Kigogo sio mtu wa kumuita Tundu Lissu mshamba, akemewe

Kigogo sio mtu wa kumuita Tundu Lissu mshamba, akemewe

Rais huyu kasema Katiba isubiri apange uçhumi kwanza. Mwendazake alisema Katiba mpya siyo ahadi yake ya kampeni. Hakuna mtu alimuuliza mpaka anakufa.

Huyu ana siku 120 kwenye ofisi kiungwana kabisa kaomba muda. Kwa ushauri wangu tungemuacha hadi mwaka mmoja uishe ndipo tumuulize tena.

Kitendo cha kujifanya tunaijua nchi kuliko yeye na wakati Mbowe na Lissu walishiriki kula Mabilioni ya Bunge la Katiba mwaka 2014 na wasitupatie Katiba siyo FAIR
Leo umekula nini? Mbona unatema madini tu.
 
Mshamba ni nani?

Mshamba ni yule anayejificha nyuma ya kibodi na kuwashambulia wengine au anapambana kwa kujitokeza na kuongea bila kupepesa macho kama Tundu Lissu anavyofanya?

Mshamba ni nani yule aliyeanza kupigania haki toka akiwa shule ya msingi, Sekondari, JKT na kuendelea au yule aliyeanza kujificha nyuma ya kibodi baada ya serikali kuvunja nyumba yake Kimara?

Mshamba ni yupi? Ambaye anaweza kumtukana kila mtu kisa tu kamkosoa au ni yule anayetumia hoja kujibu hoja za wale wote wanaomshambulia?.


Kuwablock watu wanaomkosoa kwenye post zake sio ushamba? Yaani mtu anapokukosoa ni adui yako wewe ni malaika Mbona Tundu Lissu hata Siro hajawai kumtukana ila uwa anamjibu kwa hoja?

Kwangu Mimi mshamba ni yule asiyejua anafanya nini, Anataka nini, Anapataje lini na wapi? Kumtukana kila mtu ni ushamba sana.

Imagine mtu anamtukana na kumzalilisha mtoto kama Zuchu au Nandy watu ambao hawaelewi maana ya siasa ni nini baada ya kuwapa elimu ya uraia wewe unatoka kuwatukana tu and you don't care!

Kwa taarifa Kigogo ni mtoto mdogo mno kwenye siasa za nchi hii harakati zako hazijafikisha hata miaka 10 wakati Tundu Lissu ameanza harakati miaka ya 1990 wewe jiulize ulikuwa wapi na ulikuwa unafanya nini?

Kigogo awaulize waliokuwepo kwenye utawala wa Mkapa walivyopambana na Tundu Lissu na Lissu kushinda miaka huyo hata twitter ilikuwa hakuna.

Waulize waliojaribu kumhonga Tundu Lissu kwenye utawala wa Mkapa ili aache kuwatetea watu waliokuwa wanatolewa maeneo ya migodi kwa nguvu kwenye mikoa ya Shinyanga, Mpanda, Tabota, Geita, Mara na Kagera watakupa majibu.

Lissu angekuwa mshamba si angechukua tu pesa za wazungu na kuachana na kuwatetea wananchi?

Tundu lissu miaka yote amekuwa akifanya kazi field tena akiwa sambamba na mke wake akiwa front line kabisa nafikiri hata mwaka Jana alipokuja kufanya kampeni bado mliona alivyokuwa akisumbuana na Police kule Nyamongo na kwingine.

Sasa wewe ndugu yetu unamuita mtu mshamba ambaye yupo ulaya kwa kufanyiwa operation zaidi ya 25 baada ya kupigwa risasi halafu wewe upo ulaya nyuma ya kibodi.

Afadhari Lissu hata akifa leo Mungu akipenda historia ya Maisha yake tayari kashaimaliza historia aliyonayo ni kubwa mno.

Washamba ujificha, Washamba upanic, Washamba ujifanya wanajua kila kitu ili wasikosolewe, Washamba uzusha, hakika Washamba wakikosa ajenda ya kusimamia uwa wanaona kila binadamu ni adui wa maendeleo yao.

Wanaharakati wote duniani uwa hawapambani na mtu uwa wanapambana na mifumo, Jifunze kwa wanaharakati kama wakina Martin Luther King JR na wengine walipambana na mifumo na wakaja kushinda hata kama walikuwa hawapo tena.

