Tony Laurent
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 5,606
- 7,032
Kuna watu/walimu wana vipaji vya kufundisha hadi kuwafanya wanafunzi waelewe vizuri wanachofundishwa pamoja na kuwa na GPA ya chini. Kuwa na GPA kubwa si kigezo cha kuwa mwalimu mzuri/ mahiri. Hata katika ajira za kawaida, unaweza kukuta mtu ana GPA kubwa, lakini anazidiwa uwezo wa kiutendaji na mwenye GPA ya chini.GPA haina tija yoyote ile kwenye fani ya ualimu wa sekondari na msingi. Kinachotakiwa huko ni uwezo sahihi wa mwalimu wa kumfundisha mwanafunzi na kuelewa. Hizo GPA mngeendelea kuzitumia kuombea Uasistant tutorio kule chuo kikuu.