Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Kifo cha Steven Kanumba na hatma ya Elizabeth Michael (Lulu)

Mwanga wa milele umpe ee bwana, mtumishi wako Kanumba apumzike kwa amani.
 
Ni masikitiko makubwa kwetu Watanzania kumpoteza balozi wetu kwenye tasnia ya Filamu. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akupumzishe kwa amani huko peponi, malaika wake wakulinde na Ibilisi ili siku ya mwisho tuweze kuonana tena juu mbinguni Mpendwa wetu Steve.
Kwa wenzetu walioweza kufika kutoa rambirambi zao kwenye familia hapo nyumbani kwa Marehemu wamewakilisha sisi ambao hatukuweza kupata fursa ya kufika hapo msibani, lakini nafsi zetu zinaungana nao kwenye kipindi hiki kigumu. Niipongeze pia Kamati ya Mazishi iliyowezesha ushawishi kwa familia kuzika mwili hapa DSM.
Niipongeze tena Serikali yetu tukufu ya awamu ya nne kwa ushiriki wake kwenye msiba huo na kubeba jukumu zima la mazishi ya shujaa wetu na mpendwa wetu kwa kweli ni ishara tosha kuwa Serikali yetu inajali sana shughuli za michezo.
Lakini pia uwepo wa makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa juu Serikalini kwenye mazishi yatakayofanyika leo ni kielelezo kingine cha kuonyesha kujali na kushirikiana na wananchi kwenye Matatizo makubwa kama haya.
Mwisho limenijia swali GUMU sana ambalo nimeshindwa kupata jawabu lake nikaona niliunganishe hapa leo, hawa viongozi wetu wa kitaifa wameshiriki kwenye misiba yote mikubwa kuanzia ya Wabunge wetu wanaopoteza maisha.
Alivyofariki Gavana wa Benki kuu Mzee Balali ni kwa nini Serikali ilishindwa kuhudhuria mazishi yake au alikuwa na makosa ambayo hata Balozi wetu aliyeko Marekani kushindwa kumuwakilisha Raisi wetu? Kwa mwenye kuwa na upeo zaidi yangu anaweza kunisaidia.
Mwisho nawatakia wote mtakaoweza kwenda kushiriki mazishi, mtatuwakilisha nasi tupo pamoja.
BURIANI THE GREAT STEVEN KANUMBA
 
kwani wote wanaozikwa na makanisa yao unjua wamekufaje? au kwa sababu hujui?
 
Mitindo ya maisha ndiyo inayowauwa Wasanii maarufu. Kumbuka the Jackal, Whitney, Tupac, Notorious BIG na wengineo wataongezeka.
TUJIHADHARI.
M4C
 
Wana Jf,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ambayo niseme kabisa ni ya hovyo kabisa kuhusu matokeo ya uchunguzi wa madaktari baada ya kuufanyia mwili wa marehemu uchunguzi.

Ujinga huo nimeusikia kupitia power bfast ya clouds leo. Haiingii akilini kwa watu walioaminiwa kusema ukweli wakaishia kupokea maelekezo kutoka kwa wenye 'mali zao' na hatimaye kupindisha matokeo na kuishia kutoa maujinga yao kama ripoti ya kitaalam. Kanumba alikuwa katika tifu zito baada ya kubaini kicheche wake anajadili miadi mingine. Ili kukwepa simu yake isikwapuliwe na Kanumba, na hakika kulinda namba ya bwana ake, Lulu alifanya kila aliloweza hii ikiwa ni pamoja na kusukumana na kutwangana na vitu vizito. Huu ndio ukweli na sio ujinga walioutangaza.

Jeshi la polisi nalo liwe na uzalendo, wamezoea sana kuficha ukweli hasa wakijua kuna mkubwa anahusika. Nadhani wote mnakumbuka mauaji ya mwandishi wa dira huko Mwanza na maripoti ya hovyohovyo ya polisi.

Lulu ndio chanzo cha kifo cha Kanumba hata kama madaktari watang'ang'ana na ujinga wao wa mtikisiko wa akili. Upuuzi mtupu hapa. Na clouda nao ndio wakaileeemba utadhani hata wanajua undani wa kifo hicho, hawa nao... Mbona hamkusema kuhusu simu aliyopigiwa Lulu kabla ya ugomvi wao? Sasa taarifa zilizozagaa ni kuwa alipigiwa simu na waziri wa JK ndio maana wanajaribu kuua soo kwa kudai eti unaweza kukumbwa na mtikisiko wa ubongo halafu ukaanguka chini na kufa. Kawadanganyeni watoto wenu mataahira.

Mwisho ndugu zangu tuache ubaguzi. Kifo ni kifo hata ufie ikulu ni kifo tu. Tuwe na uzalendo.

Ni mimi,
Pangu Pakavu.
 
na kwa bahati mbaya kama Lulu ndo alimsukuma Kanumba akakosa balance na kuanguka na kufa je kifo cha kanumba kitakuwa kimesababishwa na nani?
 
Siku nyingine tafadhari tuache kuwa tunazusha kwa mfano hii ishu ya mgogoro wa ndani wa baba na mwana umekuzwa pasipo maana yoyote ya msingi jambo ambalo kifamilia siyo zuri hata kidogo

Mungu akulaze Kanumba mahala pepma peponi,Amen!
 
kasafishwaje wakati haijasemwa huo mtikisiko kwa Kanumba umesababishwa na nini? Kuna mambo hayajawekwa wazi bado nadhani yaliyobaki ni ya kipolisi zaidi kwa upelelezi..
jukumu la kujua mtikisiko umetokana na nini ni kazi ya polisi.
 
Samahani kwa kuchanganya habari ya Mzee Jangala, naomba Mods wa-edit heading.....
 
kaeso mzee jangala unamuuwa wewe
kwa kupost bila uhakika
samahani yako imekubaliwa
unaweza kuedit post yako
 
Watanzania ha2endelei sabab ya UVIVU yaan badala ya wa2 kufanya kaz wanajipanga kushangaa msafara wa msanii
 
Kwani ubongo unaweza kutikisika bila kutikiswa na mtu? Haya maelezo bado yanahitaji ufafanuzi zaidi wa kitaalamu.
Ubongo unatikiswaje?
 
kaeso mzee jangala unamuuwa wewe
kwa kupost bila uhakika
samahani yako imekubaliwa
unaweza kuedit post yako
Nilikuwa sijamsikia muda mrefu ndio maana nikachanganya habari, lakini nimeshindwa ku-edit heading.....
 
Hapa kuna kesi inayomkabili Lulu either ya kuua kwa kukusudia au kuua kwa kutokukusudia, mpaka uchunguzi ukamilike
 
Back
Top Bottom