Kigezo cha Rais bora hakipimwi na wanyonge, Wanyonge hawaelewi chochote kuhusu siasa wala uchumi

Kwani kuna tofauti na hapa kwetu? watu huko vijijini wanatumia maji na mifugo tena maji yenyewe ni tope tupu.
Makampuni ya kimataifa ndio hayo serikali hii ya ccm imekuwa ikizunguka duniani kuyaleta yawezekeze hapa nchini, huenda hujui mambo hayo.
Watanzania wenyewe sometimes wanapenda. Nazungumzia hili kwasababu Mimi siyo Mwanasiasa wala MASLAHI ya kisiasa.

Mimi nimewahi kwenda Morogoro, Kilosa nikakuta watu wanaishi mbali sana Porini.

Na wanahamia huko, wanaanzisha miji mipya halafu wanataka serikali ipeleke HUDUMA ZA AFYA, SHULE, WATUMISHI, UMEME na MAJI.

Ukiwaambia waishi sehemu ambazo Zina huduma tayari HAWATAKI.

Nyerere aliwahi kutumia mabavu kwenye hili mpaka Leo analaumiwa.

Na hivi vimji vipya kila siku vinaanzishwa.

Tembea ujionee.
 
Naona watu fulani wanapiga sana ngonjera kuhsu rais huyu kupendwa na wanyonge na mwingine kutopendwa na wanyonge, siju kama ni kweli

Lakini hebu tuwaangalie hawa wanyonge ni watu gani.. Wanyonge wanasemwa kuwa ni watu wa kipato kidogo wasio na ajira rasmi wala elimu kubwa, hata hapa JF wanasema mitandao kama ya Facebook ina wanyonge wengi ambao wanamkubali kiongozi fulani na kumkataa mwingine

Sasa ukipima uelewa wa hawa wanyonge kuhusu maswala ya siasa, utawala na uchumi ndio utajua kuwa hawa watu maoni yao hayana maana yoyote kuhusu rais bora ama asiye bora ni yupi

Ukiwauliza kuhusu ripoti ya CAG hawajui lolote, ukiwauliza majukumu ya bunge hawajui, ukiwauliza kuhusu uchumi wa kati ni nini hawajui lolote, yaani hawaelewi chochote kuhusu mihimili na mifumo ya serikakali

Na kutokana na uelewa finyu wanyonge hawa ni rahisi sana kulaghaiwa na wanasiasa, mfano kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 Chadema walijipatia sifa na umaarufu sana kutoka kwa wanyonge kwa kuwaambia kuhusu ufisadi wa Lowassa, lakini Chadema walipobadilisha gia angani na kumsimamisha Lowassa kwenye urais, Wanyonge waliwakubali tena Chadema na kufikia kudeki barabara na kumpa Lowassa kura nyingi sana

Miaka ya hivi karibuni kulitokea kiongozi mmoja akafanikiwa sana kuwalaghai wanyonge, na ndio mtaji mkubwa unaotumika na wanaomtetea huyo kiongozi

Wanyonge wanapenda kuambiwa tu nitawapa vitu vya bure, nitawafilisi matajiri, nitrawaruhusu kufanya biashara popote, nitawaruhusu kuchunga mifugo popote n.k bila kuelewa hasara za hivyo vitu kwa mapana

hivi sasa crisis ya dunia na vitu kupanda bei imewapa nafasi nzuri wanasiasa laghai kuwatapeli wanyonge, utasikia mtandoni wakisema ingekuwa flani angekuwepo vitu visingepanda na wanyonge kutokana na kutoelewa wanawaamini

Sisemi wanyonge wakandamizwe ila sio kipimo cha ubora wa Rais
Unyonge,kwenye Siasa ni subjective, inategemea na muktadha..hata wewekwenye mazingira Fulani unaweza kufanywa mnyinge na Mwanasiasa!
Mbona Prof.Kabudi,na wengineo wengi tu walifanywa wanyonge na JPM
Au wananchi wote wa Mtera Si Wanyonge Kwa Lusinde
Tafakari!
 
So imehalalasha wizi wenu wa kutisha wa awamu yenu pendwa ya kinyonge? Wapuuzi sana walituita wanyonge ili watuibie. Nashukuru Mungu nilipinga kuitwa mnyonge mpaka siku alipotwaliwa aliyekuwa anatuita wanyonge.
Hata Mungu wa mbinguni anajua wanyonge wapo,(Zaburi 41:1)Heri amkumbukaye myonge Bwana atamwokoa siku ya tabu)wewe ni nani kupinga neno hili
 
Mfano population imeongezeka hawana Ardhi wala lkipato chochote utawaacha wafe na njaa wakati eneo la kulima lipo hiyo mbuga Utaona wanyama muhimu kuliko uhaini wao?
Misitu na hifadhi ni muhimu kwa kutunza mazingira, ikolojia, na maji kwa vizazi vijavyo na vya sasa,

