Kifo cha Ulomi: Taarifa ya Polisi imezua maswali magumu na mabaya. Haya hapa baadhi...

Screenshot_20241216-193620.png
 
Kwa kuwa matukio ya mauwaji na kuppotezwa kwa watu yamekuwa mengi basi ni lazima watu wapate mashaka kwa kila familia inaposema mtu wao hajulikani alipo

Inawezekana huyu jamaa alipata ajali kweli na kupelekwa hospital na hatimae kufariki
Kuhusu vitu vyake kama simu na hata wallet tunajua watu wengi huwa hawajali mtu aliepata ajali na jambo la kwanza ni kumsachi ana nini hili tunaona kwenye ajali nyingi

Maiti zinavuliwa saa na hata kuvuliwa viatu
Jamani kuna watu zaidi ya wanyama
Ila sio vizuri pia kukurupuka na kuamua akili inakuambia nini bali ni lazima kusubiri ukweli kwanza
Lazima kuna watu walioshuhudia ajali na hata waliompokea hospital kama Dr na manesi pia wote wana la kusema

Tumuombe Mungu sana kwa haya yanayoendelea na pia tuwe na uhakika wa mambo
 
Je hakuwa na vitambulisho?
Je hakuwa na simu mfukoni? Namba ya simu iliyo mfukoni ilikuwa na line iliyosajiliwa kwa jina lipi?
Je namba ya pikipiki aliyokuwa anaiendesha ilikuwa imesajiliwa kwa jina lipi?

Hiyo ajari ilimuhusisha nani mwingine? Mpaka wasamalia wema wamuokote!

We have lost trust....and in deed this is one of the things we don't have any trust.
 
Naomba nianze na taarifa yenyewe.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa Daisle Simion Ulomi, aliyekuwa ameripotiwa kwamba amepotea, alifariki dunia baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia siku ya Desemba 11, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 16, 2024 na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro ambapo ameeleza kuwa tarehe 11 Desemba, 2024 Jeshi hilo lilipata taarifa ya kupotea kwake na ndugu hawakuwa wanampata kwenye mawasiliano ya simu, baada ya yeye kuondoka ofisini kwake Sinza na kudai anaelekea Temeke kufuatilia makontena yake ya biashara.

"Ulomi aliondoka eneo lake huku akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe, ufuatiliaji umefanyika kwa kushirikiana na ndugu na kubainika kuwa Ulomi alipelekwa kituo cha afya cha Makuburi Ubungo External mchana wa tarehe 11 Desemba, 2024 baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia, wasamaria wema walimsadia kumpeleka kwenye kituo hicho akiwa hajitambui na hakuwa na kitambulisho chochote," imeeleza taarifa ya Kamanda Muliro.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, " Baadae alipelekwa Mwananyamala hospitali na ikabainika tayari alikuwa amefariki na maiti yake kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo kama mtu asiyefahamika akisubiri kutambuliwa na ndugu, ndugu tayari wameutambua mwili huo ukiwa na majeraha maeneo mbalimbali ya mwili. Aidha, Pikipiki aliyopata nayo ajali pia imepatikana ikiwa imeharibika. uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na taarifa zaidi itatolewa,".

#EastAfricaRadio

Maswali
Kwahio Afisa wa TRA ni kweli alipiga simu? Ni kweli kulikua na mawasiliano kati yake na Afisa wa TRA? Mbona baada ya "Afisa wa TRA" kumkosa (maana hakufika alikoitwa) hakuchukua hatua Yoyote ya kumpata "mteja" wake? Iko wapi simu ya Ulomi? Nani hasa alimpigia Ulomi kwenda bandari kavu? Mawasiliano ya mwisho ilikua chang'ombe, hapo jirani kuna hospital ya Temeke, why apelekwe Makuburi External?

Kwa maswali haya, Polisi wanakua Kwenye nafasi nzuri ya kujibu, wapi Ajali ilitokea, namna Ajali ilivyotokea (kugongwa au kugonga au kuanguka mwenyewe), huyu msamaria mwema ni nani hasa? Alitumia usafiri gani kumfikisha "Makuburi health Centre?"! Kutoka Makuburi (Ubungo) Hadi Mwananyamala kuna hospital kadhaa, mojawapo ikiwa ni Sinza Palestine, ambayo ina uwezo pia WA kupokea maiti, why wafunge safari ndefu Hadi Mwananyamala?

PIA SOMA
- TANZIA - Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

Kama Polisi ndio walioupeleka mwili Huko, mbona hawakutoa taarifa kwa umma, na mitandao yote iliandika kuhusu kupotea kwa Ulomi? YAANI Polisi walikaa na taarifa Hii Hadi "alipopatikana" kwenye mafriji ya Mwananyamala.

Kama Polisi Wanakiri kuwa Ulomi hakua na Kitambulisho, LAKINI si alikua na Bodaboda "iliyopata Ajali"? Walishindwaje kuangalia usajili WA Bodaboda Kwenye mfumo wa TRA na kumtambua mmiliki? Ina maana angezikwa na Manispaa kwa kua hakua na Kitambulisho?

Kwangu Mimi hii taarifa imenipa mashaka Sana kuliko majibu.

View attachment 3178202
Jeshi la polisi limejiweka katika hali ya kutoaminika tena. Inahitaji kujitoa ufahamu ili uwaamini polisiccm.
 
