Kifungo cha jela kimempa mabadiliko chanya ya maisha

Kifungo cha jela kimempa mabadiliko chanya ya maisha

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Jana nilikua kwenye basi kuelekea nyumbani Kwamtogole. Jirani yangu alikaa mwanaume mwenye umri unaokaribia miaka 35. Hajui Kiswahili vizuri. Tuliongea hivyo hivyo na Kiingereza changu cha yes, no lakini nilifanikiwa kumuelewa.

Huyu mwanaume ni raia wa Ghana lakini alifanikiwa kwenda Ulaya. Aliishi Ulaya kwa miaka 15 kabla hajapata kesi iliyomfunga. Kisa cha kesi inawezekekana alinihadithia lakini sikumuelewa.

Aliniambia baada ya kifungo kule jela wiki ya kwanza ni ya kukaribishwa. Unapata chumba mna share wawili na choo chenu. Mna anza ratiba ya kuingia darasani na mwana saikolojia. Kuna maswali mengi unaulizwa na kutokana na majibu ndiyo wanajua unapaswa kujifunza kitu gani.

Mafunzo ni kutoka na muda ya kifungo chako. Ukiamua kujifunza kilimo au catering ni muda wa kifungo na akili yako itakuwezesha kuondoka na certificate, diploma au degree.

Huyu bwana aliamua kuwa mkulima na alipanda vitunguu. Alipata certificate ya City and Guilds. Alifundishwa aina za udongo vitunguu vinaweza kustawi, jinsi ya kusia mbegu, kumwagilia, kuangalia magonjwa na kuweka mbolea. Kisehemu alichopewa hakikua kikubwa sana na alivuna vitunguu magunia mawili. Vilitumika jikoni pale jela lakini alilipwa pesa yake.

Wakati anavuna aliwaza ardhi ya babu zake aliyoiacha kule Ghana. Kama kile kipande kidogo tu kimemletea pesa aliyopata. Baada ya kifungo aliamua kurudi kwao Ghana.

Alipitia Tanzania kwakuwa alikuwa na swahiba alifanya nae kazi kwa miaka 10 kati ya ile 15 aliyoishi Ulaya na swahiba amerudi nyumbani. Aliipenda Dar hivyo alikuwa ana peruzi mji mwenyewe.
 
Jana nilikua kwenye basi kuelekea nyumbani Kwamtogole. Jirani yangu alikaa mwanaune tmwenye umri unaokaribia miaka 35. Hajui Kiswahili vizuri. Tuliongea hivyo hivyo na Kiingereza changu cha yes, no lakini nilifanikiwa kumuelewa...
Interesating narration, asante dada yangu
 
Jana nilikua kwenye basi kuelekea nyumbani Kwamtogole. Jirani yangu alikaa mwanaune tmwenye umri unaokaribia miaka 35. Hajui Kiswahili vizuri. Tuliongea hivyo hivyo na Kiingereza changu cha yes, no lakini nilifanikiwa kumuelewa...
Aisee..
Nzuri, lakini ni kama simulizi imeishia katikati
 
Stori zako na mada zako nzuri, una mawazo mengi ya kuanzisha mada za mafundisho mengi sana, lakini 'nadhani' kama ungeweza kuboresha namna unavyo malizia mada na stori zako zingekua nzuri zaidi.
 
Stori zako na mada zako nzuri,una mawazo mengi ya kuanzisha mada za mafundisho mengi sana...lakini 'nadhani' kama ungeweza kuboresha namna unavyo malizia mada na stori zako zingekua nzuri zaidi.
Bado yuko naye anamhadithia, akimaliza atatuletea kipande kilichobaki.
 
Sio jela zetu huku za kupelekeana moto, mtazame yule ex-DC pendwa wanavyomfanya…. oops masikini!!!!
Kwanza jela kuwa na watu 800+ Huyo mwana saikolojia atafanya kazi vipi kutambua vipaji walivyo navyo na kuviendeleza.
 
Jana nilikua kwenye basi kuelekea nyumbani Kwamtogole. Jirani yangu alikaa mwanaune tmwenye umri unaokaribia miaka 35. Hajui Kiswahili vizuri. Tuliongea hivyo hivyo na Kiingereza changu cha yes, no lakini nilifanikiwa kumuelewa.

Huyu mwanaume ni raia wa Ghana lakini alifanikiwa kwenda Ulaya. Aliishi Ulaya kwa miaka 15 kabla hajapata kesi iliyomfunga. Kisa cha kesi inawezekekana alinihadithia lakini sikumuelewa.

Aliniambia baada ya kifungo kule jela wiki ya kwanza ni ya kukaribishwa. Unapata chumba mna share wawili na choo chenu. Mna anza ratiba ya kuingia darasani na mwana saikolojia. Kuna maswali mengi unaulizwa na kutokana na majibu ndiyo wanajua unapaswa kujifunza kitu gani.

Mafunzo ni kutoka na muda ya kifungo chako. Ukiamua kujifunza kilimo au catering ni muda wa kifungo na akili yako itakuwezesha kuondoka na certificate, diploma au degree.

Huyu bwana aliamua kuwa mkulima na alipanda vitunguu. Alipata certificate ya City and Guilds. Alifundishwa aina za udongo vitunguu vinaweza kustawi, jinsi ya kusia mbegu, kumwagilia, kuangalia magonjwa na kuweka mbolea. Kisehemu alichopewa hakikua kikubwa sana na alivuna vitunguu magunia mawili. Vilitumika jikoni pale jela lakini alilipwa pesa yake.

Wakati anavuna aliwaza ardhi ya babu zake aliyoiacha kule Ghana. Kama kile kipande kidogo tu kimemletea pesa aliyopata. Baada ya kifungo aliamua kurudi kwao Ghana.

Alipitia Tanzania kwakua alikua na swahiba alifanya nae kazi kwa miaka 10 kati ya ile 15 aliyoishi Ulaya na swahiba amerudi nyumbani. Aliipenda Dar hivyo alikua ana peruzi mji mwenyewe.
Vipi hakukumwagia "sera"?
 
Madame Sky Eclat mada zako zako ni nzuri zinamafunzo fulani hivi japo zinaishia njiani na nyingi zikiwa ni kamba lakini tunajifunza mazuri.
 
Back
Top Bottom