Kwa sababu hiyo BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Tazama, nitawaadhibu watu hawa; vijana watakufa kwa upanga; wana wao na binti zao watakufa kwa njaa’ (Yeremia 11:22. Manenomepesi kukazia).
BWANA wa majeshi asema hivi, ‘Tazama, nitaleta juu yao upanga, na njaa, na tauni, nami nitawafanya kuwa kama tini mbovu zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu’ (Yeremia 29:17).
Mwanadamu! Nchi itakapofanya dhambi na kuniasi kwa kukosa, nikaunyosha mkono wangu juu yake na kulivunja tegemeo la chakula chake, na kuipelekea njaa, na kukatilia mbali mwanadamu na mnyama … (Ezekieli 14:13. Maneno mepesi kukazia).
Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake. Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake. Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono (Hagai 1:9-11. Maneno mepesi kukazia).