Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Jana nilikua kwenye basi kuelekea nyumbani Kwamtogole. Jirani yangu alikaa mwanaume mwenye umri unaokaribia miaka 35. Hajui Kiswahili vizuri. Tuliongea hivyo hivyo na Kiingereza changu cha yes, no lakini nilifanikiwa kumuelewa.
Huyu mwanaume ni raia wa Ghana lakini alifanikiwa kwenda Ulaya. Aliishi Ulaya kwa miaka 15 kabla hajapata kesi iliyomfunga. Kisa cha kesi inawezekekana alinihadithia lakini sikumuelewa.
Aliniambia baada ya kifungo kule jela wiki ya kwanza ni ya kukaribishwa. Unapata chumba mna share wawili na choo chenu. Mna anza ratiba ya kuingia darasani na mwana saikolojia. Kuna maswali mengi unaulizwa na kutokana na majibu ndiyo wanajua unapaswa kujifunza kitu gani.
Mafunzo ni kutoka na muda ya kifungo chako. Ukiamua kujifunza kilimo au catering ni muda wa kifungo na akili yako itakuwezesha kuondoka na certificate, diploma au degree.
Huyu bwana aliamua kuwa mkulima na alipanda vitunguu. Alipata certificate ya City and Guilds. Alifundishwa aina za udongo vitunguu vinaweza kustawi, jinsi ya kusia mbegu, kumwagilia, kuangalia magonjwa na kuweka mbolea. Kisehemu alichopewa hakikua kikubwa sana na alivuna vitunguu magunia mawili. Vilitumika jikoni pale jela lakini alilipwa pesa yake.
Wakati anavuna aliwaza ardhi ya babu zake aliyoiacha kule Ghana. Kama kile kipande kidogo tu kimemletea pesa aliyopata. Baada ya kifungo aliamua kurudi kwao Ghana.
Alipitia Tanzania kwakuwa alikuwa na swahiba alifanya nae kazi kwa miaka 10 kati ya ile 15 aliyoishi Ulaya na swahiba amerudi nyumbani. Aliipenda Dar hivyo alikuwa ana peruzi mji mwenyewe.