Kigezo cha ajira kwa waalimu iwe GPA

Kigezo cha ajira kwa waalimu iwe GPA

Mathayo Christopher

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
413
Reaction score
289
Kwako mheshimiwa waziri wa OR-TAMISEMI napenda wizara yako itambue kuwa mfumo wa waalimu Tanzania wanaandaliwa kwa mitihani na kufaulu kwa Madaraja tofauti hivyo wizara yako kupendekeza kigezo cha kujitolea kama kipaumbele cha kuajiri hamtatenda khaki kwa waliotuma maombi.

Mosi,uongozi awamu ya Magufuli walituambia tujiajiri.

Pili,kuna waalimu wangi wamefundisha na wanafundisha shule za binafsi kwa mda mrefu lakini kwenye fomu za maombi wameweka shule za umma kwa mantiki hiyo kigezo cha uzoefu hakina maana.

Maoni yangu tumieni kigezo vinavyoeleweka kama vile GPA, mwaka wa kuhitimu na kwa waalimu wa arts mnaokusudia kuwaajiri shule za msingi tumieni kigezo cha matokeo Yao ya kidato cha nne kwenye masomo ya Hisabati na biology, physics na chemistry ili muwaajiri waalimu Wenye uwezo wa kufundisha masomo yote.
 
GPA haina tija yoyote ile kwenye fani ya ualimu wa sekondari na msingi. Kinachotakiwa huko ni uwezo sahihi wa mwalimu wa kumfundisha mwanafunzi na kuelewa. Hizo GPA mngeendelea kuzitumia kuombea Uasistant tutorio kule chuo kikuu.
 
GPA haina tija yoyote ile kwenye fani ya ualimu. Kinachotakiwa ni uwezo wa kumfundisha mwanafunzi na kuelewa. Hizo GPA mngeendelea kuzitumia kuombea Uasistant tutorio kule chuo kikuu.
GPA ni kigezo muhimu na hiyo ndio msingi wa measurement and evaluation na ndio mfumo tunaotumia kwenye elimu ndio maana mwenye four kidato cha nne hana sifa ya kusoma kidato cha tano
 
Kada zingine kama Afya, Engineering, Law, pamoja na hiyo wanabatizwa na moto wa namna hii hata kama uwe na GPA ya 5. Hapo angalau wanapikwa kwa kiasi chache ingawa mapungufu hayakosekani.

Ila mtindo huo kwa walimu haupo hadi chokochoko za kujitolea zimeanza kujitokeza, mfumo wa enzi za JK urudishwe tukate mzizi wa fitina hii
 
GPA haina tija yoyote ile kwenye fani ya ualimu wa sekondari na msingi. Kinachotakiwa huko ni uwezo sahihi wa mwalimu wa kumfundisha mwanafunzi na kuelewa. Hizo GPA mngeendelea kuzitumia kuombea Uasistant tutorio kule chuo kikuu.
I doubt about your education level.
GPA haina tija kwenye ualimu wa sekondari na msingi!
Rubbish.
 
I doubt about your education level.
GPA haina tija kwenye ualimu wa sekondari na msingi!
Rubbish.
Bado unanyonya! Ukikua utanielewa nilichomaanisha. Mimi naongelea walimu wewe unaongelea elimu! Jinga kabisa wewe.
 
St.John University ukiwa rais wa wanafunzi lazima utunukiwe na GPA ya 5.0. Kwa hiyo msicheze na ole Sabaya.
 
Back
Top Bottom