Kigamboni: Watuhumiwa kutandaza mabomba na kuiba mafuta yanayoenda bandarini

Kigamboni: Watuhumiwa kutandaza mabomba na kuiba mafuta yanayoenda bandarini

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama wamebaini nyumba iliyopo mtaa wa Ugindoni iliyotandazwa mashine zinazotumika kuchimba visima vya maji lakini badala ya kuchimba chini kuelekea maji yalipo, wanachimba kuelekea usawa yalipo mabomba ya mafuta yanayotoka baharini kuelekea bandarini.

Mafuta hayo yanachukuliwa baada ya 'flow meter' kusoma na kutambulika yamepokelewa nchini lakini kabla ya kufika kituo cha mwisho ndipo mabomba hayo yanapoelekea.

Ndani ya nyumba hiyo kuna mashine na mipira ambayo inavuta mafuta na kujazwa. Nyumba hiyo ina ulinzi mkubwa na taarifa za awali zinasema muhusika amepangisha eneo hilo lenye kodi ya milioni 60 kwa mwaka huku akiwa amelipa miaka miwili na hakuna shughuli inayoendelea zaidi ya kisima ambacho mabomba yake yanaelekea baharini.

=========

Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana
 
Yaaaan mwendazake aliwa fool wapumbavu na wajinga kwamba hakuna upigaji kumbe....kunaaa jamaa angu ni hawa wakula vitu aka unga..nmewahi kumuuliza mtapata wapi hiyooo ktu ..jamaaa alijibu hakunaaa kipindi unga unaingia kwa wingi kama zama hizi za mwendazake..
Huo ni ujambazi siyo wizi wa serikalini. Huyu siku zake zilikuwa zinahesabiwa tu, angekamatwa. El-Chapo alikamwata itakuwa huyu
 
Duh... Nchi hii!!! Mafuta yana faida sana! Manake gharama iliyo tumika kukamilisha huo wizi sio ndogo! Wangeweza kupata kifaa chao chenye security footage, nadhani ingekuwa bora zaidi.

Pili, kama wametoboa baada ya flow meter, ina maana kuna wahusika wa ndani ya bandari. Kwahiyo nao wachunguzwe!

List ni ndefu!

Sent from my S20 Ultra using JamiiForums mobile app
 
Sio rahisi upigaji kama huo kusiwe na mkono wa vigogo serikalini.

Halafu wale teeth wa kipindi Cha mwenda zake walikuwa wapi? Maana tunaambiwa walikuwa hatari balsa

Hivi kwa mfano wangekuwa ni magaidi na kuamua kulipua hayo mapipa ya mafuta si walikuwa washafanikiwa.
 
Nimetaza video hii zaidi ya mara tatu.kwanza huyu mtu anapesa ndefu maana mitambo na vifaa sio vya kitoto.pili inaonesha kuna mtu kachoma hii ishu,. inatakiwa wabaini mtandao wote.haiwezekani kila mwaka rais alikuwa anasema nchi haina kitu kumbe wengine ilikuwa ni neema kwao?🤔🤔
 
Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana
𝙺𝚎𝚜𝚒 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚑𝚞𝚠𝚎𝚣𝚒 𝚔𝚞𝚖𝚞𝚑𝚞𝚜𝚒𝚜𝚑𝚊 𝚖𝚠𝚎𝚗𝚍𝚊𝚣𝚊𝚔𝚎 𝚣𝚊𝚒𝚍𝚒 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚊𝚗𝚐𝚊𝚕𝚒𝚔𝚞𝚠𝚎𝚙𝚘 𝚊𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚐𝚎𝚎𝚗𝚍𝚊 𝚓𝚎𝚛𝚊 𝚖𝚊𝚕𝚒 𝚣𝚊𝚘 𝚔𝚝𝚊𝚒𝚏𝚒𝚜𝚑𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚊𝚌𝚌𝚘𝚞𝚗𝚝 𝚣𝚊𝚘 𝚔𝚞𝚏𝚞𝚗𝚐𝚒𝚠𝚊 𝚝𝚑𝚎𝚗 𝚊𝚗𝚐𝚎𝚔𝚞𝚓𝚊 𝙼𝙰𝙼𝙰 𝚑𝚞𝚛𝚞𝚖𝚊 𝚗𝚊 𝚔𝚞𝚊𝚖𝚞𝚛𝚞 𝙰/𝙲 𝚉𝚒𝚏𝚞𝚗𝚐𝚞𝚕𝚒𝚠𝚎 𝚗𝚊 𝚔𝚎𝚜𝚒 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚒𝚔𝚊𝚓𝚞𝚖𝚞𝚒𝚜𝚑𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚗𝚒 𝚔𝚎𝚜𝚒 𝚢𝚊 𝚔𝚞𝚋𝚊𝚖𝚋𝚒𝚔𝚒𝚣𝚠𝚊 𝚔𝚊𝚝𝚒𝚔𝚊 𝚣𝚒𝚕𝚎 147. 𝚒𝚗𝚐𝚎𝚜𝚘𝚖𝚊 148.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa Magufuli anahusikaje hapo. Hao si wezi Kama wezi wengine au kosa lake ni kule kupiga vita wizi kwa maslahi ya taifa. Lazima tukubali alijitahidi kwa uwezo wake ila haizuii ukweli kwamba kuna wachache walikuwepo bado ambao mmoja wapo ni hawa
 
Mimi najiuliza kama aliiba muda wote bila kujulikana au hasara kupatikana basi mafuta yana faida sana
Duh... Nchi hii!!! Mafuta yana faida sana! Manake gharama iliyo tumika kukamilisha huo wizi sio ndogo! Wangeweza kupata kifaa chao chenye security footage, nadhani ingekuwa bora zaidi.

Pili, kama wametoboa baada ya flow meter, ina maana kuna wahusika wa ndani ya bandari. Kwahiyo nao wachunguzwe!

List ni ndefu!

Sent from my S20 Ultra using JamiiForums mobile app
 
𝙺𝚎𝚜𝚒 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚑𝚞𝚠𝚎𝚣𝚒 𝚔𝚞𝚖𝚞𝚑𝚞𝚜𝚒𝚜𝚑𝚊 𝚖𝚠𝚎𝚗𝚍𝚊𝚣𝚊𝚔𝚎 𝚣𝚊𝚒𝚍𝚒 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚊𝚗𝚐𝚊𝚕𝚒𝚔𝚞𝚠𝚎𝚙𝚘 𝚊𝚘 𝚠𝚊𝚗𝚐𝚎𝚎𝚗𝚍𝚊 𝚓𝚎𝚛𝚊 𝚖𝚊𝚕𝚒 𝚣𝚊𝚘 𝚔𝚝𝚊𝚒𝚏𝚒𝚜𝚑𝚠𝚊 𝚗𝚊 𝚊𝚌𝚌𝚘𝚞𝚗𝚝 𝚣𝚊𝚘 𝚔𝚞𝚏𝚞𝚗𝚐𝚒𝚠𝚊 𝚝𝚑𝚎𝚗 𝚊𝚗𝚐𝚎𝚔𝚞𝚓𝚊 𝙼𝙰𝙼𝙰 𝚑𝚞𝚛𝚞𝚖𝚊 𝚗𝚊 𝚔𝚞𝚊𝚖𝚞𝚛𝚞 𝙰/𝙲 𝚉𝚒𝚏𝚞𝚗𝚐𝚞𝚕𝚒𝚠𝚎 𝚗𝚊 𝚔𝚎𝚜𝚒 𝚔𝚊𝚖𝚊 𝚑𝚒𝚢𝚘 𝚒𝚔𝚊𝚓𝚞𝚖𝚞𝚒𝚜𝚑𝚠𝚊 𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚗𝚒 𝚔𝚎𝚜𝚒 𝚢𝚊 𝚔𝚞𝚋𝚊𝚖𝚋𝚒𝚔𝚒𝚣𝚠𝚊 𝚔𝚊𝚝𝚒𝚔𝚊 𝚣𝚒𝚕𝚎 147. 𝚒𝚗𝚐𝚎𝚜𝚘𝚖𝚊 148.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida ya mwendazake alikuwa anatuficha mno ili asichafuke
 
Back
Top Bottom