Kuruhusu watu wavamie misitu itakuwa ni kuwaangamiza bila wao kujua
 
Cha kushanhaza, kura za wanyonge wakati wa uchaguzi zina thamani sawa na PHD holders. Na hamzikatai
 
Kuwajali wanyonge ni sifa ya kipekee haswa unapokuwa unapanda kimaisha na kupata utajiri. Ni sifa ya ubinadamu.
Naona hutaki kuelewa, sijasema anayewajali wanyonge vs asiyewajali

Hapa ni kuhusu anaysifiwa na wanyonge anaweza akawa laghai tu ila wanyonge wakawa hawajui

Mfano anaweza akaja kiongozi akasema bei ya sukari iwe 1000 kwa kilo huyu kwa kipimo cha wanyonge ni rais bora ila kiuhalisia atasababisha sukari kuadimika mtaani sababu hakuna mfanyabiashara atakayeuza
 
Uko sahihi, kwenda kwenye hiyo route hakumaanishi kuna faida. Wanaweza wasifunge kwa sababu za kisiasa lakini hiyo route ni baadhi ya maeneo yatakayozidi kulipa hilo shirika hasara. Rejea mashirika mengi ya umma yalivyokufa kutokana na hasara kwani yaliendeshwa kisiasa nani si kwa nguvu ya soko.
Mkuu umefanya uchambuzi kuhusu hiyo route? Unaweza kuwa sahihi lakini JF nako siasa nyingi
 
Yapo mengi aliyafanya uzuri video huwa hazizeeki, zipo nyingi youtube.

Hakuyafanya kwa hisani bali ni wajibu wake au yoyote aliye katika cheo cha urais, na malipo sio kufanyia ukatili wasiokubaliana na mitazamo yake kisa amesimamia ujenzi wa miradi fulani.
 
Mkuu umefanya uchambuzi kuhusu hiyo route? Unaweza kuwa sahihi lakini JF nako siasa nyingi

Ripoti ya CAG imeweka hilo wazi. CAG sio jf ndugu, huku jf na social media nyingine ni platform za mijadala ya kinachojiri kwenye jamii.
 
Naona hutaki kuelewa, sijasema anayewajali wanyonge vs asiyewajali

Hapa ni kuhusu anaysifiwa na wanyonge anaweza akawa laghai tu ila wanyonge wakawa hawajui

Mfano anaweza akaja kiongozi akasema bei ya sukari iwe 1000 kwa kilo huyu kwa kipimo cha wanyonge ni rais bora ila kiuhalisia atasababisha sukari kuadimika mtaani sababu hakuna mfanyabiashara atakayeuza
Anayewajali wanyonge akitumia lugha ya utapeli ni lazima wanyonge hao watamuonyesha aina ya ulaghai wake hadharani.

Anayewajali wanyonge ambaye aliishi maisha yao akiwa kijana au mtoto pia watamuelewa kwani ataongea lugha ya kwao kutoka moyoni mwake.
 
Ni wazo zuri ila Tusifike huko,jambo la muhimu kwanza ni Katiba Bora bila shaka itapunguza role ya wajinga kwenye kufanya maamuzi ambayo mwisho wa siku inakuwa ni costful sio tuu kwao bali kwa Nchi..
Hakuna ujinga kama kuamini eti katiba bora itatuondolea matatizo.
Chukua Afrika Kusini na Marekani nchi mbili tunazozipigia mfano wa kuwa na Katiba bora.... Wanamatatizo mengine makubwa kuliko sisi
1. Ubaguzi ni mkubwa na una madhara kuliko chochote afadhali Tanzania
2. Kuna Mauaji ya holela tena wako kwenye 10 bora duniani na wahalifu hawakamatwi kuliko hata Tanzania
3. Polisi wanaua na kunyanyasa kuliko Tanzania
4. Afrika kusini wana matatizo makubwa ya Ajira kuliko hata Tanzania
5. Pale Kenya our model kuna ukabila ufisadi rushwa wizi na uhalifu kuliko Tanzania wenye Katiba mbovu
Marekani wenye Tume huru na Katiba bora duniani wameingia kwenye matatizo makubwa ya uchaguzi na watu wanasema kuna wizi toka enzi za Al Gore na Bush mpaka hapa kwa Biden na Trump.

Kwangu mimi Katiba mpya ni matakwa ya wanasiasa na sisi wenzangu na mie tunaimbishwa kama Kasuku wimbo tusioujua
 
Wewe toa ujinga wako,nimesema Katiba Bora itapunguza baadhi ya shida hasa za kimfumo.
 
