajika nyie vp....akisema alikuwa anabadili bulb akadondokea chongo?(Kumbuka ndio shahidi pekee)Mahakama ya Muumba ndio haihitaji shahidi ila ivi za binadamu lolote lawezekana na ndio maana haki haipatikani mahakamani .Inawezekana kihalisia hajausika hata kidogo na akatiwa haiani kwa kushindwa kujitetea..na inawezekana kahusiaka kwa kukusudia au kuto kukusudia asitiwe hatiani akijetetea vema.

 
hili ni tamko la BAVICHA tuletee na la UVCCM.
 
RIP Kanumba. Nadhani tusubiri zaidi majibu ya hayo maini yaliyochukuliwa, huenda kukawa na sababu nyingine ya ziada iliyosababisha kifo chake
 
Kanumba alikuwa ni enterpreneur ambaye aliajiri/ alikuwa na mpango wa kuajiri Watanzania wengi sana siku za usoni, hivyo kumsaidia JK katika motto yake!
Kwa hiyo hii ndio sababu ya serikali kutia nguvu zake katika mazishi yake??
 
R.I.P ndugu yetu mpendwa kanumba. limetokea kwa njia hiyo na ni ngumu kuamini ila lolote lifanywalo baada ya kifo chake halitarudisha roho yake chuki na hisia mbaya kwa huyu mtoto sio njia halisi ya kuomboleza msiba
 
Back
Top Bottom