Kigamboni: Watuhumiwa kutandaza mabomba na kuiba mafuta yanayoenda bandarini

Kigamboni: Watuhumiwa kutandaza mabomba na kuiba mafuta yanayoenda bandarini

Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana
Punguzeni chuki kwa marehemu.. Mumejazwa chuki dhidi yake kias cha kumchukia kwa kila kosa na makosa ambayo hausiki nayo..

Hapo mwendazake anahusika vipi? Mbona hata kipindi chake alishawahi kukamata watu kama hao na ndio hao mlikuwa mnalaumu kuwa anawabambikia kesi? Ndio haohao leo hii wanafunguliwa A/C zao na mnashangilia??

Lakn naamini Jpm sio bure, iko siku midomo na vidole hivi vinamuandika vibaya siku itafika vitakuja kuandika kulilia uwepo wake na midomo itakuja kutamka umuhimu wa uwepo wake.
 
Aisee

Sasa hii inahusiana vipi na Magufuli?

Hivi ukiwa chadema unakua taahira? Mbona watu wengi wanaomuamini Mbowe ni kama haziwatoshi?

By the way, huwezi kua na akili timamu ukawa mfuasi wa Mbowe na cham chake alichopewa kama zawadi ya birthday na baba mkwe wake.
 
Flowmeter zilizopo ni mbovu kama zinafanya kazi ni Mara chache Sana.
Kwa flowmeter zilizopo mtoto wa form 2 aliyeiva kwenye physics anaiba mafuta na hagunduliki.
 
Tatizo kubwa la mwendazake alikuwa anataka ale yeye tu ilhali wengine wanakufa na kwashakoo sasa kwa jinsi binadamu alivyo unapombana sana anatafuta njia mbadala ya kutokea, katika kipindi chake kulikua na chawa wake ambao uwepo wake ulikua unawanufaisha sana ndio maana hata walikua radhi kuua hata mtu aliyekua anampinga.

Ukweli ni kwamba aliharibu sana hili Taifa, Mungu wa mbinguni amesikia kilio cha watanzania akaamua kumchukua maana alikokua anaelekea kulikuwa siyoooo kabisaaaaa.
 
Yaaaan mwendazake aliwa fool wapumbavu na wajinga kwamba hakuna upigaji kumbe....kunaaa jamaa angu ni hawa wakula vitu aka unga..nmewahi kumuuliza mtapata wapi hiyooo ktu.. jamaaa alijibu hakunaaa kipindi unga unaingia kwa wingi kama zama hizi za mwendazake..
Tunakosea sana kuwaza kwamba Raisi ajue mpaka yanayoendelea mtaani,wapo watendaji wa kata,wenyeviti wa mtaa,n.k,hawa kazi yao nn?...yaani tunawaza raisi awe anapita kila nyumba kukagua yanayofanyika humo??tutakua wajinga na wapumbavu siku zote kwa kuwaza hivyo
 
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiwa na kamati ya Ulinzi na usalama wamebaini nyumba iliyopo mtaa wa Ugindoni iliyotandazwa mashine zinazotumika kuchimba visima vya maji lakini badala ya kuchimba chini kuelekea maji yalipo, wanachimba kuelekea usawa yalipo mabomba ya mafuta yanayotoka baharini kuelekea bandarini.

Mafuta hayo yanachukuliwa baada ya 'flow meter' kusoma na kutambulika yamepokelewa nchini lakini kabla ya kufika kituo cha mwisho ndipo mabomba hayo yanapoelekea.

Ndani ya nyumba hiyo kuna mashine na mipira ambayo inavuta mafuta na kujazwa. Nyumba hiyo ina ulinzi mkubwa na taarifa za awali zinasema muhusika amepangisha eneo hilo lenye kodi ya milioni 60 kwa mwaka huku akiwa amelipa miaka miwili na hakuna shughuli inayoendelea zaidi ya kisima ambacho mabomba yake yanaelekea baharini.

=========

Nchi ilitafunwa na watafunaji wakafichwa ila sio na serikali. Wafichuaji walizibwa midomo. Inasikitisha sana
Hili jambo liliwahi onekana kipindi cha mzee kikwete
 
Mwendazake kaliwa mno mno, miaka miwili imagine kama walikuwa wananyonya lita 20,000 kwa siku tu piga mara miaka miwili siku 760 inakuwa 20,000 times 760 = 15,200,000 Lita. Fanya kila lita bei ya kuuza 2000 unapata bei gani.

Piga mwenyewe uone watu walivyoondoka na mzigo wa uhakika!! Huyo jamaa sasa hivi atakuwa Congo ama Somalia.
 
Tatizo kubwa la mwendazake alikuwa anataka ale yeye tu ilhali wengine wanakufa na kwashakoo sasa kwa jinsi binadamu alivyo unapombana sana anatafuta njia mbadala ya kutokea, katika kipindi chake kulikua na chawa wake ambao uwepo wake ulikua unawanufaisha sana ndio maana hata walikua radhi kuua hata mtu aliyekua anampinga.

Ukweli ni kwamba aliharibu sana hili Taifa, Mungu wa mbinguni amesikia kilio cha watanzania akaamua kumchukua maana alikokua anaelekea kulikuwa siyoooo kabisaaaaa.
Hivi ili Mtanzania aishi Maisha Mazuri ni lazima awe mpigaji!? Maana hao Watanzania wenye Maisha Mazuri ndiyo Wapigaji wakuu! Wengine wanatupiga hadi kwenye posho za vikao huko Serekalini!! Inaonekana Kama Maisha ya straight hayalipi, ndiyo maana ukitaka Maisha Mazuri lazima uwe mpigaji!!
 
Back
Top Bottom