Kigoma kuna upungufu mkubwa sana wa wanaume, ni rahisi dada kuokota hela Kigoma kuliko kupata mchumba

Utalishwa mawese mixer kuogea gwanji.
Atakula numbu na migebuka hadi aseme poo...ila Kasulu kuna karanga zao zile wanazisaga daah nilikua nazinunua nyingi nikisikia hamu naanza kuzila kavu kavu maisha ya Kasulu yalikua safi sana...wikend unaenda Kigoma Town..unakutana na watoto wazuri wa Kimanyema, Kikongomani, unakula good time basi unarudi zako bush...
 
Ngoja mabaharia tukaweke kambi Kigoma kama tulivyokubaliana hakuna kurudi na mwanamke.
 
Mabinti wa Kiarabu wapo? Na vipi mahari zao si kubwa sana
 
Kweli
Kweli Kama unatoka Mkoa tofauti na Kigoma na ukaoa na kuishi Kigoma utapata taabu sana! Utakuwa nikama umeoa Ukoo mzima kila Ndugu wa Mwanamke akija kwako jiandae kuombwa pesa akitaka kuondoka!


Dawa ndogo tu...anzisha mashamba maduka na viwanda vya sembe wapange huko....
 
Hahaha..Nyie wenye mapenzi ya ubondia huko ndio pana wafaa aisee....
 
Naupenda sana mkoa huu..
Watu smart na wenye vipaji wanatoka huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…