Kigezo cha Rais bora hakipimwi na wanyonge, Wanyonge hawaelewi chochote kuhusu siasa wala uchumi

Mnaojiona mna "akili" ndio mnaongoza hili taifa tangu tupate uhuru, mmelifanyia nini taifa cha maana?
 
Labda kweli hawana wanachoelewa hawana maana yoyote lakini kura zao zina maana sana.
Ndio wanaoamua nani awe Raisi wa nchi.. nani awe Mbunge au Diwani.
Hao tabaka maalum la wenyenacho kielimu na kipato ni wachache sana.

Ila tu msije kulalamika mmeibiwa kura.

Ndio maana kuna utafiti ulifanywa wapumbavu kama wewe wakafurahia eti oooh kuna chama kinapendwa na wakijijini wasionacho wasoelimika wazee na wanawake..
Wakijisifu kupendwa na wasomi vijana na wenyenacho bila kuwa hilo ni kundi dogo kwenye kura halitoshi
 
Lini wamesema hawatapeleka?

ATC inaenda Geita mara mbili kila week na wanapata abiria wengi tu.

Halafu huo ujinga wao umeupima kwa lipi?

What a trash!

Geita sio Chato, na kwenda huko haimaanishi kuwa ni route yenye faida.
 
Raisi hutokana na wanyonge ambao asilimia kubwa ndio majority Tanzania

Tanzania toka tupate uhuru maraisi wote na viongozi wa juu kama mawaziri wakuu nk ni kutoka familia maskini .mno

Tatizo lililoanza kujitokeza ni kuwa hawa waliotoka familia maskini wakashika nyadhifa za juu wakapata pesa kwa njia halali na haramu sasa wamegeuka kujiona na wao ni class ya juu sehemu ya high class sio sehemu ya wanyonge tena na kuanza kuponda wanyonge na maskini na wasio nacho

Mleta mada ni mmojawapo wa hilo kundi la "maskini akipata matako hulia mbwata"
 

Ingekuwa kura ndio zinaamua nani awe rais hapa nchini, leo hii ccm Ingekuwa kwenye kaburi moja na KANU ya Kenya. Na siku ccm itakubali kutegemea kura hizo za huko vijijini ndio itageuka kuwa historia. Ongelea sifa nyingine lakini sio box la kura maana chaguzi mbili tu zinatosha kuweka hicho chama cha kizazi kilichopita pembeni.
 

Siku za nyuma wakati ccm ilipokuwa na ushawishi, rais alikuwa anapatikana kwa kura. Lakini toka uchaguzi wa 2010 kizazi kilipobadilika na ccm kupoteza ushawishi, rais anapitishwa na kigenge kidogo kiitwacho system.
 
Tafakari maana ya serikali, chanzo cha kuwa na serikali, mamlaka ya serikali yanatokana na nini.
 
Hiyo mentality ya unyonge ikutoke kbs! Yaan mna praise hiyo kitu tangu mkiwa mnatawala awamu ya tano. Una praise vp unyonge eti kama kasifa flan hivi, achen mentality za umasikin
 
Danganyanane huko mitandaoni lakini tulioko vijijini tunajua jinsi CCM inakubalika. Huku hakuna upinzani. Ni chini ya 30% na kumbuka 70% ya population wako vijijini.
Uje uchaguzi wa kusimamiwa na malaika bado itaongoza vijijini
 
Kamarada, asante sana kwa ufafanuzi mzuri na mfupi. Kazi njema
 
Kujiita 'Rais wa wanyonge' hakuna maana ya kuwa Rais wa wanyonge. Ni kama mtu kujiita muadilifu hakuna maana ya kuwa muadilifu. Ila wanyonge wakimwita kiongozi wa nchi 'Rais wa wanyonge' inaweza kuwa na hiyo maana au watu wakisema 'x ni muadilifu' inaweza kuwa kweli maana wanaona matendo na maneno yake yana huo mwelekeo.
 
Ogopa sana hilo tabaka.

Siku wakichoka hapatakalika na utatamani uombe nafasi ya kutubu lakini haitakuwepo.

Ni hatari sana kuendelea kumkandamiza maskini kwa muda mrefu bila kumpa pumzi.
 
Danganyanane huko mitandaoni lakini tulioko vijijini tunajua jinsi CCM inakubalika. Huku hakuna upinzani. Ni chini ya 30% na kumbuka 70% ya population wako vijijini.
Uje uchaguzi wa kusimamiwa na malaika bado itaongoza vijijini
Wewe hata kijijini hupajui,unalelewa sebuleni na shemeji waulize wanakijiji licha ya uhaba wa mvua lakini wameshindwa kununua mbolea kwa sababu ya kupanda bei?
 
Tulia unapotaka kuupeleka ujumbe. Kama huna utulivu hutaeleweka kwani utaandika kama mtu mzima anayeogea nje mchana kweupe
 
Awamu zote kulikuwa na wizi
So imehalalasha wizi wenu wa kutisha wa awamu yenu pendwa ya kinyonge? Wapuuzi sana walituita wanyonge ili watuibie. Nashukuru Mungu nilipinga kuitwa mnyonge mpaka siku alipotwaliwa aliyekuwa anatuita wanyonge.
 
Kueleweshwa siyo ukandamizaji wala siyo dharau ndugu. Mbona unafika mbali haraka? Tulia uuelewe ujumbe
 
Huna akili timamu.

KANU ni jina tu kama ilivyo JUBILEE na ODM, Leo Kuna Azimio na UDA lakini watu Ni WALE WALE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…