KIGOMA: Madereva waandamana, wafunga barabara wataka nauli zipande

KIGOMA: Madereva waandamana, wafunga barabara wataka nauli zipande

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baadhi ya madereva wa Bajaji katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameandamana na kufunga barabara kushinikiza kupandishwa kwa bei za usafiri kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

Walifanya mgomo huo wakitaka mamlaka ziwaruhusu wapandishe nauli. Kwa sasa usafiri wa kuchangi abiria mmoja analipa Sh 500 wanataka iwe Sh 1,000.

Lita moja ya petroli Mkoani humo inauzwa kwa Tsh 3,093 na Diseli Sh 2,924, mabadiliko ambayo wanadai ni changamoto kwao. Jeshi la Polisi liliingilia na kuwatuliza kwa amani wakiwataka kufikisha malalamiko yao kwenye mamlaka husika jambo.



#JamiiForums


Chanzo: Dar24
 
Kwa wenzetu wanaojitambua👇👏👏👏
7UID.jpeg
IMG_20220404_100611_745.jpg
IMG_20220402_184504_432.jpg
AARD4K.jpeg
Kwa Mitanzania ambayo haijitambui baada ya kuruhusu vibaka kupora chaguzi na kushika dola 👇🐒🐒🐒
022040141919.jpg
16493135505330.jpg
 
Wanaandamana kushinikiza bei ya nauli ipande badala la kushusha bei ya mafuta,ni akili za wapi hizi?
Mafuta yamepanda, we unategemea wao watabaki kulipisha nauli ya zamani
Lazima nauli zipande

Ova
 
duh aiseee toka 500 hadi 1500 parefu
 
Hapa ni kupaki kushinikiza nauli ipande ili tuisome namba vizuri.
Tunasubiri kuanzia wiki ijayo hapa DAR watalianzisha Tu...
Daladala zinazopitia kilwa road wanalia na FOLENI ambayo inapelekea kukosa hesabu ya kilasiku SASA ukijumlisha na bei ya mafuta ni kimbembe hichoo
 
sasa si wauze bajaji hizo kwan lazima waendelee kusafirisha ila bongo bhn😂😂
 
Back
Top Bottom