Kigezo cha ajira kwa waalimu iwe GPA

Kigezo cha ajira kwa waalimu iwe GPA

Inategemea umesoma chuo gani? C I liana alama 40 au 50 ndo uanzie hapo
 
Achen nongwa ndugu zangu,.h mshahara yenyewe kiduchu Sana,..Bado mnataka mfanye certification sijui kuwe na bodi ...zote za Nini..mwachen mwalimu ale chake Bila bughudha
 
Kada zingine kama Afya, Engineering, Law, pamoja na hiyo wanabatizwa na moto wa namna hii hata kama uwe na GPA ya 5. Hapo angalau wanapikwa kwa kiasi chache ingawa mapungufu hayakosekani.

Ila mtindo huo kwa walimu haupo hadi chokochoko za kujitolea zimeanza kujitokeza, mfumo wa enzi za JK urudishwe tukate mzizi wa fitina hii
Sawa mkuu nimekuelewa vizuri sana. Sasa mkuu, mbona walimu hawafanyiwi interview kama waajiriwa wa kada zingine?
 
Hata ya afya walikuwa hawafanyiwi usahili isipokuwa tu kwa baadhi wanaoajiriwa na mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Afya.

Ila hao watu wa Afya ni lazima uwe na leseni(usajili kamili kutoka baraza husika).

Hizi kada(Ualimu na Afya) zina umuhimu wa haraka na Mona kwa moja kwa jamii ndio maana walikuwa wanaajiriwa moja kwa moja bila usahili.

Serikali pekee ndio haiwafanyii walimu wa Msingi na Sekondari usahili nadhani kwa sababu niliyoitaja hapo juu, sambamba na hilo Hawa hawahitaji leseni(kusajiliwa) sijui sababu nini.

Mimi naona bora wasajiliwe(Wawe na leseni) hata kama hawafanyiwi usahili, hizi leseni lazima zipatikane kwa mfumo wa kada zingine.

Mfumo wa upatikanaji leseni utawezesha kuimarisha maadili na miiko ya kazi, pia mtu ukiwa na leseni utailinda ili usiweze kufutiwa pindi ukifanya makosa kwani ukifutiwa leseni hautaweza kuajiriwa tena
 
Hakuna cha GPA ualimu ni zaidi ya akili za darasani. Cha muhimu ni kufanyiwa interview kama wafanyavyo shule za private.
 
Sawa mkuu nimekuelewa vizuri sana. Sasa mkuu, mbona walimu hawafanyiwi interview kama waajiriwa wa kada zingine?
Wanafanya lakini inategemeana unaajiriwa wapi.

Kama shule inahitaji walimu 10 kukidhi mahitaji yake na waombaji wakawa 200 lazima usaili utafanyika.

Lakini serikalini mpaka sasa walimu hata ukiajiri wote waliopo bado uhaba utakuwepo, sasa hapo utafanya interview ya nini kama siyo upuuzi na kupoteza muda.
 
Which GPA? Fafanua. Kama Ni hii ya ya good papupichi award na pacha mwenzake CPA( chawa protocol award) hapana kwa kweli
 
Wanafanya lakini inategemeana unaajiriwa wapi.

Kama shule inahitaji walimu 10 kukidhi mahitaji yake na waombaji wakawa 200 lazima usaili utafanyika.

Lakini serikalini mpaka sasa walimu hata ukiajiri wote waliopo bado uhaba utakuwepo, sasa hapo utafanya interview ya nini kama siyo upuuzi na kupoteza muda.
Kwa hiyo uhaba wa walimu ndio unaifanya serikali iajiri hata wale vilaza kwa kuogopa kuwafanyia interview?
 
Mimi naona bora wasajiliwe(Wawe na leseni) hata kama hawafanyiwi usahili, hizi leseni lazima zipatikane kwa mfumo wa kada zingine.

Mfumo wa upatikanaji leseni utawezesha kuimarisha maadili na miiko ya kazi, pia mtu ukiwa na leseni utailinda ili usiweze kufutiwa pindi ukifanya makosa kwani ukifutiwa leseni hautaweza kuajiriwa tena
Ushauri mzuri sana huu
 
Kwa hiyo uhaba wa walimu ndio unaifanya serikali iajiri hata wale vilaza kwa kuogopa kuwafanyia interview?
Kwahiyo unamaanisha vyuo vinazalisha vilaza ?

Mtu anasoma miaka 2 au 3 mpaka ana graduate, anatunukiwa astashahada, stashahada au shahada unawezaje kusema ni kilaza.

Tena ni mwalimu anaeenda kufundisha ngazi ambayo yete aliifaulu.

Target ya interviews huwa ni kuchuja watu ili upate TOP TALENTS kama hizo talents zenyewe zipo.

Hapa ni kanuni za uchumi tu, huwezi kukataa kazi eti kwakuwa ina malipo kidogo wakati ambao hata shilingi 100 kwako ina umuhimu.
 
Kuna wakati kulikuwa na vugu vugu la kuanzishwa kwa bodi ya elimu.

Lakini walimu wakivyoona jinsi itakavyowabana, CWT wakaanza kuipinga tena.

Mwisho wa siku hizi bodi na leseni ni ulaji tu wa watu na kuongeza makato kwenye mishahara ya watumishi ndio maana sometimes wanaziogopa.
 
Kwahiyo unamaanisha vyuo vinazalisha vilaza ?

Mtu anasoma miaka 2 au 3 mpaka ana graduate, anatunukiwa astashahada, stashahada au shahada unawezaje kusema ni kilaza.

Tena ni mwalimu anaeenda kufundisha ngazi ambayo yete aliifaulu.

Target ya interviews huwa ni kuchuja watu ili upate TOP TALENTS kama hizo talents zenyewe zipo.
Kama hauamini kuna walimu vilaza hiyo dhana yako ya TOP TALENT umeitoa wapi? Kwanini utafute hao TOP wakati wote wamehitimu elimu inayolingana?
 
Kuna wakati kulikuwa na vugu vugu la kuanzishwa kwa bodi ya elimu.

Lakini walimu wakivyoona jinsi itakavyowabana, CWT wakaanza kuipinga tena.

Mwisho wa siku hizi bodi na leseni ni ulaji tu wa watu na kuongeza makato kwenye mishahara ya watumishi ndio maana sometimes wanaziogopa.
Makato inatakiwa iwe wakati wa kuhuisha leseni mwisho wa mwaka tu kama zilivyo bodi zingine.
 
Kama hauamini kuna walimu vilaza hiyo dhana yako ya TOP TALENT umeitoa wapi? Kwanini utafute hao TOP wakati wote wamehitimu elimu inayolingana?
Sisemi ni vilaza. Hapa namaanisha uwezo unatofautiana.

Na mtu kuwa na uwezo wa kawaida haimaanishi kuwa hawezi kutimiza majukumu yake.

Ishtoshe elimu yetu imewekewa mipaka na wakufunzi. Ili uonekane una akili inabidi ufikiri vile lecturer anavyofikiri.

Vinginevyo huwezi kufaulu mitihani yake kwa kuandika tofauti na alivyokwambia.
 
Back
Top Bottom