Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Naona watu fulani wanapiga sana ngonjera kuhsu rais huyu kupendwa na wanyonge na mwingine kutopendwa na wanyonge, siju kama ni kweli
Lakini hebu tuwaangalie hawa wanyonge ni watu gani.. Wanyonge wanasemwa kuwa ni watu wa kipato kidogo wasio na ajira rasmi wala elimu kubwa, hata hapa JF wanasema mitandao kama ya Facebook ina wanyonge wengi ambao wanamkubali kiongozi fulani na kumkataa mwingine
Sasa ukipima uelewa wa hawa wanyonge kuhusu maswala ya siasa, utawala na uchumi ndio utajua kuwa hawa watu maoni yao hayana maana yoyote kuhusu rais bora ama asiye bora ni yupi
Ukiwauliza kuhusu ripoti ya CAG hawajui lolote, ukiwauliza majukumu ya bunge hawajui, ukiwauliza kuhusu uchumi wa kati ni nini hawajui lolote, yaani hawaelewi chochote kuhusu mihimili na mifumo ya serikakali
Na kutokana na uelewa finyu wanyonge hawa ni rahisi sana kulaghaiwa na wanasiasa, mfano kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 Chadema walijipatia sifa na umaarufu sana kutoka kwa wanyonge kwa kuwaambia kuhusu ufisadi wa Lowassa, lakini Chadema walipobadilisha gia angani na kumsimamisha Lowassa kwenye urais, Wanyonge waliwakubali tena Chadema na kufikia kudeki barabara na kumpa Lowassa kura nyingi sana
Miaka ya hivi karibuni kulitokea kiongozi mmoja akafanikiwa sana kuwalaghai wanyonge, na ndio mtaji mkubwa unaotumika na wanaomtetea huyo kiongozi
Wanyonge wanapenda kuambiwa tu nitawapa vitu vya bure, nitawafilisi matajiri, nitrawaruhusu kufanya biashara popote, nitawaruhusu kuchunga mifugo popote n.k bila kuelewa hasara za hivyo vitu kwa mapana
hivi sasa crisis ya dunia na vitu kupanda bei imewapa nafasi nzuri wanasiasa laghai kuwatapeli wanyonge, utasikia mtandoni wakisema ingekuwa flani angekuwepo vitu visingepanda na wanyonge kutokana na kutoelewa wanawaamini
Sisemi wanyonge wakandamizwe ila sio kipimo cha ubora wa Rais