Kigezo cha kuwa Sheikh (Shehe) ni nini?

Sheikh ni nani?

Hili neno linatafsirika kilugha na kiistilahi/kisheria. Kilugha lina maana ni mtu mzima ambaye kuanzia miaka 50+. Huku Tanzania tunamuita au tunatamka Mzee.

Kiistilahi Sheikh lina maana ni mjuzi aliyebobea elimu ya dini ambaye jamii inamtegemea kupata mwongozo kutoka kwake. Na sheikh anakuwa ni mwenye fani zote kwa maana kwenye dini ya kiislamu kuna fani au taaluma 9+...

Hivyo sheikh amebobea kwenye fani zote. Mpaka kuwa sheikh inakuchukua miaka mingi sana ni sawa sawa kama mtu aanze nursery mpaka chuo kikuu.

Hivyo kuna masheikh na masheikh majina kwa maana Tanzania tumeshazoea kuitana hivyo kwa kila kiongozi wa dini ya kiislamu kwani kuna wengine ni maustadhi na si masheik.
 
Hizo nchi baada ya kuhitimu sharia umekuwa mpiga madufu au ni sheikh?
 
Hata wanawake?
 
asante. Nimejua tatizo linakoanzia.
 
Wakristo mara nyingi wamekuwa wakijifanya wasomi.

Wanaenda mbali zaidi kwa kuwadharau waislamu kwamba ni 'wazee wa mdarasa' hawana elimu.

Cha ajabu usomi wao upo mdomoni tu huku nchi ikizidi kufubaa na wao wasomi wakiangalia tu.
1. Rais ni mwenzenu
2. PM ni mwenzenu
3. Rais zenji ni mwenzenu
4.mawaziri wengi ni wenu
5. Marais wastaafu wote ni Dini yenu

Wakristo watafanya Nini zaidi ya kuongea
 
Ee
1. Rais ni mwenzenu
2. PM ni mwenzenu
3. Rais zenji ni mwenzenu
4.mawaziri wengi ni wenu
5. Marais wastaafu wote ni Dini yenu

Wakristo watafanya Nini zaidi ya kuongea
Eeh eeh imekuwaje tena hao wote ni waislamu na tunaambiwa waislamu shule hamna?

Au kuna sehemu nyie wenzetu wasomi mlijisahau mkawaachia wasio wasomi kushika nafasi?
 
Angalau wewe umejibu nusu ya swali, Sasa mwambie mleta mada, hizo hatua za kusomea mpaka kuwa sheikh,maana umetaja tu ulinganifu wa nursery to chuo kikuu, yeye anataka umtajie hatua ya 1 mpaka mwisho

NB
Mimi hapa ni Kama kibatala tu mahakamani
 
Ee

Eeh eeh imekuwaje tena hao wote ni waislamu na tunaambiwa waislamu shule hamna?

Au kuna sehemu nyie wenzetu wasomi mlijisahau mkawaachia wasio wasomi kushika nafasi?
Mimi hapa kwenye huu uzi sitaki kutoa maoni yangu binafsi Niko hapa kuhoji tu Mkuu, ukitoa maoni yako nakuhoji utetee hoja yako basi, Dini yangu Mimi ni kimbanguist ,Mimi sio dini hiyo unayodhani
 
Kuna jamaa hapa Magomeni baba yake alitoa eneo la kujenga msikiti. Kwahiyo yeye anapata mgao wa mapato ya msikiti. Hapa anaitwa Shekhe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…