Yaani unamtukana Tundu Lissu halafu unamsifia Mbowe? Wakati Mbowe na Tundu Lissu ufahamu hata walikutana vipi?

Kama wewe ni mwanamageuzi kweli njoo na I'd yako original na uje front line uongoze maandamano unayoyapigia kelele, njoo uanzishe chama ukiendeshe kiwe kikubwa kama angalau ACT.

Lissu mageuzi na mapambano aliyoyafanya yanatosha kabisa hata leo akistaafu siasa ila najiuliza kigogo ameshafanya kitu gani zaidi ya kutukana watu?

Mambo ya kuita watu washamba ni ushamba pia.
Hajakosea chochote Kigogo ametathmini siasa za chadema na kuona ni za kishamba sana, Chadema wanajidai wana watu milioni 7 hadi 8 wameshindwa kuonyesha nguvu yao kwa kiongozi wao mkuu ambaye yupo magerezani kwa propaganda, Lakini Tundu Lissu amesahau siku aliporudi pale Airpot Mbowe alikuja kumpokea kwa magongo leo unabaki nje na kurusha rusha maneno kupitia clip za mitandaoni kuliko kuja kuangalia namna yeye na wanachama wa Chadema kuonyesha nguvu ya pamoja kumtoa Mwenyekiti wao magerezani.,

Juzi nimemsikia hata shangazi Fatma Karume akimtusi Tundu lissu kwa kumwambia hana adabu wala heshima., yote haya ni kwa sababu Chadema ni chama dhaifu sana, chadema wanashindwa ni hata watu laki tatu kule Zanzibar, Tundu Lissu anaporoja kila leo chadema ndio chama kikuu cha upinzani kila leo lakini hatuoni ukuu wowote wa upinzani wao.

Nchi kama Tanzania ambayo imekubuhu kwenye udikteta haiwezi kujali chochote kwa vipindi anavyoandaa Tundu Lissu siju aljazeera na DW na sijui mikutano uchwara huko ulalaya, haiwezi kuathiri chochote kwa hawa watu it is good for nothing.,

Maalim seif hakuwahi kukimbia nchi kwa vyovote vile, Lissu anatakiwa arejee as soon as possible siasa za kiafrika ni mapambano ya ana kwa ana otherwise muache kujitangaza chadema ndio chama kikuu cha upinzani sijui muna wanachama milioni 8 for nothing.
 
..wangempa miezi sita, halafu wakaaza harakati zao wangeambiwa kwanini hawakumpa mwaka mmoja.

..wangempa mwaka mmoja, wangeambiwa kwanini hawajampa miaka miwili, visingizio na lawama dhidi ya wapinzani haziwezi kuisha.
Kwahiyo wakaaamua wamlazimishe.

Sisi tukawasihi na kuwataka wasiwe wapumbavu, wao wakabisha na wakaamua kuwa wapumbavu.

Kazi kwao, kazi na iendelee..
 
Hajakosea chochote Kigogo ametathmini siasa za chadema na kuona ni za kishamba sana, Chadema wanajidai wana watu milioni 7 hadi 8 wameshindwa kuonyesha nguvu yao kwa kiongozi wao mkuu ambaye yupo magerezani kwa propaganda, Lakini Tundu Lissu amesahau siku aliporudi pale Airpot Mbowe alikuja kumpokea kwa magongo leo unabaki nje na kurusha rusha maneno kupitia clip za mitandaoni kuliko kuja kuangalia namna yeye na wanachama wa Chadema kuonyesha nguvu ya pamoja kumtoa Mwenyekiti wao magerezani.,

Juzi nimemsikia hata shangazi Fatma Karume akimtusi Tundu lissu kwa kumwambia hana adabu wala heshima., yote haya ni kwa sababu Chadema ni chama dhaifu sana, chadema wanashindwa ni hata watu laki tatu kule Zanzibar, Tundu Lissu anaporoja kila leo chadema ndio chama kikuu cha upinzani kila leo lakini hatuoni ukuu wowote wa upinzani wao.

Nchi kama Tanzania ambayo imekubuhu kwenye udikteta haiwezi kujali chochote kwa vipindi anavyoandaa Tundu Lissu siju aljazeera na DW na sijui mikutano uchwara huko ulalaya, haiwezi kuathiri chochote kwa hawa watu it is good for nothing.,

Maalim seif hakuwahi kukimbia nchi kwa vyovote vile, Lissu anatakiwa arejee as soon as possible siasa za kiafrika ni mapambano ya ana kwa ana otherwise muache kujitangaza chadema ndio chama kikuu cha upinzani sijui muna wanachama milioni 8 for nothing.
Sasa kama chadema imekufa mnahangaika nayo ya nini ?

