PreGE2025 POTOSHI Kigogo avujisha video ya wizi wa kura ulivyokuwa ukifanyika 2020

PreGE2025 POTOSHI Kigogo avujisha video ya wizi wa kura ulivyokuwa ukifanyika 2020

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Kigogo anadai video hii inaonesha jinsi afisa wa uchaguzi walivyokuwa wakichagua viongozi katika vituo vya kupigia kura huku ulinzi ukiendelea nje kwa lengo la kuhakikisha hakuna Mwananchi atakayeshuhudia

1744209463898.png
 
Tunachokijua
Taarifa sahihihi ni chanzo chenye kuchochea maamuzi sahihi katika jamii, pia husaidia kuepusha taharuki zinazoweza kuibuka kutokana na uwepo wa taarifa zisizo za kweli. Baadhi ya watu kwa kujua ama kutokujua wanaweza kufanya upotoshaji unaosababisha kugeuzwa kwa uhalisia wa jambo husika huku wengine wakifanya ili kutimiza madhumuni yao. Mathalani maudhui yanayohusisha uchaguzi au katika kipindi cha uchaguzi, kunakuwa na ongezeko la taarifa zisizo sahihi zinazolenga kupotosha wananchi kuhusu wagombea wa kisiasa, sera zao, michakato ya uchauzi na hata utendaji wa serikali.

Kumekuwapo na kipande cha video kinachomuonesha mtu mmoja akiweka alama kwenye karatasi inayoonekana kuwa ni ya kupigia kura, kikidaiwa kuwa ni kutoaka Tanzania Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kwamba ni afisa wa uchaguzi walivyokuwa wakichagua viongozi katika vituo vya kupigia kura.


Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search ulibaini kuwa video hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza mtandaoni mnamo tarehe 1 Novemba, 2020.

Aidha video iliambatanishwa na maneno (Caption) yaliyo katika lugha ya kifaransa, "Présidentielle en Côte d'Ivoire : Les preuves d'un bourrage d'urne" ambayo kwa lugha ya kiswahili yametafsiriwa, "Uchaguzi wa Urais nchini Côte d'Ivoire: Ushahidi wa kujazwa kwa masanduku ya kura"

Pia video hiyo ilichapishwa Novemba 03, 2020 katika mtandao wa X, ikiambatana na ujumbe unaosomeka "Scrutin présidentiel en Côte d’Ivoire .Véritable mascarade. Regardez par vous même." ambao kwa kiswahili umetafsiriwa, "Uchaguzi wa Urais nchini Côte d’Ivoire: Sarakasi halisi. Tazama mwenyewe."

Hivyo Video imebainika kuwa ni kutoka nchini Ivory Coast wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Oktoba 31, 2020. Aidha moja kati ya vigezo vilivyobainika katika ni pamoja na Karatasi ya kupigia kura inayoonekana ambayo inafanana na karatasi halisi zilizokuwa zikitumika katika upigaji wa kura katika uchaguzi huo.

Picha ya karatasi za kupigia kura
screenshot-2025-04-09-121348-png.3297628


Picha ya karatasi ya kupigia kura inayoonekana katika video inayopotoshwa
screenshot-2025-04-09-121656-png.3297630
Back
Top Bottom