Tetesi: Kifuatacho: Mtafaruku wa CHADEMA na TeamLowassa kuinufaisha ACT Wazalendo, Kafulila kumfuata Zitto

dah! siasa bhana yataka moyo maana chadema kazi mnayo awamu hii naona nondo zinatupwa kutoka upande wa pili duh!
 
Sugu anahamia chama gani?
Prof nae atakimbilia wapi?
Mbona nawaona wabunge wengi sana ambao hawajatoka Kilimanjaro na Arusha na hawana dalili ya kukihama chama hicho?
By the way,who is Zitto? Maana naona kila rejea yako ni Zitoo, na huyo Zitto alikuwa CDM mkamnunua na akajiita ni mwana mageuzi wa kweli...hata siku moja usimwamini mtu anayejiita mwanamageuzi na huku anashinda akibuni mbinu za kumaliza mageuzi....
Asante kwa post yako.
 
Tanzania vyama vya siasa viko vingi, wanasiasa waliohama vyama nao wako wengi! Katika vyama hivyo vingi, kuna vyama vichanga na dhaifu na vingine vya umri zaidi ya miaka ishirini lakini vimedumaa na pia kuna vyama ambavyo vinaendelea kumea na kustawi katikati ya "magugu", chama cha magugu (CCM). Vivyo hivyo viongozi nao wapo waliohama toka chama cha magugu na kuingia upinzani na pia toka upinzani kwenda chama cha magugu, kati yao wapo wenye nguvu na ushawishi mkubwa na pia wapo dhaifu. Hili ni jambo la kawaida sana kisiasa. Mimi nawashangaa baadhi ya watu humu kila kukicha ni kuisema Chadema tu na au Lowasa au Mbowe. Binafsi sivutiwi kabisa na uandishi wa aina hii. Sote tunajuwa Chadema na washirika wake wanaounda UKAWA nyuma yao kuna Watanzania millioni 6 waliokipigia kura kwenye uchaguzi mkuu. Idadi hii sio ya kukejeli hata kidogo. Kwa mantiki hiyo, huwezi ukalinganisha Chadema na na chama kingine dhaifu kilichopata kura chini ya laki tano halafu unakisifia chama dhaifu ! itakuwa ni wendawazimu kufanya hivyo! Kuendelea kuviponda vyama vinavyojiimarisha na kukua huku kuvisifu vyama dhaifu ni kuvidumaza vyama hivyo dhaifu.
 
Wenye akili tumekuelewa, lakini Mazuzu CHADEMA yatakupinga. Na hawaoni dalili wao ni kuongea tu bila kufikiri. Hilo nasisitiza litatokea tu. Maana Chadema sasa wamekwisha no way to go.
 
Wenye akili tumekuelewa, lakini Mazuzu CHADEMA yatakupinga. Na hawaoni dalili wao ni kuongea tu bila kufikiri. Hilo nasisitiza litatokea tu. Maana Chadema sasa wamekwisha no way to go.
Kuishabikia ccm Inatakiwa Ujipunguze Akili Kama Sivyo Hauwezi Kua Mwanachama wa ccm

Tanzania ni Nchi ya Viwanda Hapa Kazi Tu.!
Kiongozi Atakae Sema Mkoa wake una Njaa Ajiandae Kuacha Kazi.

Tanzania Imepanga Kutoa Mahindi ya Chakula tani Million 1.5

Watakaovaa Ma T-shirt Yaliyoandikwa Njaa Kukamatwa.
 
Jielekeze kwenye hoja...mwambie alipe kodi
 
Jikite kwenye hoja.
 
Kuna wizi mpya wa pesa za umma,Wajanja baada ya kugundua mkulu hapendi Wapinzani wameamua kubuni miladi mikubwa ya kula pesa za Umma kama Lipumba anavyozitafuna kiulaini.
Jikite kwenye hoja
 
Endelea kupiga ramli sie tunasonga mbele... lkn maisha yamekuwa magumu sana kwa wenzetu wa ccm, lazima mjitoe ufahamu ili mkono uende kinywani
Kweli mkuu hali mbaya Lumumba hata kazi ya kusafisha vyoo haipatikani
 
Mbowe na Lowassa ni wasanii tu,wanawageuza wafuasi kama chapati za maji.hakuna watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri kama wafuasi wa chadema
 
Ndiyo maana hatupati mvua. Ni kwa sababu ya kuongezeka watu wenye mawazo ya hovyo hovyo kama huyu. Mungu hapendi haya mambo.
 
Hawa Chadema walishaambiwa toka mapema kumkaribisha Lowassa ndani ya chama ndio mwanzo wa anguko lao, nasikia hali ni mbaya ndani ya chama, hata vile viposho vya sh 50000/= vimeyeyuka, Tundu Lissu analia njaa ndio maaana anaimbuka na hoja zisizo na msingi kujaribu kutoka, lakini kila anapojaribu anakwama, dawa ni moja tu kama ni wajasiri wamfukuze LOWASSA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…