Chama kilichokufa unaweza pambana nacho?


Njoo field ucheki mziki uliopo yaani kanda ya ziwa 2025 ccm itafutwa kabisa.

Hakuna mtanzania anaweza kuandamana wewe unatoka watu waandamane wavunjwe miguu? Wakati kigogo mwenyewe yupo nyuma ya keyboard kuhamasisha vurugu?

Hatuingii kwenye mtego huo tutapambana na uchaguzi ujao ndio mtajua sasa nguvu ya umma ilipo endeleeni kujidanganya.
 
Hawataki kukosolewa wanataka wasifiwe hata kwa mambo ya kijinga wanayoamua. Tanzania kwanza vyama baadaye.
Nyie mnaosema Tanzania kwanza uwa nawashangaa sana tasisi yenu hiyo uwa ina ofisi wapi? Inafanya nini?

Mbona matozo nyie hamkutoka barabarani? Au nyie tozo haziwahusu?
 
Chadema bhana 😂😂😂 mchawi yupo katikati yenu wenyewe
 
Hiyo ni akaunt ya watu wa mfumo waliochukia mirija yao kufungwa na hayati magufuli
 
Hawamjui yule,labda. Wamejulia twitter
January? January huyu huyu? Hizo akili kapata lini? Au zile tweet ndio zinakuongopea?
Nakukumbusha tu leo tunamlaumu mwigulu kwa kuleta tozo kwenye miamala
Ila hata January makamba ndio alieleta Sheria ya kipumbavu na ya kinyonyaji ya cyber crime act mwanzoni mwa 2015
 
Kwahiyo wakaaamua wamlazimishe.

Sisi tukawasihi na kuwataka wasiwe wapumbavu, wao wakabisha na wakaamua kuwa wapumbavu.

Kazi kwao, kazi na iendelee..

..mnawasingizia ili kupata sababu ya kuwapiga na kuwasweka magerezani.

..chadema wamemlazimisha Rais namna gani wakati hawakumfuata ikulu, au kuingilia taratibu wala ratiba ya shughuli za Raisi?
 
Umeandika ukweli sahihi mbowe siku zote alikuwaga na busara na hekima ila licha ya kusikilizwa na kuheshimiwa sijui mbowe ni kichaa gani kilimpanda na kutaka kumfanya Samia aonekane dhaifu ona sasa yuko jela pekee yake. CDM kwa Samia walitumia wrong approach kiasi mama hasikilizii yoyote na CDM itapotea wasipobadilika na kuendeleza harakati bila good calculations, sio siri napenda mabadiliko ila mbowe na CDM walikosa vision ya jinsi ya ku deal na Samia, nchi hii inahitaji upinzani makini usio na mihemko kusaidia taifa.
Ukweli 100%

Yaani alishikilia nafasi ya Urais wa nchi na kutoa Matamko na Maamuzi, hilo likamcost tofauti na alivyokuwa na subira na uvumilivu zamani.
 
Huyo kigogo anayejiita shemasi ni 'mpuuzi' flani kajificha kwa mzungu, Tutamlipua tu soon.

Kwanza hana hata hadhi ya kumlinganisha na TL, hata Mdude hamfikii, wenzake wako 'battlefield' yeye kazi yake kupika majungu na umbea na ku'insult watu, halafu anajiita whistleblower.

Akili kubwa gani unaingizwa Chaka na Jasusi proCCM Chahali.
Kajificha kwa Mzungu yupi?
 
Ni madikteta, hawataki hata kukosolewa..Wlimtukana Lowassa miaka 8, then wakaja kumpokea na kumjaza sifa zote, ajitokeze hapa mwanachadema kuutetea uamuzi wa kumchukua Lowassa 2015
Walisema Siasa haina rafiki wa kudumu wala Adui wa kudumu

Siasa bana.....! [emoji23]
 
Kukamatwa ni sehemu ya harakati za kisiasa. Ni aida kwa anayekamatwa historia imeprove hivyo
Mbona wananchi wafuasi wa Chadema hawataki kuandamana kama walivyoahidi kwa kuogopa kukamatwa?

Waandamane tu hata wakikamatwa ni sehemu ya harakati za siasa
 
Back
Top Bottom