One day what happen to Assad will occur here. They can do it for so long. They need to understand that a day without a name will come for all the injustices to come to light. I fear for my country because on that day no amount of power will stop the masses.
MENE MENE TEKEL!
Mimi huwa naamgalia haya yanayotokea sasa nakuyafananisha kama ya afrika kusini wakati wa ubaguzi.. ukienda afrika kusini ya leo pale hata raisi anapaogopa maana nipamoto kwenye upande wa sheria inaungunza pande zote, hakuna aliyejuu ya sheria. Watoto wadogo wa kizazi chaleo wajua sheria zao nakuzitekeleza.

Unadhani ilichukua muda gani kutoka uchaguzi mpaka wakayaanza kuishi hayo maisha ya hivi leo? Watu wangapi walipotea na kufariki kipindi hicho
 
Naomba nianze na taarifa yenyewe.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa Daisle Simion Ulomi, aliyekuwa ameripotiwa kwamba amepotea, alifariki dunia baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia siku ya Desemba 11, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 16, 2024 na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo SACP Jumanne Muliro ambapo ameeleza kuwa tarehe 11 Desemba, 2024 Jeshi hilo lilipata taarifa ya kupotea kwake na ndugu hawakuwa wanampata kwenye mawasiliano ya simu, baada ya yeye kuondoka ofisini kwake Sinza na kudai anaelekea Temeke kufuatilia makontena yake ya biashara.

"Ulomi aliondoka eneo lake huku akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe, ufuatiliaji umefanyika kwa kushirikiana na ndugu na kubainika kuwa Ulomi alipelekwa kituo cha afya cha Makuburi Ubungo External mchana wa tarehe 11 Desemba, 2024 baada ya kupata ajali mbaya na pikipiki aliyokuwa akiitumia, wasamaria wema walimsadia kumpeleka kwenye kituo hicho akiwa hajitambui na hakuwa na kitambulisho chochote," imeeleza taarifa ya Kamanda Muliro.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, " Baadae alipelekwa Mwananyamala hospitali na ikabainika tayari alikuwa amefariki na maiti yake kuhifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo kama mtu asiyefahamika akisubiri kutambuliwa na ndugu, ndugu tayari wameutambua mwili huo ukiwa na majeraha maeneo mbalimbali ya mwili. Aidha, Pikipiki aliyopata nayo ajali pia imepatikana ikiwa imeharibika. uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na taarifa zaidi itatolewa,".

#EastAfricaRadio

Maswali
Kwahio Afisa wa TRA ni kweli alipiga simu? Ni kweli kulikua na mawasiliano kati yake na Afisa wa TRA? Mbona baada ya "Afisa wa TRA" kumkosa (maana hakufika alikoitwa) hakuchukua hatua Yoyote ya kumpata "mteja" wake? Iko wapi simu ya Ulomi? Nani hasa alimpigia Ulomi kwenda bandari kavu? Mawasiliano ya mwisho ilikua chang'ombe, hapo jirani kuna hospital ya Temeke, why apelekwe Makuburi External?

Kwa maswali haya, Polisi wanakua Kwenye nafasi nzuri ya kujibu, wapi Ajali ilitokea, namna Ajali ilivyotokea (kugongwa au kugonga au kuanguka mwenyewe), huyu msamaria mwema ni nani hasa? Alitumia usafiri gani kumfikisha "Makuburi health Centre?"! Kutoka Makuburi (Ubungo) Hadi Mwananyamala kuna hospital kadhaa, mojawapo ikiwa ni Sinza Palestine, ambayo ina uwezo pia WA kupokea maiti, why wafunge safari ndefu Hadi Mwananyamala?

PIA SOMA
- TANZIA - Mwili wa Ulomi, Mfanyabiashara aliyedaiwa kupotea wakutwa mochwari Mwananyamala

Kama Polisi ndio walioupeleka mwili Huko, mbona hawakutoa taarifa kwa umma, na mitandao yote iliandika kuhusu kupotea kwa Ulomi? YAANI Polisi walikaa na taarifa Hii Hadi "alipopatikana" kwenye mafriji ya Mwananyamala.

Kama Polisi Wanakiri kuwa Ulomi hakua na Kitambulisho, LAKINI si alikua na Bodaboda "iliyopata Ajali"? Walishindwaje kuangalia usajili WA Bodaboda Kwenye mfumo wa TRA na kumtambua mmiliki? Ina maana angezikwa na Manispaa kwa kua hakua na Kitambulisho?

Kwangu Mimi hii taarifa imenipa mashaka Sana kuliko majibu.

View attachment 3178202
Kuna kitu nili taka kuandika vidole vika kataa
Ndio maana una kuta mtu amewahi kuwa RPC akistaafu ana kwenda kuwa mlinzi kwa kampuni za watu.. Malaaana
 
Maswali ya kufikirisha:-
1. Maswala ya forodha hufanywa na clearing agent, kwanini Ulomi apigiwe simu Moja kwa moja na asipigiwe clearing agent wake kwenda kukagua container? Polisi na TRA Tanzania watupe ukweli
Hasa ukizingatia ni majuzi tu hapo maafisa wa TRA walitaka kumkamata mtu usiku usiku na kusababisha maafa. Maswali ni mengi sana.

Katika zama hizi mtu kupata ajali mjini na kusaidiwa na wanaoitwa wasamaria wema tangu tarehe 11 picha yake inatembea mitandaoni na asitokee mmoja kati ya wasamaria wema au wahudumu wa hospitali kusema lolote, au labda alipasuka kichwa na kuharibika kabisa?

Back
Top Bottom