KIGOMA: Madereva waandamana, wafunga barabara wataka nauli zipande

KIGOMA: Madereva waandamana, wafunga barabara wataka nauli zipande

Kupanda wanafurahia ila wakiambiwa washushe wanakuwa wazito kupunguza bei.
 
Baadhi ya madereva wa Bajaji katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameandamana na kufunga barabara kushinikiza kupandishwa kwa bei za usafiri kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

Walifanya mgomo huo wakitaka mamlaka ziwaruhusu wapandishe nauli. Kwa sasa usafiri wa kuchangi abiria mmoja analipa Sh 500 wanataka iwe Sh 1,000.

Lita moja ya petroli Mkoani humo inauzwa kwa Tsh 3,093 na Diseli Sh 2,924, mabadiliko ambayo wanadai ni changamoto kwao. Jeshi la Polisi liliingilia na kuwatuliza kwa amani wakiwataka kufikisha malalamiko yao kwenye mamlaka husika jambo.

#JamiiForums

Chanzo: Dar24
Bei ya mafuta iongezeke kwa sh.300 afu wao waongeze nauli kutoka jero hadi 1000 ,,hii haipo..

Nauli ya bajaji isizidi 700
 
Wanaandamana kushinikiza bei ya nauli ipande badala la kushusha bei ya mafuta,ni akili za wapi hizi?
Nawaona kama wasiojua Biashara, Acha wafikishe 1000 waone daladala zitakavyochukua nafasi. Mafuta yamepanda Kwa 320/- per litre, wewe unapndisha 500 Kwa abiria hii akili ya nchi gani hii?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
1649345160697.png

Daa, hakika !.
 
nauli zikipanda hapo Kigoma watu watarudia usafiri wa mababu zao(nyungo)
 
Back
Top Bottom