Naona watu fulani wanapiga sana ngonjera kuhsu rais huyu kupendwa na wanyonge na mwingine kutopendwa na wanyonge, siju kama ni kweli

Lakini hebu tuwaangalie hawa wanyonge ni watu gani.. Wanyonge wanasemwa kuwa ni watu wa kipato kidogo wasio na ajira rasmi wala elimu kubwa, hata hapa JF wanasema mitandao kama ya Facebook ina wanyonge wengi ambao wanamkubali kiongozi fulani na kumkataa mwingine

Sasa ukipima uelewa wa hawa wanyonge kuhusu maswala ya siasa, utawala na uchumi ndio utajua kuwa hawa watu maoni yao hayana maana yoyote kuhusu rais bora ama asiye bora ni yupi

Ukiwauliza kuhusu ripoti ya CAG hawajui lolote, ukiwauliza majukumu ya bunge hawajui, ukiwauliza kuhusu uchumi wa kati ni nini hawajui lolote, yaani hawaelewi chochote kuhusu mihimili na mifumo ya serikakali

Na kutokana na uelewa finyu wanyonge hawa ni rahisi sana kulaghaiwa na wanasiasa, mfano kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015 Chadema walijipatia sifa na umaarufu sana kutoka kwa wanyonge kwa kuwaambia kuhusu ufisadi wa Lowassa, lakini Chadema walipobadilisha gia angani na kumsimamisha Lowassa kwenye urais, Wanyonge waliwakubali tena Chadema na kufikia kudeki barabara na kumpa Lowassa kura nyingi sana

Miaka ya hivi karibuni kulitokea kiongozi mmoja akafanikiwa sana kuwalaghai wanyonge, na ndio mtaji mkubwa unaotumika na wanaomtetea huyo kiongozi

Wanyonge wanapenda kuambiwa tu nitawapa vitu vya bure, nitawafilisi matajiri, nitrawaruhusu kufanya biashara popote, nitawaruhusu kuchunga mifugo popote n.k bila kuelewa hasara za hivyo vitu kwa mapana

hivi sasa crisis ya dunia na vitu kupanda bei imewapa nafasi nzuri wanasiasa laghai kuwatapeli wanyonge, utasikia mtandoni wakisema ingekuwa flani angekuwepo vitu visingepanda na wanyonge kutokana na kutoelewa wanawaamini

Sisemi wanyonge wakandamizwe ila sio kipimo cha ubora wa Rais
Takataka.
 
Ripoti ya CAG imeweka hilo wazi. CAG sio jf ndugu, huku jf na social media nyingine ni platform za mijadala ya kinachojiri kwenye jamii.
Hakuzungumzia safari za ATCL bali pay back ya investment ambayo haihusiani na ATCL ila operations za uwanja. Issue ni investment kubwa ya uwanja bila kuangalia requirements za watumiaji. Kulikuwa na sababu ya kuweka 3 km runway wakati traffic ni ya Bombardier? Yaani 1.8 or 2 km can do.
 
Hakuna ujinga kama kuamini eti katiba bora itatuondolea matatizo.
Chukua Afrika Kusini na Marekani nchi mbili tunazozipigia mfano wa kuwa na Katiba bora.... Wanamatatizo mengine makubwa kuliko sisi
1. Ubaguzi ni mkubwa na una madhara kuliko chochote afadhali Tanzania
2. Kuna Mauaji ya holela tena wako kwenye 10 bora duniani na wahalifu hawakamatwi kuliko hata Tanzania
3. Polisi wanaua na kunyanyasa kuliko Tanzania
4. Afrika kusini wana matatizo makubwa ya Ajira kuliko hata Tanzania
5. Pale Kenya our model kuna ukabila ufisadi rushwa wizi na uhalifu kuliko Tanzania wenye Katiba mbovu
Marekani wenye Tume huru na Katiba bora duniani wameingia kwenye matatizo makubwa ya uchaguzi na watu wanasema kuna wizi toka enzi za Al Gore na Bush mpaka hapa kwa Biden na Trump.

Kwangu mimi Katiba mpya ni matakwa ya wanasiasa na sisi wenzangu na mie tunaimbishwa kama Kasuku wimbo tusioujua
Ona Kenya, wenye Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi.

Ambao kila siku ndio mifano.

Sometimes watu wameaminishwa hata vitu visivyokuwepo.

Hivi hii nchi inawatu werevu kabisa? Labda uniambie wezi ndio unahisi labda watakua werevu.
Nchi haiendelei miaka yote ipo nchi masikini halafu tunaambiwa kuna tabaka la watu wanajiita wenye akili?
Tuache utani hii nchi inakila kitu inakosa watu tu basi.
Watu wa kuwa viongozi tunakosa, watu wakuwa wananchi tunakosa pia ni shida sana kupata walau watu wenye akili sahihi.
 
Hata Mungu wa mbinguni anajua wanyonge wapo,(Zaburi 41:1)Heri amkumbukaye myonge Bwana atamwokoa siku ya tabu)wewe ni nani kupinga neno hili
Tafsiri ya Biblia sio hiyo yako. Kwamfano wanaposema Heri Masikini wa Roho maana Ufalme wa Mbinguni ni wao we jifanye masikini oune kama Mbinguni utaenda. Kasome utajiri wa Eliya Mtishbi ndo utajua Mungu hawezi kutuma watu ambao ni masikini na Wanyonge. Biblia sio ilani ya CCM ndugu yangu. Unahitaji tafakuru kubwa sana kuijua na kuielewa.
 
Back
Top Bottom