Jambo lolote kabla halijafanyika/halitatimia/tokea katika ulimwengu wa MWILI huanza kwanza kutokea/kutimia/kufanyika katika ulimwengu wa ROHO.Yani mfano mwangwi wa sauti husikika baada ya sauti kwanza kusikika ndio baadae unafuatia mwangwi.
Muda hutofautiana toka jambo lilipotokea katika ulimwengu wa Roho mpaka kuja kutokea katika ulimwengu wa Mwili(inaweza kuwa siku,majuma kadhaa n.k)
Njia moja wapo ya mwanadamu kupata taarifa ya yale yanayotokea katika ulimwengu wa Roho ni kupitia ndoto mtu anazoota.Ndoto zote binadamu anazoota ni matukio halisi yanayotokea katika ulimwengu wa Roho ,tafuta sana kujua maana ya ndoto zote unazoota,usipuuze ndoto yoyote.Ndoto zote zina maana .Ya mambo yatakayokutokea ,au yaliyokwishatokea.TAARIFA hizi unazozipata kwenye ndoto ukizifanyia kazi kwa kuombewa na watumishi wa Mungu unaweza kubatilisha ku reverse madhara waliyokusudia uyapate adui zako hasa ufalme wa giza(wachawi,mizimu,waganga wa kienyeji,roho za mauti ,mapepo,majini)
njia nyingine taarifa zinaweza za kitu kibaya au hatari,ni kwa roho au nafsi yako kujisikia vibaya ,huzuni,kukosa amani,kuchukia au kukataa,au kusikia kabisa sauti inakusemesha ndani yako juu ya hatari fulani,au inakukataza jambo fulani la hatari,au inakutahadharisha .
DAWA SULUHISHO
Ukisikia dalili hizo au ukiota ndoto hizo,ni kusali kuomba rehema,neema kwa YESU kristo ndiye pekee anayeweza kukuokoa hata katikati ya mateso,hasa kama mateso yanasababishwa na ufalme wa giza na si mapenzi ya Mungu yakupate hayo.YESU anaweza kukuokoa kutoka nguvu za giza.