Kifuatacho baada ya Job Ndugai kujiuzulu, tukae mkao wa kula

Hiyo mihimili mingne ni kiini macho.ni mihimili yakwenye makaratasi.ndomaana namimi naunga mkono nchi kua na katiba inayijielewa.Katiba ikiyopo inamapungufu menhi ambayo hayaendani na nyakati.
Kabisaa chifu na huo ndo ukweli
 
Nadhan unajidanganya ww mwenyew,tegemeo lao kubwa lipo ktk ile katiba chakavu fullstop
 
Swali je akiingia speaker mwingine naye pia akaonekana kuihoji serikali, je kutatokea kuombwa kungatuka madarakani
Umekwenda mbali...je atakuwa na uthubutu hata wa kuihoji serikali? Sasa washafumbwa midomo.
 
Reactions: Ame
Hilo swala la Katiba mpya, wengi wa wana CCM wamekua wakiliona kama wao haliwahusu kwa sababu wanaona linawatibulia mpango wao wa kuongoza milele. Hiki kilichotokea ni mpango wa Mungu kulipeleka Taifa kwenye kuipata Katiba Mpya. Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama na tofauti zingine, tulione swala la Katiba Mpya ni la lazima. Katiba iliyopo ya 1977 ilikua ni ya chama kimoja cha CCM, haiwezi kukidhi matakwa ya sasa. Tupate Katiba Mpya na Bora kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
 
Hapa ume underline the fact kuwa hii mihimili haipo sawa wala huru na unathibitisha assertion kuwa katiba hii haikidhi haja...Kwani Head of State yeye anatakiwa kuja public kuubagaza muhimili ulio huru?

Simkubali Ndugai kwa tabia zake za huko nyuma lakini kwa hili no it was not right! Nani atasimama tena kuuhoji muhimili wa executive?
 
Kuondoka kwa ndugai kumenifanya nione mapungufu mengi sana kimfumo

1 . Hii nchi ina mhimili moja tu hizi zingine geresha
2. Hoja za mashiko hazipewi nafasi
3. Tunako elekea wimbo wa katiba mpya tutaimba wote ...muda ni mwalimu mzuri
Hiyo No 3 ilifaa iwe hoja ya Kitaifa muda mrefu, lakini kuna watu wamekua wakiona kama inakisumbua chama chao kisiimiliki nchi hii milele. Wanadanganywa na wanasiasa (kina Ndugai) ambao wako High Table wanakula na kusaza, huku wao hawajui mlo wa siku ya pili, wakiwa wamevalishwa mashati ya kijani.
 
Umekwenda mbali...je atakuwa na uthubutu hata wa kuihoji serikali? Sasa washafumbwa midomo.
Watu hawajui tatizo lililopo...Je kwa bahati mbaya kukitokea state capture nani ataleta balance of power? Judge Mkuu naye atathubutuje kuhukumu iwapo na yeye ni mteuliwa?

What happened is bad kwa nchi yetu kila mwenye sense of integrity hawezi kubali hili kwa hiari au kwa shari....naamini katiba mpya itakayoleta mazuio ya individuals kutumia institution power zao kuvuruga mihimili ambayo inatakiwa iwe independent and complementing each other ili kuleta unity, peace and harmony ndani ya nchi, ndiyo suluhisho ya haya mambo kutotokea tena; hakuna ziada wala pungufu...Hao wenye mihimili wame cross red line kwa usalama wa nchi yetu na tukiwa fair ni personalities zao ndiyo zimekuwa tatizo kubwa kwakua wameshindwa kujizuia kuvuruga mihimili.
 
Hahah!muwe hata mnashare Wi-fi pale bando linapokata
Hawa ndiyo wale ukiwaambia kuna umuhimu wa kupata Katiba Mpya hawawezi kukuelewa, hawaendi na wakati, wanaitaka ile ile ya 1977 ya chama kimoja cha CCM.
 
Wacha Ndugai akinywee hiki kikombe pia. Amehusika kuwanywesha kikombe hicho wengine akishirikiana na JPM. Kumbuka issue ya CAG Prof Musa Assad na suala la kumfuta ubunge Tundu Lissu na kumzuia matibabu na haki zake zingine, kwa kutaja machache. Wakati wake wa kunywa hicho kikombe umefika, wacha aonje machungu waliyoyaonja wengine.
 
Reactions: Ame
Ni sawa but who else anafuata? We need to put this to an end and a very good end not just an end
 
Hili bunge tangu November 2020 baada ya kuwa la chama kimoja, lilishakua la kipiga makofi. Ngoja tuwaachie hilo bunge CCM, chama "kilichoshinda kwa kishindo"

Bunge lilishaufyata muda mrefu tangu kipindi cha JPM. Angalia lilichofanya kwa CAG Prof Assad alipohoji 1.5tri.
 
Ndugai nje ya kile "kiti na lile joho" hana madhara yoyote
Hajulikani
hakubaliki
Hana mvuto kwa jamii
 
Hapa ndipo ilipo point ya kujiuzulu.
 
inasemekana ile Barua ilichapwa na Vibaraka wa Mama wakaipeleka hadi Nyumbani kwa Spika wakamwambia aweke Signature yake au wamshughulikie,na Ndiyo maana barua yake inaonekana kuwa na dosari kadhaa, Tuendelee kunywa mtori
 
Mkao wa Kula au Kuliwa ?

Officially Bunge ni Rubber Stamp na hata kama ukibadilisha Katiba na Kumpa Nguvu bado atatoka kwenye hiki Chama chenye Monopoly na Kinachoendelea ndani kwao ni dhahiri tutaendelea kuliwa..., Pia uelewa na ushabiki wa Mwananchi kutokuona kwamba kuna Hitilafu ni kwamba we have a long way to go.....
 
Tatizo ni KATIBA. Tupate katiba mpya tuyarekebishe hayo.
 
Kwahiyo ndugu unataka kuniambia kuwa spika akiwa nje ya Bunge na kuongea hoja za msingi Kwa taifa hiyo inakuwa sio hoja Kwa sababu hajaisemea bungeni......na je Raisi yeye ni wapi akisemea kauli yake inakuwa ni official i.e. ni ikulu pekee au??
Spika wa bunge ni mwananchi, lakini yeye ana maamuzi.
Spika ni sehemu ya maamuzi ya serikali na ndani chama chake.
Kwa wadhfa wake wa Uspika, anakuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama.
Bunge ni sehemu ya maamuzi ya mambo mbalimbali ya serikali.
Mkopo ulipitia bungeni, ukajadiliwa na kamati za bunge, ukaidhinishwa.
Unatoka nje ya bunge unalalamika!?
Unamlalamikia nani?
Alikuwa na uwezo wa kuukwamisha huko huko bungeni, lakini ameuidhisha, kisha unakuja kullalamika, huoni kama hakulitendea haki bunge kama kiongozi wake!!?
Hata baada ya maamuzi, kwa cheo chake anaweza kuomba kukutana na rais ili wajadiliane kuhusu mikopo na namna nzuri ya kukopa, kuipunguza au kuachana nayo.

Lakini kusimama hadharani kuiponda serikali ya chama chako na ukiwa mjumbe wa vikao vyake ni usaliti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…