Kifuatacho baada ya Job Ndugai kujiuzulu, tukae mkao wa kula

Kwahiyo ndugu unataka kuniambia kuwa spika akiwa nje ya Bunge na kuongea hoja za msingi Kwa taifa hiyo inakuwa sio hoja Kwa sababu hajaisemea bungeni......na je Raisi yeye ni wapi akisemea kauli yake inakuwa ni official i.e. ni ikulu pekee au??
 
So, hoja ni ipi kuomba msamaha au amevunja protocol za kiongozi kukosoa mhimili mwingine??
Kuhoji muhimili mwingine sio ishu kabisa na infact ndio kazi yake. Alitimiza wajibu wake kwa asilimia mia tatu! Shida ni 'ujinga' aliokuwa nao ambao kimsingi alifundishwa na Marehemu kuwa yeye anawajibika kwa Rais na ni mtumwa wa Rais. Pumbaf kabisa sasa kawajibishwa kweli.
 
Ajabu ni kwamba hoja yake aliielekeza zaidi kwa rais Samia hadi anataja mambo ya 2025, sijui kwanini aliamua kufika mbali kiasi hicho.

Kama kweli alikuwa na uchungu wa deni lote la 70T basi angeunga mkono hoja ya Nape.
 
Kwahiyo ndugu unataka kuniambia kuwa spika akiwa nje ya Bunge na kuongea hoja za msingi Kwa taifa hiyo inakuwa sio hoja Kwa sababu hajaisemea bungeni......na je Raisi yeye ni wapi akisemea kauli yake inakuwa ni official i.e. ni ikulu pekee au??
Kwamba hujaelewa nilichoandika? Anyway nimesema kitu kinaitwa "functus officio" pia nikaongelea Uhuru wa kutoa maoni nje ya bunge una mipaka kulingana na kiapo Cha kazi yake.

Speaker anajadili mada za serikali bungeni, anatoka chama tawala anapitisha mipango ya chama chao, kwa namna yeyote hapaswi kumkosoa Rais ambaye ni boss wake na Mwenyekiti wake nje ya bunge au nje ya vikao vya chama.

Unamuona IGP au General wa Jeshi na Mkurugenzi wa usalama wa Taifa, wanaweza kuwa na maoni yao na Wana haki ya kutoa maoni Ila kulingana na kiapo Cha kazi yao na nature ya kazi yao Wana channel za kumshauri Rais Ila sio kuitisha press na kuongea hovyo.

Speaker ana nafasi ya kujadili hoja za serikali ya chama chake bungeni, hutegemei aende kinyumr na Sera ya chama chake kwa namna yeyote Ile lazima ajiondoe au afukuzwe so angetumia busara kujiondoa.
 
Yeye kalazimishwa kusaini tu barua, barua ya spika haiwezi kuoksa address, haiwezi kuwa na maandishi makubwa tu. Pia Taratibu za kujihudhuru hazijafuatwa. Kikubwa Mhimili mmoja umepoka madaraka kwa lazima na hapo ndiyo tutamshukuru Dkt Magufuli kwa uwazi wa kutuletea maendeleo ila ya huyu Mama ni mabaya zaidi kwa sababu huwezi kutumia state machinery kulazimisha mhimili mwingine uachie ngazi. Kitakachofuata Mama ajue that state machinery iko siku itamsumbua yeye huyo huyo tena kwa fedheha kubwa sana. Nina uhakika najua wao kazi yao ni kutekeleza kumfurahisha rais lakini haya mambo huwa yanageuka kama alivyokuwa anfanya Ndugai juu kuhoji wabunge.
 
Kuondoka kwa ndugai kumenifanya nione mapungufu mengi sana kimfumo

1 . Hii nchi ina mhimili moja tu hizi zingine geresha
2. Hoja za mashiko hazipewi nafasi
3. Tunako elekea wimbo wa katiba mpya tutaimba wote ...muda ni mwalimu mzuri
Haya mambo ndo yanayotakiwa,
Hawa vigogo wakipata cha Moto akili ndo zinakaa sawa.
Hatimaye tutazungumza lugha moja kama Taifa.
 
Umeeleza nikakuelewa vizuri Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…